Posta Tanzania naombeni mnieleweshe, sielewi ni uzembe au ndio kawaida

Nieleze

New Member
Aug 8, 2021
1
0
Wadau

Nimekuja humu ndani ili nipate uelewa kutoka Posta Tanzania, na wana jamiiforums. Nimejaribu kuwasiliana na Posta Tanzania kwa njia rasmi zaidi ya wiki moja sasa, hawanijibu, huwenda huku wakajibu.

Nina nyaraka nimetuma zaidi ya mwezi sasa kwa EMS, hadi leo ukiingia kwenye mfumo, nyaraka inaonekana imesajiliwa kwenye Posta niliyotuma, baada ya hapo hakuna maelezo zaidi ya mfumo kusema "Please Wait".


Umbali kutoka Makuu ya Mkoa nilipotuma hadi Makao Makuu ya Mkoa inapoenda ni chini ya km 300.

Screenshot inaonyesha.

20210808_141018.jpg
 
Hao jamaa ovyo sana, wameshanipotezea docs zangu za muhimu mara mbili, hiyo mara ya pili nilikasirika nikawadai fidia niliwaambia docs zimecost laki2 wakanilipa.
 
Yaan kuliko kutumia posta bora mabasi mzigo unafika salama na kwa haraka😀😀😀
 
Pole sana. Tatizo kama ili limewahi kunikuta ila ni shida tu ya utoaji taarifa. Hiko hivi tangu mwaka jana mfumo wa kawaida wa EMS umekuwa hautoi taarifa ya uhalisia mzigo ulipo.(haya maelezo nilipewa hapo posta).

Hivyo nakushauri fika pale ofisini kwao ghorofa ya pili watatumia mifumo yao kukusaidia ku track mzigo.

Au try this link

 
Back
Top Bottom