Posta yashiriki kumbukumbu ya mashujaa wa vita ya kwanza ya dunia

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
877
955
Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa Shirika la Posta Tanzania Ndg. Constantine Kasese amehudhuria tukio la kuweka mashada katika makaburi ya Mashujaa waliopigana vita ya kwanza ya dunia kati ya mwaka 1914-1918 kama ishara ya kuwaenzi mashujaa hao,ijulikanayo kama #Layingwreathceremony# katika ofisi za Shirika la Posta zilizopo Posta ya zamani, jijini Dar es Salaam

Kasese amemwakilisha Postamasta Mkuu wa Shirika katika Kumbukumbu hii ambayo huadhimishwa duniani kote kila siku jumapili ya mwanzo ya mwezi Novemba, ambapo mataifa mbalimbali hutumia hufanya ibada maalum, kuwaombea mashujaa hao pamoja kuweka mashada maalum katika makaburi yao

Kwa upande wa Tanzania tukio hili limeratibiwa na Jumuiya ya wanajeshi wastaafu waliopigana vita ya kwanza na ya pili ya dunia (The Tanzania Legion Club) na hufanyika katika mkoa wa Dar es Salaam katika maeneo ya makumbusho, Posta ya Zamani na katika maeneo mengine yenye makaburi hayo

Shirika la Posta Tanzania kama Taasisi ya mawasiliano iliyokuwepo tangu kipindi cha vita hizo imetunza kumbukumbu ya mashujaa hao kwa kuweka makaburi ya mashujaa hao katika ofisi zake za Sokoine zilizopo Posta ya zamani, jijini Dar es Salaam

Sambamba na hilo, Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara Ndg. Kasese alipata wasaa wa kuwakabidhi zawadi ya Stempu wageni waliofika katika ofisi za Shirika la Posta (Posta ya zamani) kama sehemu ya kumbukumbu kwao

Tukio hili limehudhuriwa na Meneja mkoa wa Dar es salaam wa Shirika la Posta Tanzania, maafisa waandamizi wa Shirika hilo, wawakilishi kutoka ubalozi wa Uturuki, Mwambata wa Jeshi kutoka ubalozi huo, wawakilishi kutoka Jumuiya ya wanajeshi wastaafu (The Tanzania Legion Club) Mstaafu kutoka jeshi la Scotland pamoja na wawakilishi kutoka Jumuiya ya watanzania waliosoma nchini Uingereza.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.
14 Novemba,2021
 
Back
Top Bottom