Posta yatimua wakurugenzi.. kisa JF!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,929
Habari ambazo zinaingia mida hii kutoka Dar zinasema kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta baada ya kukutana leo imeamua kuwatimua wakurugenzi wake watatu kwa kile kinachoaminika ni kuvujisha siri za shirika hilo hususan zihusiano na vitendo vya kifisadi.

Habari za ufisadi kwenye shirika hilo zilitemwa kwenye mtandao huu wa JF siku chache zilizopita. Hata hivyo kwa wale "wanaojua" habari hizi hazikutoka kwa afisa yeyote wa juu ndani ya shirika hilo isipokuwa baadhi ya Watanzania ambao wamechoshwa na hujuma na vitendo vya kifisadi.

Kama ufukuzwaji huo utathibitishwa hii itakuwa ni mara nyingine ambapo JF imetumiwa kisingizio cha kufukuza watu ili kutishia watumishi wa umma wasifichue uovu kwenye taasisi za umma na ambazo ni nyeti. Miezi michache iliyopita shirika la ndege la ATC nalo lilitimua watumishi wake watano kwa kisingio cha kuvujisha siri za ununuzi wa dege la Airbus na vitendo vya kifisadi ndani ya shirika hilo.

Wakati huo huo mojawapo ya Vyuo Vikuu vya Tanzania nacho kimemfuta kazi mmoja wa wahadhiri wake waandamizi kwa kile amacho viongozi wa chuo hicho wanadai kuwa ni "pressure" toka juu hasa baaada ya mhadhiri huyo mwishoni mwaka jana kujitokeza hadharani na kumnyoshea kidole cha ufisadi mmojawapo wa mawaziri na kumtaka ajiuzulu.

Kama tabia hii ya "kufukuza fukuza" itaendelea bila kukomeshwa mara moja, Taifa la Tanzania litakuwa limeanzisha utawala wa vitisho na utamaduni wa kuziba habari za vitendo vya kifisadi kwa kutishia retaliation kwa mtu yeyote yule.

Hadi hivi sasa haijajulikana ni kwa kiasi gani sheria ya "Whistleblowing" imefikia na ni lini sheria hiyo itaanza kuwalinda Watanzania ambao wanaibua vitendo vya kifisadi, kuhujumu uchumi, rushwa, na ukiukwaji wa maadili katika sehemu zao za kazi.
 
Whistleblowing is the only solution in a system were there is complete disregard of accountability procedures...As long as kuna mkweli ndani yake..wacha wananchi tuendeshe nchi yetu!!!
 
Ikulu baada ya kuona mambo mazito walimwekja Kulumanga akashidwa wakamweka Salva .Posta hawajapata akili ya Ikulu ?Miaka hii watu wamechoka na watazidi kuwafukuza mwishowe wajiletee balaa .JF hongera
 
Habari ambazo zinaingia mida hii kutoka Dar zinasema kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta baada ya kukutana leo imeamua kuwatimua wakurugenzi wake watatu kwa kile kinachoaminika ni kuvujisha siri za shirika hilo hususan zihusiano na vitendo vya kifisadi.

Habari za ufisadi kwenye shirika hilo zilitemwa kwenye mtandao huu wa JF siku chache zilizopita. Hata hivyo kwa wale "wanaojua" habari hizi hazikutoka kwa afisa yeyote wa juu ndani ya shirika hilo isipokuwa baadhi ya Watanzania ambao wamechoshwa na hujuma na vitendo vya kifisadi.

Kama ufukuzwaji huo utathibitishwa hii itakuwa ni mara nyingine ambapo JF imetumiwa kisingizio cha kufukuza watu ili kutishia watumishi wa umma wasifichue uovu kwenye taasisi za umma na ambazo ni nyeti. Miezi michache iliyopita shirika la ndege la ATC nalo lilitimua watumishi wake watano kwa kisingio cha kuvujisha siri za ununuzi wa dege la Airbus na vitendo vya kifisadi ndani ya shirika hilo.

ASANTE KWA HIZI HABARI LAKINI KUNA WALAKINI KIDOGO HAPA:

-majina na vyeo vya hawa waheshimiwa waliotimuliwa mbona hujatupatia?

Wakati huo huo mojawapo ya Vyuo Vikuu vya Tanzania nacho kimemfuta kazi mmoja wa wahadhiri wake waandamizi kwa kile amacho viongozi wa chuo hicho wanadai kuwa ni "pressure" toka juu hasa baaada ya mhadhiri huyo mwishoni mwaka jana kujitokeza hadharani na kumnyoshea kidole cha ufisadi mmojawapo wa mawaziri na kumtaka ajiuzulu.

Hii nayo haijakaa sawa

-CHUO KIPI?

-WAHADHIRI WEPI WALIOTIMULIWA

-PRESSURE TOKA JUU KWA NANI (dont tell me ni Msolla kwani huyu hayupo tena kule)

-MHADHIRI GANI ALIYETIMULIWA?

Kama tabia hii ya "kufukuza fukuza" itaendelea bila kukomeshwa mara moja, Taifa la Tanzania litakuwa limeanzisha utawala wa vitisho na utamaduni wa kuziba habari za vitendo vya kifisadi kwa kutishia retaliation kwa mtu yeyote yule.

Hadi hivi sasa haijajulikana ni kwa kiasi gani sheria ya "Whistleblowing" imefikia na ni lini sheria hiyo itaanza kuwalinda Watanzania ambao wanaibua vitendo vya kifisadi, kuhujumu uchumi, rushwa, na ukiukwaji wa maadili katika sehemu zao za kazi.

NAKUBALIANA NAWE 100% Lakini ni vizuri tukawapa hawa watu namna ya kufanya leaks bila kustukiwa na pili tutakuwa tunawasaidia zaidi kwa kuweka majina bayana vile vile otherwise tutakuwa tunajaza maji kwenye gunia au nunasemaje mzee

if worse becomes worse ipo WIKILEAKS
 
mzee nilipoweka habari ya kukamatwa wanachama wa JF sikuweka majina kulikuwa na sababu... so, ipe muda kidogo. Wakati mwingine tunaziweka hizi habari kusababisha mambo fulani...

Wale wa ATC majina yao tayari yapo hapa somewhere...
 
ASANTE KWA HIZI HABARI LAKINI KUNA WALAKINI KIDOGO HAPA:

-majina na vyeo vya hawa waheshimiwa waliotimuliwa mbona hujatupatia?

Hii nayo haijakaa sawa

-CHUO KIPI?

-WAHADHIRI WEPI WALIOTIMULIWA [/B]

-PRESSURE TOKA JUU KWA NANI (dont tell me ni Msolla kwani huyu hayupo tena kule)

-MHADHIRI GANI ALIYETIMULIWA?

NAKUBALIANA NAWE 100% Lakini ni vizuri tukawapa hawa watu namna ya kufanya leaks bila kustukiwa na pili tutakuwa tunawasaidia zaidi kwa kuweka majina bayana vile vile otherwise tutakuwa tunajaza maji kwenye gunia au nunasemaje mzee

if worse becomes worse ipo WIKILEAKS

Absolutely Pumba of the highest degree.
Wilmot said:
When an intelligent man refuses to use his brains, he's the biggest fool of all.
 
Toba!:eek: Sasa barua zangu itakuwaje...tehe si ndio basi. Eti waliotimuliwa wametumia P.O Box ya JamboForums? au?
 
lazima muelewe kwamba sio kila kitu kinatakiwa kuwa public, kuna mambo mengine kama ya kikazi ni ya kikazi na inaweza ikatoa taarifa kwa jamii baada ya process kukamilika, pengine hawa watu walifanya ndivyo sivyo ndio maana wakatimuliwa, sio kila kitu ni public jamani eehhhhhhh !
 
Kweli kabisa SteveD,

Nakumbuka kuna memba mmoja alisema hiki kuwa Posta wameanza kufuatilia watu wanaodhaniwa kuwa wamevujisha habari kwa JF

Soma hizi posts zake:

9th April 2008, 06:35 AM
ulusungu
Junior Member Join Date: Sun Apr 2008
Posts: 5
Rep Power: 0

Thanks: 2
Thanked 2 Times in 2 Posts
Credits: 263

Re: Ubadhirifu mkubwa Benki ya Posta

--------------------------------------------------------------------------------

Tuhuma nzito Benki ya Posta....UPUPU UMEMWAGWA KUNA MTAFUTANO BODI YAENDELEA NA KIKAO SI CHA KUTAFUTA UKWELI WA TUHUMA BALI NI CHA KUMTAFUTA ALIYETOA TUHUMA LA...WANATARAJIA KUIPIGA CHINI MENEJIMENT YOTE,WANAAMINI NI MENEJIMENT TU INAYOJUA UFISADI HUO NA KUUTUO.... HAKIKA WANAWAONEA KABISAA....

Na hii hapa toka kwa ulusungu ...

9th April 2008, 06:38 AM
ulusungu
Junior Member Join Date: Sun Apr 2008
Posts: 5
Rep Power: 0

Thanks: 2
Thanked 2 Times in 2 Posts
Credits: 263

Re: Ubadhirifu mkubwa Benki ya Posta

--------------------------------------------------------------------------------

Sms Za Vitisho Kwa Wakurugenzi Wanodhaniwa Kutoa Habari....wana Jf Tukemee.tuhuma Zinakanushwa Kwa Kuutoa Ukweli Na Si Kumtafuta Mtoaji.....

Ulusungu uko wapi? tafuta mtu mwingine na utafute namna ya kutuma hizo namba za simu zilizotumika kwenye sms au message zenyewe kwa mtu yeyote unayemwamini hapa (hata invisible) ili tuwafuatilie hawa watu.

Hawawezi kufanya ujinga kama huu .... Grrrrrr
 
wenye kutaka majina moja ndio hilo ulusungu.

pole mkuu ndio kazi karibu tena japo kwa jina jengine
 
nafikiri kama kulikuwa na tuhuma basi kulikuwa na sehemu nzuri zaidi ya kupeleka hizo tuhuma kabla hazijaenda public, ona sasa kibarua kimeota nyasi !
 
wenye kutaka majina moja ndio hilo ulusungu.

pole mkuu ndio kazi karibu tena japo kwa jina jengine

No Ulusungu alifikisha ujumbe na sidhani kama ni lazima iwe yeye ni mmoja wa waliofukuzwa kazi. Kuna mengi sana yametokea hapa toka hii habari ivuje JF. Polisi wamepewa report, PCCB hadi kwa level ya juu ya uongozi walifikishiwa taarifa. Hii ni baada ya malalamiko ya muda mrefu ya wafanyakazi wa Posta kwa level zote za uongozi.

Sidhani kama ni wazo kufurahia hawa ndugu kufukuzwa kazi, Hii attachment imemfikia hata Kikwete mwenyewe for a while now. Ni kazi kubwa sana kutokomeza ufisadi huko Tanzania. Watu wana zile hisia za zamani za kuwataka wafanyakazi waaminifu kuwa kama wao au wapoteze kazi.

Very sad indeed!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom