PPF, NSSF, PSPF, etc. wanakimbilia miradi yenye rushwa

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,009
2,169
Huenda wewe kama mimi umeshajiuliza ni kwa nini mifuko hii ya hifadhi ya jamii inavyo kimbilia miradi ya ujenzi kwa miaka ya hivi karibuni. Kila mfuko unakimbilia kujenga majengo ya vioo.

Miradi hii haina faida kwa wanachama wa mifuko hii na bahati mbaya kabisa pia haipitishwi na wanachama wenyewe. Bodi za mifuko ndo wanaofanya madudu haya. Walioko ktk bodi za mifuko hii wamekuwa kama kamati ya olimpiki. Wanabaki humo kwa miaka mingi bila kutoka, sababu kubwa ikiwa ni kulinda uchafu ulioko ndani ya mifuko hii ili isitoke nje ya bodi.

Kwa ujumla miradi ya ujenzi imekuwa ni fasheni kwa sababu moja kubwa, kwamba sekta ya ujenzi ni moja ya sekata zinazoongoza kwa rushwa. Ni rahisi wakurugenzi wa mifuko hii kupata 10% kutoka miradi hii ya ujenzi.

Sasa tunambiwa takribani kila mfuko uko taabani kifedha. Hayo ndo matokeo na bado Wakurugenzi bado wanapanga jinsi ya kuanzisha miradi mingine ya ujenzi!

Kifuatacho ni wastaafu kukosa pesheni au serikali kupunguza viwango vya pesheni.
 
Back
Top Bottom