Posta kama Ulayaaa kudadeki!

RayB

JF-Expert Member
Nov 27, 2009
2,751
196

Posta kama Ulayaaa kudadeki!
Serikali imeanzisha mfumo mpya wa anuani na alama za siri za posta ambapo sasa watu watakuwa wanapokea barua na vifurushi majumbani mwao badala ya kwenda kwenye ofisi za Posta.

Tayari mfumo huo ambao unatumika katika nchi zilizoendelea, umeshaanza kuwekwa mkoani Arusha huku ukifuatiwa na Mkoa wa Dodoma ambapo lengo ni kuanzishwa huduma hiyo nchi nzima.

Akielezea juu ya mfumo huo,Naibu Mkurugenzi wa Huduma za Posta katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), Haruni Lemanya alizitaja kata zenye huduma hiyo mkoani Arusha kwamba ni Kati, Levolosi, Ororian, Kaloleni na Themi na kwamba wanaendelea katika Kata za Unga Limited na Sekei tunaendelea.

Alisema gharama za awali za mradi huo ni Sh bilioni 18 ambazo ni kwa ajili ya kuweka mfumo wa uendeshaji, kuanzisha kitengo cha ukusanyaji takwimu na mfumo wa kompyuta. Wanaochangia gharama ni halmashauri husika na wadau mbalimbali ambao ni watoa huduma.

Chini ya mpango huo kila ghetto litakuwa na anuani mpya pamoja na visanduku nje ya nyumba na kwamba mbali na kufikishiwa huduma za barua pia itasaidia katika utambuzi wa makazi ya mtu.

Mfumo huo mpya ulianza Juni mwaka jana baada ya kukamilika utafiti uliofanywa na Mtaalamu kutoka Umoja wa Posta Duniani kati ya Mei 17 na Juni 8 mwaka jana


My stand:
Labda niswalike swali kwa miundo mbinu hii inawezekana kweli? Na je ni kweli huduma hii ipo kwa hiyo mikoa tajwa? Tujuzane wenyeji au waliokweisha tembelea huko. Hili jambo lilishawahi kufanyika?

from darhotwire.com
NB:( NI habari ya 2009)
 
Haya mambo yalikuwepo toka enzi za utoto wangu, time table ya public transport pia zilikuwepo vituoni kama ulaya, enzi hizo public transport tuliita hekarus (mliokula chumvi kama mimi mtakumbuka haya).

Nakumbuka tulikuwa na school buses. Nilihudhuria ufunguzi wa yale mabasi, tena mabasi mapya yalituchukua toka mashuleni mpaka Karimjee. Tukacheza sana disco uwanjani tukiwa na uniform zetu, soda pia tulikunywa sana siku hiyo.
Masikini kumbe ile ndo ilikuwa mwisho wa kuyaona yale mabasi. Yote yalipotea, na huenda ndiyo zile DCM za mwazo kuwa private buses. Mungu utusaidie.

Hivyo kurudia tena sanduku za posta majumbuni ni jambo jema, lakini siyo ngeni sana, swala je maeneo ya ugavi wa barua yanafikika??? Utaipata barua yako kweli??

Kwa kweli Tanzania tumechanganyikiwa hatujui pa kushika sasa, tunatapatap kama mfa maji, nchi giza, baranara ndo hivyo tena, uchafu ni nyumbani kwetu. Mi nadhani tungesafisha kwanza nchi ndipo ufuate ugavi barua majumbani, maana mgawaji atapita uchochoroni na kwenye madimbwi chungu nzima??.

Kila la heri ktk juhudi za kulibomoa Taifa.
 
kama nakaa manzese watanipataje?

Watakuja na pikipiki mzee! Mimi wasiwasi wangu kuzitambua izo nyuma amabzo haziko kimpamgilio wala kinamba itakuwaje? Ni ishu kubwa ujue? Mtu anaweza kutembea kutwa nzima anatafuta nyumba na asiione? Si unajua mtu ukielekezwa maeneo fulani kabla ya hivi vilonga longa? Kutokezea ****** ilkuwa ni moja ya direction!!?
 
Mmh hiyo ni habari njema.Mambo yakwenda kwenda Posta yanaboa sana.
 
Mambo yote haya yanaendana na kukua kwa miji na population katk sehemu husika na pia kama kweli wanataka basi kunatakiwa kuwe na mipangilio ya miji na makazi husika
 
Tatizo lingine ni ule uaminifu kwa wafanyakazi wa posta. Manake anaweza akakaa chini na mizigo yake na kuchambua mizigo ya maana sidhani kama huwa wanaandikishwa kuwa amechukua barua kadhaa na za sehemu fulani. Sidhani kama huwa wanakuwa answerable kkwa upotevu wa mali. Nasema hivyo kwa kuwa imeshanitokea sana nimetuma vitu vya thamani na vingi havikufika.
 
Huduma bora kwa jamii ! Mipango miji imekaa kama jalala la takataka sijui hizo anuani zitakuaje
 
Wasiwasi wangu ni kuwa kwa jinsi vibaka walivyotapakaa mitaani watakuwa wanaiba hata barua za watu kwenye visanduku vya nyumbani kwao hasa vile vilivyo nje ya nyumba zao. Labda kama kutakuwa na utaratibu wa kuwa na funguo na kuingia ndani ya geti. Hapa napo linakuja suala la uaminifu wa hao wasambaji wa hizo barua maana wanaweza kuwa chanzo cha kuja kwa majambazi nyumbani kwako kama wameona kuna kitu cha kuiba hapo. Taabu tupu kwenye nchi zetu maskini.
 
tena kwa bi manayuu!

Watu nimeona Avatar yako nimekumbuka kuwa kuna kipindi nilimtunia mtu jezi ya mpya ya Fabregas enzi zile hizi wanazovaaa sasa ndo zimetoka ebwanaa ee kwani ilifika hakuna kabisa walikwiba sasa hii ya kuwapa vifurushi wapeleke nyumbani si ndo zitaibiwa zote
 
Back
Top Bottom