Poulsen ataja kikosi cha kuivaa Msumbiji.......Ni majina yale yale.....Je Tufafika kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Poulsen ataja kikosi cha kuivaa Msumbiji.......Ni majina yale yale.....Je Tufafika kweli?

Discussion in 'Sports' started by Balantanda, Feb 16, 2012.

 1. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Kikosi kamili kinaundwa na makipa Shabani Kado (Yanga), Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ali (Azam).

  Mabeki ni nahodha Shadrack Nsajigwa (Yanga), Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba), Juma Jabu (Simba), Stephen Mwasyika (Yanga) na Kelvin Yondani (Simba).


  Viungo ni Jonas Gerard (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Shomari Kapombe (Simba), Salum Abubakar (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Abdi Kassim (Azam).

  Washambuliaji ni Hussein Javu (Mtibwa Sugar), John Bocco (Azam), Nizar Khalfan (Philadelphia Union, Marekani), Mrisho Ngasa (Azam), Ally Badru Ally (Canal Suez, Misri), Uhuru Selemani (Simba) na Nsa Job (Villa Squad).


  My Take :

  Kwa staili hii tutaendelea kuwa ni kichwa cha Mwendawazimu.........Hawa akina Nsajigwa,Kaseja,Nditi,Nyoso,Mwasyika, Abdi Kassim, Nizar Khalfan, Nsa Job, Boko wa nini?............Tunahitaji kuwa na timu ya wachezaji chipukizi wa aina ya akina Kado,Mwadini,Kapombe,Salum Abukbakar 'Sure Boy', Gerald Jonas,Ally Badru,Hussein Javu, Ramadhani Singano 'Messi wa Msimbazi' na chipukizi wengine....Hapo ndipo tutajenga timu ya maana....Tujaribu japo kuwaiga wenzetu wa Zambia na Zimbabwe(walileta timu ya vijana Challenge kwa ajili ya kijenga timu yao ya Taifa na ikaonesha kandanda safi )......

  Kwa staili hii tutaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu na wasindikizaji......Tutaendelea kuwa washangiliaji wa Timu za mataifa mengine....
   
 2. Iramusm

  Iramusm JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 424
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Lakini zambia walipoleta timu ya vijana hapa haimaanishi hawakuwa na timu ya wakubwa ! Na mashindano ya challenge sio sawa na mashindano ya kugombea kushiriki kombe la dunia, hata zambia hawawezi kupeleka timu waliyoleta hapa kwenda kushiriki qualifications za world cup au AFCON . Point yako ya kuwa tuwekeze kwa vijana ni nzuri, lakini si katika hii style unayosema. I beg to differ.
   
 3. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  kwani tunaweza pata wachezaji zaidi ya hawa ambao hawajui? tuambie wako wapi?
   
 5. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hawa wote akina Kado,Mwadini,Kapombe,Salum Abukbakar 'Sure Boy', Gerald Jonas,Ally Badru,Hussein Javu, unaowataka mbona kawataja kwenye kikosi!? Au ulitaka awataje mara mbilimbili? yaani awataje kwenye nafasi za mabeki awarudie kwenye ushambulia. Husomeki!!!!!
   
 6. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wangechukua wale wa coka cola.
   
 7. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2012
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  hasomeki kabisaaa atuachie Yanga yetu!
   
 8. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hao ndo wazuri kuliko wengine
   
 9. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Vyovyote........

  Umekurupuka ama?.....Zambia hawakuileta timu ya vijana kwenye challenge mwaka jana,walioleta timu ya vijana ni Zimbabwe(soma vizuri post yangu),kocha wa Zimbabwe Norman Mapeza alisema kwamba ameileta timu hii ili ipate uzoefu wa kushiriki mashindano ya Afrika.......Concern yangu ni kwamba tuanze kuwapeleka vijana wakashiriki mashindano haya ili waanze kuapata uzoefu wa mashindano makubwa...Hao wazee wameshafail katika kila mashindano waliyoshiriki sasa ya nini kuendelea kuwakumbatia?....

  Tanzania tunao wachezaji wengi tu na wazuri ambao wako Ngorongoro Heroes,Manyara Stars na Serengeti Boys na Karume Boys.....Pia Copa Coca Cola huwa inao wachezaji wazuri tu...Hizo timu za vijana zina wachezaji ambao ni wazuri zaidi ya hao wazee akina Kaseja,Nsajigwa,Nditi,Nizar na wengine.......Kama uliangalia mechi ya Simba na Azam FC utakubaliana na mimi kwamba bwana madogo Shomary Kapombe wa Simba na Salum Abubakary 'Sure Boy' wa Azam ndio walikuwa nyota wa mchezo kutokana na jinsi walivyolitawala dimba la kati(kiungo).....Pia Ramadhani Singano(wenyewe Simba wanamwita Messi) aliwanyanyasa vilivyo beki ya Azam....
   
 10. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Tanzania tunao wachezaji wengi tu na wazuri ambao wako Ngorongoro Heroes,Manyara Stars na Serengeti Boys na Karume Boys.....Pia Copa Coca Cola huwa inao wachezaji wazuri tu...Hizo timu za vijana zina wachezaji ambao ni wazuri zaidi ya hao wazee akina Kaseja,Nsajigwa,Nditi,Nizar na wengine.......Kama uliangalia mechi ya Simba na Azam FC utakubaliana na mimi kwamba bwana madogo Shomary Kapombe wa Simba na Salum Abubakary 'Sure Boy' wa Azam ndio walikuwa nyota wa mchezo kutokana na jinsi walivyolitawala dimba la kati(kiungo).....Pia Ramadhani Singano(wenyewe Simba wanamwita Messi) aliwanyanyasa vilivyo beki ya Azam....
   
 11. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Si vibaya ukautumia muda wako kutulia na kusoma vizuri na kukielewa nilichokiandika badala ya kukimbilia kujibu na kupotosha maana ya nilichokiandika mkuu.......Nimesema "Tunahitaji kuwa na timu ya wachezaji chipukizi wa aina ya akina Kado,Mwadini,Kapombe,Salum Abukbakar 'Sure Boy', Gerald Jonas,Ally Badru,Hussein Javu, Ramadhani Singano 'Messi wa Msimbazi' na chipukizi wengine....Hapo ndipo tutajenga timu ya maana...."............

  Hao akina Nsajigwa,Kaseja,Nizar Khalfan,Shaban Nditi,Mrisho Ngassa, Nsa Job,Stephano Mwasyika, Chollo, Juma Jabu, Abdi Kassim,John Boko et al hawafai kuchezea Stars......Tunahitaji chipukizi(damu changa) wa kuwaendeleza kwa kuanza kuwapeleka kushiriki kwenye mashindano makubwa(maana kujitoa na kuandaa timu hata kwa miaka mitano imeshindikana)........Timu ya Taifa ya Mali iliyoshiriki AFCON 2002 iliundwa na vijana wadogo kiasi kwamba mchezaji mwenye umri mkubwa alikuwa na miaka 28(http://en.wikipedia.org/wiki/2002_African_Cup_of_Nations_(squads)#Mali)......Timu hii ilishiriki na kushika nafasi ya 4 katika mashindano hayo.........Waliwekeza kwa vijana na waliamua kupeleka timu iliyoonekana ni ya watoto kwenye mashindano husika...

   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwani sisi tunataka kufika au bora liende?
   
 13. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,986
  Likes Received: 3,735
  Trophy Points: 280
  gonjwa sugu hili.....ni kama lile gonjwa la "kuandika katiba mpya" ambalo lilihitaji msukumo wa opposition kuanzisha mchakato unaoendelea. JK's once fading star now appears to start blinking again - thanks to chadema & co!

  the point i want to make is..........anzisha competition (usiniulize vipi) against TFF, utaona akina tenga watakavyokurupuka na football academies na si kuporomosha magorofa mikocheni!
   
 14. Iramusm

  Iramusm JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 424
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Huwezi kuwa na timu ya chipukizi tupu katika mashindano makubwa kama haya, huu mchanyato alioufanya Poulsen ni mzuri. Nakubaliana na kutumia timu za vijana kwenye challenge au makombe madogo tunayoalikwa kama Kombe la Bonde la mto Nile , au COSAFA....lakini sio Qualifications za World Cup

  Halafu uliposema tuwaige Zambia, hebu fafanua ,tuwaige lipi?
   
 15. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 3,999
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  kaka Batalanda tuko pamoja mkuu....timu inatakiwa vijana wengi..tena ni rahisi tu angeongea na mdenish mwenzake ampe vijana wa kazi ambao kule COSAFA under 18 walifanya vzr hata hiyo zambia unayosema waliona cha moto kwa hao madogo
   
 16. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  wabongo kama waingereza kwa hiyo sasahivi paulsen hafai!!mi naona tumchukue shafii dauda.
   
 17. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 3,999
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  .......hahahahaha...mkuu hatujasema kocha hafai..ila uteuzi una utata..bado anakumbatia wazee
   
 18. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Heri Paulsen ndiye aliyechagua wachezaji tisa wa Simba huku Yanga wakiwa watatu, maana Julio alipigiwa sana kelele.
   
 19. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kwani shafii ni kocha au mtoa maoni ya mpira redioni..
   
 20. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  ili kuondoa kidomodomo cha wabongo,ni bora tumpe timu dauda akisaidiana na balantanda.
   
Loading...