RayB
JF-Expert Member
- Nov 27, 2009
- 2,751
- 196
Posta kama Ulayaaa kudadeki!
Serikali imeanzisha mfumo mpya wa anuani na alama za siri za posta ambapo sasa watu watakuwa wanapokea barua na vifurushi majumbani mwao badala ya kwenda kwenye ofisi za Posta.
Tayari mfumo huo ambao unatumika katika nchi zilizoendelea, umeshaanza kuwekwa mkoani Arusha huku ukifuatiwa na Mkoa wa Dodoma ambapo lengo ni kuanzishwa huduma hiyo nchi nzima.
Akielezea juu ya mfumo huo,Naibu Mkurugenzi wa Huduma za Posta katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), Haruni Lemanya alizitaja kata zenye huduma hiyo mkoani Arusha kwamba ni Kati, Levolosi, Ororian, Kaloleni na Themi na kwamba wanaendelea katika Kata za Unga Limited na Sekei tunaendelea.
Alisema gharama za awali za mradi huo ni Sh bilioni 18 ambazo ni kwa ajili ya kuweka mfumo wa uendeshaji, kuanzisha kitengo cha ukusanyaji takwimu na mfumo wa kompyuta. Wanaochangia gharama ni halmashauri husika na wadau mbalimbali ambao ni watoa huduma.
Chini ya mpango huo kila ghetto litakuwa na anuani mpya pamoja na visanduku nje ya nyumba na kwamba mbali na kufikishiwa huduma za barua pia itasaidia katika utambuzi wa makazi ya mtu.
Mfumo huo mpya ulianza Juni mwaka jana baada ya kukamilika utafiti uliofanywa na Mtaalamu kutoka Umoja wa Posta Duniani kati ya Mei 17 na Juni 8 mwaka jana
My stand:
Labda niswalike swali kwa miundo mbinu hii inawezekana kweli? Na je ni kweli huduma hii ipo kwa hiyo mikoa tajwa? Tujuzane wenyeji au waliokweisha tembelea huko. Hili jambo lilishawahi kufanyika?
from darhotwire.com NB NI habari ya 2009)