Post moterm: Nyakarungu na Dr Makatta uso kwa uso tena Babati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Post moterm: Nyakarungu na Dr Makatta uso kwa uso tena Babati

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyakarungu, Jun 18, 2011.

 1. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Polisi wetu wameamua kusimamia uhusiano mbaya kati yao na raia, na kwa kuthibitisha hilo wameendelea kuwapiga raia na kuwaumiza hata kuwaua.

  Haya yametokea kona nyingi za nchi yetu, na week hii niliitwa babati kusimamia uchunguzi wa mtu aliyekufa akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kumkamata kwa tuhuma za uvamizi wa shamba la watu wanaomiliki aridhi ya watanzania.

  Hivyo iliwalazimu ndugu za marehemu kuzuia mwili kuzikwa hadi uchunguzi wa kitaalamu utakapothibisha sababu ya kifo cha ndugu yao, niliombwa nika wasidie kusimamia kazi hiyo ilyofanywa na dr kutoka wizara ya afya na usitawi wa jamii.

  Katika tukio hili nilikutana na Dr Makatta yuleyule niliyekutana naye kule Tarime kwenye uchunguzi wa marehemu waliouwawa nyamongo..
  Uchunguzi ulifanyika na ulianza saa sitta na nusu hadi saa nane na dakika 45, maelezo yote yako mikononi mwa wahusika...mwanasheria wa familia na familia yenyewe.

  Mungu waone hawa Binadamu uliowaumba kwa udongo, wenye hukumu ya asili ya kurudi kwa udongo, waone wanawahukumu raia wenye miili ya udongo kama yao, ee Mungu watazame kwa jicho upendalo.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Haitoshi kulalamika na kunung'unika kama watu wanaona kuna haki zimevunjwa mikononi mwa dola zungumzeni hadharani, washtakini hadharani na wahusika wawajibishwe au vinginevyo muache kunung'unika. Nashangaa pamoja na madai ya mauaji ya mikononi mwa polisi hakuna kesi iliyoletwa dhidi ya serikali au jeshi au hata watu binafsi kuhusika na mauaji hayo; sasa mnafanya uchunguzi ili mjue tu mtu amekufa halafu mnaenda kulia?

  Ndio nikabakia kujiuliza; baada ya kushindwa kufanya ibada ya maombolezo na baaday a kushindwa kupatiwa majibu huku madai yakitolewa kuwa Jeshi la polisi limekuwa likiua wananchi with impunity Chadema au wanasheria wake hawajafungua kesi yoyote aidha ya madai au ya jinai dhidi ya wahusika mbalimbali. SIyo Arusha, siyo Kiteto, siyo Tarime, na sitarajii itafunguliwe huko Babati.

  Natarajia manung'uniko zaidi na malalamiko. Aidha hamna ushahidi wa kutosha wa kuwa haki za watu zimevunjwa au ushahidi mnao lakini hamna nia ya kuwawajibisha wahusika. Sioni chaguo la tatu.
   
 3. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Bwana ametoa, bwana ametwaa
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  uwoga wa kutishiwa kifo.
   
 5. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  mwanakijiji,

  ni kweli kwa usemayo mimi binafsi sipendi mtu anyelalamika tu aua mkosoaji tu asiyechukua hatua.
  kwa hili la watu kuuwawa na kufanyiwa uchunguzi, ni zuri sana na litaonekana lina manufaa ikiwa hatua zitachukuliwa dhidi ya wakosaji.
  but kwa kazi yangu na dr mteula wa serikali, inakamilika na taarifa inaandikwa kisha wanasheria na vyomba vya usalama vinashika nafasi yake moja kwa moja, ndio sababu kule tarime nilimpa report ile mwnasheria tundu lissu na huku pia nimempa mwanasheria wa familia ndiye mwenye majukumu yaliyobaki, mm kazi yangu ya kuthibitisha kitaalamu inakuwa imekomea hapo na ninasubiri kuitwa mahakamani tu kutoa ushahidi, hivyo nakuomba wewe kama mwandishi chukua jukumu hili la kuwauliza wanasheria hawa wanangoja nini, mbona hawaendi mahakamani?
  ansante.
   
 6. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45


  ok, kaka you are copied.
   
 7. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Katiba mpya, magamba out 2015 hapo ndio tutakuwa huru ndani ya nchi yetu wenyewe
   
 8. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,009
  Trophy Points: 280
  hatimae serikali ya ccm yauvaa rasmi mzimu wa kaburu, aliyetekeleza mauaji ya soweto.
  .
   
 9. F

  FRANK MICHAEL Senior Member

  #9
  Jun 18, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kiukweli police sasa ni maadui wetu hasa huku arusha jana nilikutana grup la police baa moja inaitwa mviringo hapa arusha yani nilitamani ningekua na bomu nijitoe muhanga, Mh Lema tunakutegemea be blessed hon slaa
   
 10. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji

  Mkuu, Wewe ni mkongwe ungewasaidia kufungua kesi kuliko na wewe tena kuendelea kulalamika
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Msaidie Nyakarungu, au ujanja wenu mbele ya laptop tu
   
 12. F

  FJM JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji, police, hakimu na serikali ni kitu kimoja na wote wako kwenye mission moja- kutuangamiza huku tukiona. Kuwafungulia mashitaka hawa utaanzania wapi? na utapata haki stahiki? Wanachokifanya CHADEMA ni sawa kabisa. Wanawashitaki the entire Mungiki group (ccm,police, judges etc) kwa wananchi ili wawape hukumu wanayostahili. We need to wipe them out of this earth, na ikiwezekana baada ya kuwaondoa iwekwe sheria inayosema ni MARUFUKU kuanzisha chama (hata kama ni cha kulima mboga mboga) na kuiita CCM.
   
 13. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji nakubaliana na unayosema, ndivyo inavyotakikana - except nakuomba ukumbuke kuwa hawa watu hawana tofauti na makaburu wa Afrika Kusini wakati uleeee ! Hapa najaribu kufikiria ingekuwaje kama ndugu zao waliouawa Soweto wangetaka kuwafungulia mashtaka wauaji, sana sana labda na wao wangepotezwa. Hivyo walichofanya na kilichokuwa ndani ya uwezo wao ni kulalamika bila kuchoka na nadhani kelele zao zilikuja kufanikiwa baadaye. Je, unataka akina Chenge, Rostamu au hata Kikwete mwenyewe sisi wanyonge ndio tuwafungulie kesi ? Bila shaka unashuhudia kwa macho yako jinsi hata mbunge anavyoweza kuzimwa, sembuse sisi - naona hututakii mema.
   
 14. Esoterica

  Esoterica Member

  #14
  Jun 19, 2011
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tundu Lissu upo? Chukua hatua Mh............................
   
 15. Esoterica

  Esoterica Member

  #15
  Jun 19, 2011
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh Tundu Lissu upo? Chukua hatua bwana......................
   
 16. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #16
  Jun 19, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hii nchi imetekwa nyara na viongozi wake wenyewe, kwa miaka 50 wamejiwekea mfumo imara ambao unailinda hii serkali iliyo saliti wananchi wake . Chadema na wanasheria wao pekee hawawezi kubadilisha chochote, ni jukumu la kila raia mpenda haki na maendeleo wa nchi hii kuamka na kusema basi imetosha! Bunge, mahakama, baraza la mawaziri, wazira ya mambo ya ndani au ikulu haviwezi tena kusimamia haki za wanyonge kwa mazingira yaliyopo hivi sasa? Kupeleka kesi mahakamani ni kupotezeana muda na raslimali kwa sababu haki haitatendeka. Hatua zinazohitajika ni zile ambazo zinalenga kuwaondoa hawa wabakaji wa demokrasia kutoka madarakani na kuhifadhi documents zote zinaonyeshwa maovu yao. Watapelekwa mahakamani baada ya ukombozi na kuunda serkali inayoongozwa na katiba inayofuata haki na kuthamini maisha ya raia wake wote.
   
 17. Esoterica

  Esoterica Member

  #17
  Jun 19, 2011
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh Tundu Lissu upo? Chukua hatua bwana......................
   
 18. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #18
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Nyakarungu

  Ndugu yangu hebu acha kudanganya wana Great thinker....naamini ulieendika mada hii ni yule unayejiita daktari (SIYO DAKTARI BALI TABIBU) uliyeshiriki post morterm KULE Tarime kama daktari wa familia....kwanza tambua hivi ....Dr Makata ni senior pathologist mwenye ujuzi wa Mambo ya forensic medicine, hivyo si ajabu kwenda na kushiriki kwenye issue hizo...katika Tanzania yetu sidhani kama tuna mabingwa zaidi ya wawili katika eneo hilo (MD, Master in Pathology Japan, PHD in Pathology Japan, Postdoc in forensic Medicine Australia).....na wewe ndugu yangu ni CLINICAL OFFICER, ni makosa hata kujiita daktari.....Wacha kujenga chuki ndani ya jamii kwa inferiority complex yako.......
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #19
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mzee Mwanakijiji...hata pangekuwa na Mabingwa wa sheria kama kina OCAMPO wa ICC pale CHADEMA wasingeweza kufungua kesi....kesi ya namna hiyo inategemea sana ushahidi wa kitaalamu toka kwa timu ya madaktari waliofanyia uchunguzi....sasa kwa mtindo wa FAMILIA kuwakilishwa na MATABIBU (pengine kwa uelewa mdogo wa wahanga) badala ya MADAKTARI katika uchunguzi, wategemea nini hapo.......
   
 20. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #20
  Jun 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  We umetoka usingizini? sema unawajuwani hao wawili siyo useme Tanzania!
   
Loading...