PPF nipo katika wote scheme mwezi wa sita sasa nafuatilia pesa zangu napigwa calendar tu

live on

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
480
1,000
Wakati wana tuhamasisha tujiunge katika hi scheme walitupa maneno mazuri sana na kitu kibwa walichokuwa wanatuambia ni kuwa siku yoyote utakapo amua kuchukua pesa zako utapewa bila ya usumbufu wowote laki sasa imekuwa kinyume chake

Miezi sita iliyopita nilienda pale nikasema nataka pesa zangu nikapewa form nikaijaza baada ya siku mbuli nikairudisha nikambiwa nikae siku 60 kama haitaingia pesa kwangu ndio niende

Zilipopita siku 60 nikaenda sikupata jibu la maana nikaka mwezi mmoja nikaenda tena wakaniambia ngoja wawasiliane na Dodoma maana makao makuu yamehamia huko nikasubiri mwezi mwingine nikaenda tena bado tu story ni zile zile

Nahisi kama nimepigwa hivi lakini najiuliza hivi kweli taasisi ya serikali inaweza kuwapiga changa la macho wananchi wake
Nikienda tena wakinizingua naenda kuwashitaki mahakamani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom