Posta Tanzania hongereni kwa huduma nzuri na nafuu

Grena

JF-Expert Member
Jul 30, 2016
657
1,541
Habari zenu wakuu,

Nlikuwa na mzigo natakiwa nitume nnje, option yangu ya kwanza ilikuwa nitume na DHL lakini kunasiku kwenye mishe zangu nikapita mahali nikaona office za Posta nikashawishika kuingia na kufanya udadisi wa huduma zao.

Yule dada wa posta akanambia wanahuduma ya EMS inafanya Kazi Kama DHL mzigo utatrackiwa na utafikishwa moja kwa moja Hadi mlangoni kwa mteja.

Akanitajia gharama per grams, Yani wako very cheap. DHL walinambia laki na arobaini wao Ni elfu sabini. Nikasema ngoja nijaribu huduma zao nione zipoje.

Nimefurahishwa Sana within 2 weeks mzigo ushafika kwa Bei cheeeee.

Hongereni Posta, Endeeleni kutoa huduma nzuri.

Screenshot_20210519-144310~2.jpg
 
Sheikhe mie mizigo hua ata kama natak kusafirisha bangi ,ninaye muamini zaidi ni Posta kiufupi changamoto zipo ila posta kwangu ndio king kwa nchi ,nimekua nikinunua bidhaa za pesa mingi sama ughaibun ila posta wananiletea pasi na shida kabisa.
Ni Mara ya kwanza kuwatumia, Nlikuwa na hofu nao Kama utafika salama na kwa wakati.

Ila nimefurahi Sana na huduma zao kila ukitrack inakuonesha Hatua mzigo ulipofikia.
 
Ipi? Tujuze
Siku Ikitokea posta wakaja n idea ya kuuza vifungashio ambavyo wamevitengeneza wenyewe kupitia viwanda vyetu hapa bongo wangepiga pesa sana .Mkuu hua unaona vile percel za ulaya tukizipokea zinavyokua well packed, hadi na kaunyunyu kidogo sijui zinapuliziwa?

Uboxing proccess hua tamu kama unakata utepe kwa manzi wa kimakonde.Ukiwa na simu uko tanga unataka kumtumia babu yako kwetu kule usukumani Shinyanga, ukiipeleka simu posta unambiwa wewe ndio uipack kwa vifungashio uvijuavyo wewe na vinakopatikana ,ilhali ilikua ni suala la kulipia percel ile packing fee inakua included kabisa mzigo ufungwe safi kabisa.

Madhara ya kupack mwenyewe ndio kama ile skendo ya mwamba alikua deily anapitisha mirungi ya biashara kwenda mkoa mwingine tena posta kabisa bila wao kujua, Mara waambiwe maboksi ya blueband. Mara hao ni dagaa wa kigoma wanaenda Arusha kumbe.
 
Hee. Posta Tanzania wangejitangaza na kujulisha watu huduma zao. Wako very cheap DHL ingefilisika.
DHL kufilisika utangoja sana, wana ndege zao za cargo ni noma unajua wana ndege ngapi all over the world , na ndiyo maana ni agent wanaotoa huduma kwa bei ya juu kidogo, niliwatumia kuniletea simu yangu toka UK duh shiping ime cost almost laki2 kasoro, nachowapendea ni express shipping

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom