Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,640
- 729,672
Lakini pia unaweza kuelezea postmodernism kama dharura ya kijamii na nguvu ya upashanaji habari, mahusiano ya mtu na mtu na mahusiano ya mtu na jamii
Postmodernism ni dhana ya dunia kama kijiji na dhana yenye nguvu sana ya kupata habari za uhakika na wakati mwingine habari za kufikirika kutunga au kuzusha ndani ya muda mfupi sana
Tunaishi kwenye dunia ya kufikirika zaidi kuliko uhalisia, mkazo mkubwa ukiwa kwenye jamii inayobadilika kwa kasi ya ajabu na kuleta kizungumkuti cha sintofahamu huku jamii ikitoboka na kujigawa katika matabaka vikundi na uasili kulingana na matakwa na mahitaji inayojumuisha asili mitazamo mtindo wa maisha imani kabila hata kipato ujuzi na elimu
Jamii ya sasa haiko integrated na mitifuano na mikanganyiko ya kila aina .mtu anakuwa kwenye group la dini la kikabila la chuo la kazini la mtaani. ...huku ni kuchanganya na kuchanganyikiwa lakini kwakuwa huu ndio wakati wake hatuna la kufanya zaidi ya kuangalia
Cha muhimu ni kuchanganyikiwa na kudhani kuwa maisha ya mitandaoni ndio maisha halisi....hii ni postmodernism so take it easy