Povu la Emmanuel Mbasha baada ya madam Flora kuzindua kitabu chenye jina 'Siri za Flora Mbasha'

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
267,884
1,093,923
BAADA ya mwanamuziki wa Nyimbo za Injili Bongo, Flora Mbasha kusambaza kitabu alichokipa jina la Siri za Flora Mbasha kilichoanika ‘mabaya’ ya aliyekuwa mumewe, Emmanuel Mbasha, mumewe huyo ameibuka na ‘kumchana’ vibaya mwimbaji huyo na kusema hafai kuwa mke.

Flora alikiachia kitabu hicho hivi karibuni ambapo pamoja na mambo mengine aliyopitia kwenye maisha yake na Mbasha, alieleza namna ambavyo mumewe huyo wa zamani alivyokuwa akimtesa na hata kumuingilia kwa nguvu akiwa kwenye siku zake.

Akizungumza na mwanahabari wetu katika ofisi za gazeti hili, Bamaga- Mwenge jijini Dar, Mbasha alianza kwa kueleza masikitiko yake juu ya kitabu hicho kwa kusema anashindwa kuelewa mume wa sasa wa Flora, Daud Kusekwa anajisikiaje pale Flora anapomzungumzia mara kwa mara.

“Yaani unajua watu wengine sijui wapoje bwana. Hivi kweli wewe hata huyo mwanaume wake anajisikiaje kuona mkewe ananiongelea kila wakati? Ni kukosa adabu, kwa nini wasifanye maisha yao? “Kweli mwanamke aliyefunzwa, akafunzika anaanzaje kumuongelea mwanaume wake wa zamani? Yaani kwangu mimi mwanamke wa aina hiyo anapoteza sifa ya kuwa mke,” alisema Mbasha.

Mbasha akizidi kutema cheche mbele ya kinasa sauti cha Amani, alisema kuwa, aliamua kukaa kimya baada ya kupitia mambo mazito na mwanamuziki huyo ambayo kamwe hataki kuyasikia wala kurudi nyuma.

“Ametaka talaka mahakamani, tumeachana na mimi sikutaka tena hata kumzungumzia, lakini yeye kutwa amekuwa akinizungumzia. Halafu kwanza unamzungumziaje mtu ambaye mlishaachana? Mtu ambaye kwanza hana hata habari na wewe, anafanya maisha yake mengine, huu kama siyo ujinga ni nini?”

Alihoji Mbasha. Kama hiyo haitoshi, Mbasha alizidi kumwaga mboga kwa kusema kuwa, siku zote sikio la kufa huwa halisikii dawa kwani kitendo anachokifanya Flora cha kumzungumzia yeye kama zilipendwa wake, alishakifanya kwake kwa mwanaume mwingine.

“Kifupi ni kwamba tabia ni kama ngozi, huwezi kuibadili. Wewe unaona sasa hivi anavyoelezea mambo aliyokuwa akiyafanya na mimi na kuongeza uongo wake, alishanifanyia hata mimi wakati nimemuoa. “Yaani yule mwanamke sijui bana, Mungu amsaidie. Yaani kwanza wakati mimi naanza kumfuatilia, huwezi kuamini, alikuwa na mwanaume mwingine.
 
Hawa nao,kwani inakatazwa kufanya tendo la ndoa mtu akiwa kwenye siku zake?Si anajisafisha vizuri tu jamani then anampa mmewe?kuna ubaya gani kwani.Hawa nao sijui wakoje ndo nini kutoleana mambo yenu mliyokuwa mkifanya mkiwa mnapendana?Si waangalie yaliyopo?Yaliyopita wayaache huko huko kwenye ndoa yao ya zamani.
 
mi mwenyewe namchana ex wangu vibaya mno. yaani acha kabisa acha flora ateme cheche.taka lini ex akasifiwa?

Kumchana ex wako inaonyesha jinsi gani amekushinda/amekuachia doa.Kama wewe ndo ulimuacha huwezi kumzungumzia maana hana maana wala thamani kwenye maisha yako.Ukiendelea kumzungunmzia ex wako ina maana kwamba bado yumo moyoni mwako,kama siyo unampenda basi itakuwa kuna mahali alikukomesha.
 
Huyo mwanamke anataka kufaidika na huu mgogoro, kibinadamu ni ujinga lakini kiujasiriamali hii ni akili ya juu kabisa ya kutambua fursa.
 
Hawa nao,kwani inakatazwa kufanya tendo la ndoa mtu akiwa kwenye siku zake?Si anajisafisha vizuri tu jamani then anampa mmewe?kuna ubaya gani kwani.Hawa nao sijui wakoje ndo nini kutoleana mambo yenu mliyokuwa mkifanya mkiwa mnapendana?Si waangalie yaliyopo?Yaliyopita wayaache huko huko kwenye ndoa yao ya zamani.
alikuwa anamlala akiwa p? nasikia alimla na tigo pia
 
Hawa nao,kwani inakatazwa kufanya tendo la ndoa mtu akiwa kwenye siku zake?Si anajisafisha vizuri tu jamani then anampa mmewe?kuna ubaya gani kwani.Hawa nao sijui wakoje ndo nini kutoleana mambo yenu mliyokuwa mkifanya mkiwa mnapendana?Si waangalie yaliyopo?Yaliyopita wayaache huko huko kwenye ndoa yao ya zamani.

Labda ameamua kutumia tafsida kupunguza ukali wa neno tigo pesa
 
Back
Top Bottom