Posta, Dar: Waendesha bodaboda na bajaji watawanywa kwa mabomu ya machozi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,289
2,000
Jeshi la Polisi limetumia mabomu ya Machozi kuwatawanya Waendesha bodaboda na bajaji wanaofanya shughli zao Posta mpya karibu na jengo la Benjamin Mkapa Tower baada ga uongozi kuwataka kuondoka katika maeneo hayo kwa madao kuwa hawaruhusiwi hiki waendesha bodaboda na bajaji wakipinga hatua hiyo

 

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,510
2,000
Madai yao ya Msingi ni Yepi? Siku hizi naona wanatamalaki mjini na Bajaji na Bodaboda.
 

kayaman

JF-Expert Member
Aug 3, 2013
4,195
2,000
Pale mbele ya benjamini wanapopaki sasa bajaj zimekua nyingi sana na wengine wanapaki bila utaratibu kitu kinachofanya barabara iwe finyu ni vyema jiji liwatafutie sehem nzuri kwasababu bajaj na bodaboda wanasaidia sana!
 

Lovebird

JF-Expert Member
Sep 27, 2012
3,271
2,000
..Hope hawatumii zile risasi zipigwazo angani halafu zinakata konaaaa...

...wakimaliza nao sijui wataenda kwa kundi lipi....
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,889
2,000
Kama Taifa bado hatujapata msimamo wa kudumu kuhusiana na machinga, boda boda, mama ntilie, bajaji na wapiga debe, kila mwaka una matukio yake kuhusiana na hawa watu.

Ni muda sasa tukawa na sera ya kudumu kuhusiana na hawa watu, na kila upande ufuate taratibu. La sivyo itakua ni mtaji wa kudumu kwa wanasiasa.
 

impongo

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
8,114
2,000
Kama Taifa bado hatujapata msimamo wa kudumu kuhusiana na machinga, boda boda, mama ntilie, bajaji na wapiga debe, kila mwaka una matukio yake kuhusiana na hawa watu.

Ni muda sasa tukawa na sera ya kudumu kuhusiana na hawa watu, na kila upande ufuate taratibu. La sivyo itakua ni mtaji wa kudumu kwa wanasiasa.
Kumbe una akili
 

Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,889
2,000
Naona umeanza kupona
Naamini katika serikali ya awamu ya tano, kuwa ipo katika kutatua kero za wanyonge na hilo likiwamo.

Naamini kwamba suluhisho la kudumu litapatikana.

Wananchi nao wajifunze kufuata taratibu pale zinapowekwa.

Hatuwezi kuwa na nchi kama soko kwamba kila mtu anafanya anavyotaka.

Tukiendelea kuwa watu wa aina ambayo tunachukia kufuata taratibu, tutaendelea kusikia maendeleo kwa wenzetu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom