Powercef: Tujihadhari na matumizi yasiyo sahihi ya dawa zote kwa ujumla

verses fountain

Senior Member
Sep 30, 2018
155
191
Habari za humu wakuu.

Niende moja kwa moja kwenye mada.
Powercef ni nini?
Nina imani katika pitapita zetu iwe au isiwe ndani ya sehemu za kupata huduma za afya tumewahi kusikia neno POWERCEF.

Powercef ni antibiotic (inapambana na bacteria) yenye uwezo wa kuondoa ama kuua viumbe vidogo katika mwili (microorganism) wa aina nyingi (broad spectrum antibiotic ambayo huua gram negative na gram positive organism)kwa mara moja tofauti na narrow spectrum antibiotics.(ambayo huua gram negative peke yake au gram positive organism peke yake ila sio vyote kwa pamoja).

Hii hupewa mtu kupitia sindano ya mshipa kwenye vein(intravenous injection),sindano katika msuli (intramuscular injection),na kuwekewa kama drip(intravenous infusion) kwa ajili ya kutibu magonjwa yanayosababishwa na bacteria

Powercef ni aina ya antibiotic inayopaswa kutumika pale tu ambapo dawa zingine zitumikazo kwa ugonjwa husika zinakuwa zimeshindwa kufanya kazi kwani katika makundi ya dawa kuna madaraja ama line za madawa kuanzia daraja la kwanza,pili na tatu (first line ,second line na third line drug).first line na second line drugs zinapokuwa na uwezo wa kati(intermediate) wa kuua vijidudu vya ugonjwa inabidi kuongeza dozi ya dawa mfano kutoka 20 miligrams kuwa 40 miligrams. Ikishindkana kusaidia kutibu hapo ndipo baada ya kufanya testing ya kujua kama vijidudu hivyo ni sugu kwa dawa Fulani ndipo wataidhinisha dawa yenye nguvu zaidi ambazo ni daraja la tatu (third line drugs)

Sababu za dawa kuleta usugu na kushindwa kusaidia kuponesha ni zipi?
• Matumizi ya dawa muda mrefu (longer drug dosage duration)
• Ufuasi mbovu/usio mzuri wa dawa/Kutokuzingatia dozi ya dawa kama ilivyoelekezwa na mhudumu wa afya kwa makusudi au kutokujua.(poor adherence to dose given)
.
Faida na Madhara ya kutumia Powercef ni yapi?
Powercef ina faida ya kuua vijidudu vya aina tofautitofauti hivyo huleta ahueni kwa atakayechomwa sindano ya antibiotic hiyo.Lakini madhara yake pia kama ilivyo kwa madawa mengine ni pamoja na

Madhara ya muda mfupi ya POWERCEF
Kuharisha,kuwashwa,kichefuchefu,kutapika, ,maumivu ya kichwa,maumivu au uvimbe kwenye ulimi,kutokwa jasho,upungufu wa damu(anaemia) na kizunguzungu ambapo mgonjwa anatakiwa kuwa na mtu karibu endapo atachomwa sindano na kuhitaji kuondoka hashauriwi kutumia mashine(operate machines) ama kuendesha gari.

Madhara ya muda mrefu ya POWERCEF
Madhara ya powercef yanakuja pale ambapo mgonjwa anachomwa sindano na baada ya kujiskia afadhali anaamua kuacha kukamilisha dozi kama inavyotakiwa na baada ya hapo akiumwa tena anaenda kuchoma kwa mara nyingine baada ya muda kupita alipochoma ya kwanza.Usugu wa ugonjwa dhidi ya dawa huanza kukua na baadae huwa na madhara makubwa zaidi kiafya kwa mgonjwa huja pale ambapo anaumwa sana(critically ill) na dawa hiyo haiwezi kumsaidia kupona.

Ushauri wangu
Kwa wahudumu wa afya: Tumepewa dhamana ya kusaidia kuondoa matatizo ya kiafya kwa wanadamu kwa kila mmoja kulingana na kada yake na kwa jinsi ambayo Mungu ametubariki kuwa pale tulipo.Kazi yoyote tunayofanya hapa duniani ambayo ni halali ni wito wa Mungu ambao tuna wajibu wa kuutii.

Tusifanye kazi kumfurahisha mtu bali kutimiza wito kwa moyo mmoja kwani ipo siku tutatoa hesabu kwa matendo yetu.

Tuache tamaa,tuwe wakweli na tusifanye kazi kwa mazoea ili kupata chochote kitu kwa sababu matokeo yake ni mabaya kuliko tunavyodhani.

Ni muhimu kufahamu dozi sahihi kwa mtu sahihi kulingana na historia ya kiafya na dawa alizowahi kutumia (medical history and drug history),na majibu ya maabara kama yapo (laboratory results).Kama imeidhinishwa kutumika powercef ni muhimu kuhakikisha mgonjwa anasisitizwa umuhimu wa kutokuacha dozi njiani kwa faida yake mwenyewe kwani akiacha njiani baadae akipata ugonjwa uwezekano wa kupona unazidi kupungua.

Kwa wahitaji wa huduma za kiafya:Ni muhimu kufahamu madhara ya matumizi ya dawa tofauti na mpangilio aliopewa na mhudumu wa afya hasa yanayotokana na ufuasi mbovu wa dawa(poor adherence) ikiwemo usugu kwa madawa ambao ni hatari sana kwa afya yao.

NB:Kutokuchukua hatua kuangazia tatizo hili kutaiweka sekta ya afya kwa ujumla katika wakati mgumu pale ambapo watu watakuwa wagonjwa na dawa za kuwatibu zitakaposhindwa kufanya kazi kwa sababu ya kukosa elimu kwa wagonjwa wenyewe na kwa upande wa wahudumu wa afya kushindwa kusimamia nafasi zetu kwa uaminifu na kushindwa kutoa maelezo muhimu na sahihi ya tiba tunazowapa wagonjwa.

Kwa wanaofahamu zaidi wataongeza na kupunguza pale inapostahili.

Mnakaribishwa kufanya hivyo kwa faida ya wote.
 
Back
Top Bottom