PPF kuweni wawazi katika kutangaza nafasi za ajira

Miwatamu

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
1,450
487
PPF wametangaza nafasi mbalimbali za ajira tangu mwanzoni mwa mwezi huu na tyarehe ya mwisho wa maombi kama sikosei ni 16/6/2013.

Kubwa zaidi wameeleza kuwa maombi yote yatumwe kwa njia ya mtandao baada ya muombaji kuwa amejisajili katika mtandao wao. lakina hata baada ya kufanya hivyo pindi unapojaribu ku log in, unaambiwa kuwa password siyo!

Hii ndiyo nini sasa?

Kinachoonekana hapa ni kuwa wameweka tangazo hilo kama ushahidi tu huku tayari wakiwa na watu wao. Acheni hizo.
Kama nafasi ni kwa ajili ya watanzania wote kwa nini hizo application form hazifunguki?? Inamaana mmeziwekea ka-uzibe fulani.

Nasema tena acheni hizo kwani ajira ni kwa watanzania wote.

Pia naomba watanzania wote tusaidiane kukemea hili ikiwezekana litangazwe upya na kwa uwazi zaidi.

NAWASILISHA.
 
pole mkuu...endelea kujaribu coz mi nimefanikiwa kutuma na haikunisumbua sana labda kama sasa inasumbua sana...usichoke kujaribu...
 
ingekuwa poa kama ndugu Miwatamu ungepeleka complaints zako kwenye ofisi husika!maana watanzania tunaunafiki wakuzungumza pembeni!tunakuwa waoga kusema ukweli!
 
Last edited by a moderator:
Hata mimi pia nilituma maombi yangu kiulaiini bila hata usumbufu. labda endelea kujaribu maana pia watumaji wakiwa wengi kwa wakati mmoja network inakuwa busy. jaribu hata usiku mkuu. together tunawakilisha.
 
IT hao jamaa hawana wapo wapo tu, kuna jamaa wamewachukua kama casula labour tokea mwaka 2008 kwa hiyo kila baada ya miezi mitatu wanarenew mkataba,so usishangae hata kidogo kama page haifunguki
 
IT hao jamaa hawana wapo wapo tu, kuna jamaa wamewachukua kama casula labour tokea mwaka 2008 kwa hiyo kila baada ya miezi mitatu wanarenew mkataba,so usishangae hata kidogo kama page haifunguki

Wakuu tusaidieni na sisi hilo tangazo la ajira maana huku kijijin ni ngumu sana kupata maissue kama hizi wakuu, tunaomba sana mtusaidie kabla ya deadline
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom