Post yangu ya 1,000 inaenda kwa WANAWAKE WOTE

Bigirita

Platinum Member
Feb 12, 2007
15,986
7,366
Siku ya Wanawake Duniani ni jumatatu 8/3/2010. Napenda kutoa wito kwa Jamii inapaswa kuondokana na na vitendo vya dhuluma na nyanyaso kwa wanawake na wasichana, vinavyodhoofisha afya zao na kuongeza umaskini, badala ya kuwawezesha na kuboresha maisha ya wanawake.

Idadi ya wanaume wanaokemea vitendo vya unyanyasi wa kijinsia inazidi kuongezeka kwa kubadili tabia, mila na desturi ambazo zimepitwa na wakati zinapaswa kukoma.

Serikali na vyombo vyake haina budi kusimama kidete kupinga dhuluma na nyanyaso dhidi ya wanawake, kwa kuweka sera nzuri za kiuchumi na kijamii kwa ajili ya maendeleo ya wanawake. Vyombo vya upashanaji habari havina budi kulinda na kuheshimu utu wa wanawake na kamwe wasiwageuze kuwa ni vichokoo vya matangazo yao ya biashara. Sheria ziwe wazi kwamba, nyanyaso la kijinsi kwa wanawake na wasichana ni kosa la jinai, wahusika wawajibishwe, ile sheria ya mahusiano ya kingono (Sexual Conduct Act of 1994) isiwe ni urembo -just another document.

Nakumbuka Hayati Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa pili alisema hivi kuhusu utu wa mwanamke, "Mulieris Dignitatem" alisema kwamba, bado mfumo dume unaendelea kutawala na hivyo kuwafanya baadhi ya watu kushindwa kutambua kwamba watu wote, wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.


NAWAPENDA NA KUWAHESHIMU WANAWAKE WOTE. na hii ndiyodeclaration yangu kuanzia leo.
 
Brigitta
Umeweka kwenye jukwaa la Nafasi za Kazi na Tenda (Job Vacancies + Tenders)! Hongera kufikisha posts 1000
 
Jamani kweli tuendeleze kupiga vita unyanyasaji wa wanawake, pamoja kwamba idadi kubwa ya wanaume imeongezeka lakini unyanyasaji bado upo sana.
 
Twendelee kuwajali wanawake wote duniani maana bila wao sisi leo wanaume tusingekuwepo duniani fikiria mama ako angeamua kukuflashi wewe leo hii ungekuwepo duniani? Hongereni akina mama kwa kazi nzito mnazifanya ikiwemo kulea familia.
 
Congratulations on ur 1k post... and I am with you on fighting for women's rights ...
 
Mfumo dume ni NATURAL na hauwezi kutokomezwa! Mungu alimwambia Eva kwamba "tamaa yako itakuwa kwa mwanamume naye atakutawala!" Angalieni hata wanyama (simba, ng'ombe, nk) wanaishi kwa mfumo dume! Huo mfumo dume wa wanyama nao unatakiwa utokomezwe? Acheni kuota mchana kweupe! Mimi napinga unyanyasaji, lakini sio mfumo dume!
 
Sheria ziwe wazi kwamba, nyanyaso la kijinsi kwa wanawake na wasichana ni kosa la jinai, wahusika wawajibishwe, ile sheria ya mahusiano ya kingono (Sexual Conduct Act of 1994) isiwe ni urembo -just another document.



NAWAPENDA NA KUWAHESHIMU WANAWAKE WOTE. na hii ndiyodeclaration yangu kuanzia leo.

Hongera sana Mkuu na asante kwa dedication.
Nimeguswa na hapo kwenye red - hii ni ya nchi gani Mkuu, my recollection kama unaongelea Tanzania tunayo sheria moja tu kwenye eneo ulilotaja - Sexual Offences Special Provisions Act of 1998 al maarufu kama SOSPA.... hebu tupe somo kuhusu hii ya 1994 kama hutajali maana kuelemishana ndio moja ya sababu za kutembelea na kushiriki JF
 
Hongera dada kwa posts 1000. lakini kumbuka Mwanzo 2:18 Mungu anasema si vyema mwanamume aendelee kuwa peke yake,nitamfanyia msaidizi
kwa hiyo mwanamke ni msaidizi wa mwanamume mfumo dume upo pale pale.

Mwanzo 2:22 Mungu alichukua ubavu kutoka kwa mwanamume kuwa mwnamke
Mwanzo 2:23 "huyu ni mfupa wa mifupa yangu na nyama ya nyama yangu,huyu ataitwa mwananke kwa sababu huyu alitolewa kwa mwanamume .
Kwa hiyo ukiangalia tangu enzi na enzi mwanamke ni msaidizi wa mwanamume.Hii haitabailika milele.
 
Back
Top Bottom