Posted Date::2/2/2008

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Maalim Seif amsifu Balozi Karume kuhusu hatima ya Zanzibar
Na Mkinga Mkinga

SIKU chache baada ya Balozi wa Tanzania nchini Italia, Ali Karume, kutangaza azma yake ya kutaka kugombea urais wa Zanzibar mwaka 2010, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Sharif Hamad amesema, balozi huyo ana uwezo kuliko kaka yake ambaye ni Rais wa sasa wa Zanzibar.

Katibu huyo wa CUF aliliambia gazeti hili katika mahojiano maalum wiki hii kuwa; "Ali ana unafuu mkubwa walau anaweza kukubalika. Ameanza kutambua matatizo yaliyopo Zanzibar, hii kidogo inanipa faraja kwamba kuna mtu anayeweza kutambua matatizo yaliyopo ndani ya nchi,� alisema Maalim Seif.

Akiwalinganisha Balozi Karume na kaka yake Amani Karume, Seif alisema, Balozi Ali ni bora kwa kuwa anaufahamu ukweli na kuukubali.

"Katika miaka yote Rais Karume amekuwa hakubali kama nchi hiyo sasa inahitaji serikali ya mseto pamoja na kutatua mpasuko wa kisiasa uliopo baina ya vyama viwili vya siasa visiwani hapa," alisema.

Katibu Mkuu huyo wa CUF aliongeza kuwa, katika siku za karibuni ameanza kujawa na faraja baada ya kuona kunakuwepo watu ndani ya CCM ambao wanakuwa na mawazo ambayo yapo katika vyama vya upinzani.

Baadhi ya mawazo hayo ni pamoja na kubaini mgogoro wa kisiasa uliopo Zanzibar na kutafuta suluhu ya matatizo hayo, likiwemo la uchumi kuporomoka.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu huyo alisema kuwa mazungumzo ya muafaka kati ya CUF na CCM yanaendelea vizuri na kwamba chama chake kitayaweka hadharani yakiwa tayari.

�Kimsingi mazungumzo ya muafaka yanaendelea vizuri sana; na endapo yatakamilika tutayaweka hadharani ili wananchi wetu wote watambue nini tumekifanya kwa muda mrefu,� alisema.

Alipotakiwa kufafanua zaidi hicho ambacho sasa kimechukua zaidi ya mwaka mmoja katika mazungumzo yao, Maalim Seif Sharif alisema inakuwa vigumu ila, wananchi wasubiri mpaka dakika ya mwisho kama walivyoweza kusubiri kwa muda wote ambao mazungumzo yamekuwa yakiendelea.

Wakati huo huo; Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati amesema kuwa kitendo cha Balozi Karume kujitangaza mapema kabla ya wakati hakivunji taratibu zozote za chama hicho.

"Sio jinai kwa mtu kusema atagombea urais. Kibaya ni kufanya kampeni. Taratibu za chama zinakataza kampeni na si mtu kujitangaza. Balozi Karume hajafanya ushawishi wowote wa kuomba achaguliwe bali ametangaza nia tu," alisema.

Kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanachama wa CCM ambao wanadai kuwa, kitendo cha Balozi Karume kujitangaza wakati kipindi hakijafika, kinakiuka taratibu.

Baadhi ya makada wa CCM waliozungumza na gazeti hili wiki iliyopita walisema, chama hicho kimekuwa na tabia ya kuumiza wanachama wasio na nafasi na kisha kuwaacha wenye nguvu kuendelea kuvunja taratibu zilizopo.

Makada hao wanaeleza kuwa, wapo wenzao waliowahi kuhisiwa kufanya kampeni katika kipindi cha mwaka wa uchaguzi uliopita na wakafungiwa kugombea, lakini wakawa na hofu kuwa kwa upande wa Balozi Karume jambo hili litafumbiwa macho.

Balozi Karume mwenyewe alipoulizwa, alisimamia kauli yake ya kuwa ametangaza nia kwa lengo la kuwapa kipindi kirefu wananchi kumfahamu na kumchunguza kama anafaa kweli kuongoza nchi hiyo.

"Nimetangaza nia hii mapema na wenzangu wanatakiwa kuiga. Utamaduni wa kujificha na kujitokeza dakika za majeruhi unawafanya wananchi kupata viongozi wabovu," Balozi Karume aliliambia gazeti hili wiki iliyopita.
 
sawa tuyaangalie maana ndio ba mkubwa kasema yale ambayo cuf walikuwa wakiyapigia kelele muda mrefu
 
JK sidhani kama ana uwezo huo wa kusema ya aina hii ama kuwashawishi wana CCM kuelewa. Kuna wana CCM pale Zenji wanaamini Zanzibar ni mali yao na si wapinzani ambao pia walipa kodi na wananchi wa Zanzibar. Kasema Karume nadhani kachoka na unafiki kama he is real ama alitaka umaarufu. Lakini kalikoroga na sasa Waeznji wataanza upya kuamka na mawazo yake . Kazi iko kweli kweli visiwani.
 
Sidhani kama ni kampeni, ametoa mawazo yake juu ya mpasuko, ambayo yamewakuna wengi, hivyo akishukuriwa na kujadiliwa sio kampeni.
 
heee heee ww kibunango mwisho;

sasa tuseme lunyungu alitaka kuspin?

nimepata kali moja waungwa nnamba wenye kuijua watupasulie kuwa huyu na ka ka yake picha haziendi ?
 
heee heee ww kibunango mwisho;

sasa tuseme lunyungu alitaka kuspin?

nimepata kali moja waungwa nnamba wenye kuijua watupasulie kuwa huyu na ka ka yake picha haziendi ?

Mimi siktaka ku spin hata mara moja . Soma mabandiko yangu nyuma baada ta matamshi ya Ali Karume . Nilikuja hapa na kumoa sifa zake za wazi kabisa kwamba sasa pamoja na uozo wote kaanza kuamka .Mimi nimeleta habari zote hizi mbili kwamba ninazikubali . Kazi ya karume ni nzuri na matamshi yake lazima yememuumiza JK na kumganya aonekane Kituko nalabda kauli itakuwa imejadiliwa Dodoma pia .What he said is what supposed to be done . Naipenda Tanzania na Zanzibar is part of it .Huyu jamaa ni mpuuzi lakini kwa mara ya kwanza kasema kitu kimeniingia na ninakubali.Si mara nyingi umkute mwana CCM anakuja na kusema wazi namna hii. Wangalijaribu hata kukemea na kusema kwa wazi mara kibao Nchi ingalikuwa iko mbali .So where is my intent to spin?
 
mkuu tumekupata na kukufahamu vyema

ahsante kwa ufafanuzi

tumuombee dua awe mgombea wetu na mwisho awe rais wetu
 
Katibu huyo wa CUF aliliambia gazeti hili katika mahojiano maalum wiki hii kuwa; "Ali ana unafuu mkubwa walau anaweza kukubalika. Ameanza kutambua matatizo yaliyopo Zanzibar, hii kidogo inanipa faraja kwamba kuna mtu anayeweza kutambua matatizo yaliyopo ndani ya nchi,� alisema Maalim Seif.

Hivi Maalimu Seif amekata tamaa??? maana naona anatamani CCM ipate mgombea mzuri?

What does this mean?
 
maalim seif anataka maendeleo ya zanzibar.
ikiwa cuf au ccm watatoa wagom bea wazuri basi taifa litakuwa na uhakika wa maendeleo
 
Kuna mdau aliuliza tumejifunza nini kwenye mchakato wa USA, nahisi Ali Karume kafuata mfumo wa wagombea(wa US) kujitangaza miaka miwili kabla.

Zanzibar wanahitaji Agent of change mambo ya Dynastic Politics ni dalili za woga na kutojiamini.
 
Zeni wajitaji je CCM wako tayari kuendesha mambo ya wazi kama haya ya huko US ? Maaana hata mwenyekiti wao wa Chama alisimama na kivuli na Makamu mwenyekiti sasa uwazi na issue mezani wataweza ?
 
Back
Top Bottom