Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,906
Maalim Seif amsifu Balozi Karume kuhusu hatima ya Zanzibar
Na Mkinga Mkinga
SIKU chache baada ya Balozi wa Tanzania nchini Italia, Ali Karume, kutangaza azma yake ya kutaka kugombea urais wa Zanzibar mwaka 2010, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Sharif Hamad amesema, balozi huyo ana uwezo kuliko kaka yake ambaye ni Rais wa sasa wa Zanzibar.
Katibu huyo wa CUF aliliambia gazeti hili katika mahojiano maalum wiki hii kuwa; "Ali ana unafuu mkubwa walau anaweza kukubalika. Ameanza kutambua matatizo yaliyopo Zanzibar, hii kidogo inanipa faraja kwamba kuna mtu anayeweza kutambua matatizo yaliyopo ndani ya nchi,� alisema Maalim Seif.
Akiwalinganisha Balozi Karume na kaka yake Amani Karume, Seif alisema, Balozi Ali ni bora kwa kuwa anaufahamu ukweli na kuukubali.
"Katika miaka yote Rais Karume amekuwa hakubali kama nchi hiyo sasa inahitaji serikali ya mseto pamoja na kutatua mpasuko wa kisiasa uliopo baina ya vyama viwili vya siasa visiwani hapa," alisema.
Katibu Mkuu huyo wa CUF aliongeza kuwa, katika siku za karibuni ameanza kujawa na faraja baada ya kuona kunakuwepo watu ndani ya CCM ambao wanakuwa na mawazo ambayo yapo katika vyama vya upinzani.
Baadhi ya mawazo hayo ni pamoja na kubaini mgogoro wa kisiasa uliopo Zanzibar na kutafuta suluhu ya matatizo hayo, likiwemo la uchumi kuporomoka.
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu huyo alisema kuwa mazungumzo ya muafaka kati ya CUF na CCM yanaendelea vizuri na kwamba chama chake kitayaweka hadharani yakiwa tayari.
�Kimsingi mazungumzo ya muafaka yanaendelea vizuri sana; na endapo yatakamilika tutayaweka hadharani ili wananchi wetu wote watambue nini tumekifanya kwa muda mrefu,� alisema.
Alipotakiwa kufafanua zaidi hicho ambacho sasa kimechukua zaidi ya mwaka mmoja katika mazungumzo yao, Maalim Seif Sharif alisema inakuwa vigumu ila, wananchi wasubiri mpaka dakika ya mwisho kama walivyoweza kusubiri kwa muda wote ambao mazungumzo yamekuwa yakiendelea.
Wakati huo huo; Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati amesema kuwa kitendo cha Balozi Karume kujitangaza mapema kabla ya wakati hakivunji taratibu zozote za chama hicho.
"Sio jinai kwa mtu kusema atagombea urais. Kibaya ni kufanya kampeni. Taratibu za chama zinakataza kampeni na si mtu kujitangaza. Balozi Karume hajafanya ushawishi wowote wa kuomba achaguliwe bali ametangaza nia tu," alisema.
Kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanachama wa CCM ambao wanadai kuwa, kitendo cha Balozi Karume kujitangaza wakati kipindi hakijafika, kinakiuka taratibu.
Baadhi ya makada wa CCM waliozungumza na gazeti hili wiki iliyopita walisema, chama hicho kimekuwa na tabia ya kuumiza wanachama wasio na nafasi na kisha kuwaacha wenye nguvu kuendelea kuvunja taratibu zilizopo.
Makada hao wanaeleza kuwa, wapo wenzao waliowahi kuhisiwa kufanya kampeni katika kipindi cha mwaka wa uchaguzi uliopita na wakafungiwa kugombea, lakini wakawa na hofu kuwa kwa upande wa Balozi Karume jambo hili litafumbiwa macho.
Balozi Karume mwenyewe alipoulizwa, alisimamia kauli yake ya kuwa ametangaza nia kwa lengo la kuwapa kipindi kirefu wananchi kumfahamu na kumchunguza kama anafaa kweli kuongoza nchi hiyo.
"Nimetangaza nia hii mapema na wenzangu wanatakiwa kuiga. Utamaduni wa kujificha na kujitokeza dakika za majeruhi unawafanya wananchi kupata viongozi wabovu," Balozi Karume aliliambia gazeti hili wiki iliyopita.