Post-Mortem: Sababu Za 57.16% Kutokupiga Kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Post-Mortem: Sababu Za 57.16% Kutokupiga Kura

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Superman, Nov 6, 2010.

 1. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Wanajukwaa la Jamii

  Hatimaye NEC imetangaza matokeo yote rasmi ya Uchaguzi Mkuu 2010. Katika mchanganuo wa wapiga kura NEC imetoa takwimu zifuatazo:

  Wapiga Kura Waliojiandikisha ni: 20,137,303.

  Na Waliojitokeza Kupiga Kura Ni: 8,626,283 sawa na asilimia 42.84%.

  Hii ina maana waliojiandikisha lakini hawajapiga kura ni: 11,511,020 sawa na asilimia 57.16%.

  Ni jukumu letu pia kuangalia ni kwa nini wapiga kura wengi hawakujitokeza. Tusaidiane kuangalia sababu hizi nami nitaanza kwa chache ambazo nimezifanyia utafiti kwa kuwauliza wale ambao walijiandikisha lakini hawakuweza kupiga kura:

  1. Hawakuona majina yao ingawa walijiandikisha
  2. Walikuwa safarini nje ya Wilaya, Mkoa au Nchi
  3. Walikuwa sehemu tofauti na waliojiandikisha
  4. Walikuwa wagonjwa
  5. Kuna ambao wamefariki katika kipindi cha uboreshaji wa daftari na kipindi cha kupiga kura
  6. Kuna walioondolewa kwa madai kuwa wamekufa lakini wako hai.

  Je, kwa maoni au utafiti wako ni sababu gani nyingine zilizowafanya watu wasijitokeze kupiga kura?
   
 2. jambotemuv

  jambotemuv JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Japo wengi waliyimwa kupiga kur kwa mizengwe kama ulivyoainisha, bado idadi ilotolewa na tume ni kubwa mno na vigumu kuiamini. Zinabaki kuwa tarakimu tume ilzobuni ili kuhalalisha matokeo walojitengenezea. Japo wengi walinyimwa kupiga kura, zilizopigwa na kuhesabiwa hazikuhusika kwenye kutengeneza matokeo. Yaelekea tume iliamua kujitahidi idadi ya kura katika kila kituo iwiane na alizopata mkwere. Masanduku ya Tunduma yangefanikiwa kuingia walivyokusudia labda idadi ingezidi hata 20m na wangezua maelezo mengine.
   
 3. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Je, vitisho vya vyombo vya dola vinaweza vikawa viliwaogopesha baadhi wakaogopa kujitokeza?
   
 4. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Una maana waliojitokeza ni wachache kuliko idadi iliyotolewa na NEC? Na kama ni hivyo kwa nini wengi hawakujitokeza?
   
 5. K

  Keil JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna baadhi ya wapiga kura na hasa wale ambao walikuwa na mwelekeo wa kuvipigia kura/kuunga mkono vyama vya upinzani, shahada zao za kupigia kura zilinunuliwa ili kupunguza makali ya ushindi. Kwa kuwa shahada za kupigia kura zina picha, zisingeweza kutumiwa na mtu mwinginena hivyo ziliishia kutupwa au kuchomwa moto.
   
 6. October

  October JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wengi hawakupiga kura kwa sababu katika chaguzi nyingi Tanzania matakwa ya wananchi huwa hayaheshimiwi.
  Mara nyingi chama tawala huchukua ushindi kwa nguvu na kuiba kura, jambo linalowakatisha tamaa wapiga kura wengi, ndio maana mwaka huu vijana wengi walikua tayari kuhatarisha maisha yao ilio kulinda udhalimu huu wa tume ya uchaguzi.
   
 7. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2010
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Uchaguzi umemalizika, mshindi amepatikana na sasa watanzania wanapaswa kuchapa kazi ili kujiletea maendeleo huku wakitafakari uhalisia wa idadi ya waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura kwa kulinganisha na takwimu za idadi ya watu katika Tanzania.
  Katika hali ya kawaida, katika maeneo mengi, idadi ya watoto ni zaidi ya mara mbili ya watu wazima.
  Kwa hali hiyo, ikiwa waliojiandikisha kupiga kura ni 20m basi idadi ya watu wote ni zaidi ya 60m.
  Kuna umuhimu wa kuandikisha watanzania wote na kuacha kumbu kumbu nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa, kijiji kwa kijiji , kata kwa kata, wilaya, mkoa na mwisho taifa. Hii inawezekana na gharama inaweza kuwa ndogo kuliko hata inayotumika kwa sensa ya siku moja ambayo haina usahihi.
  Uzazi, vifo na ugeni au kuhama vinafanyiwa update monthly na taarifa inatolewa kila ngazi bila kukosa.
  Kwa njia hii tunaweza kuwa na reliable data na kuweza kufanya uchunguzi kunapotokea hali kama ilivyokuwa kwa wapiga kura.
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Kazi iliyoko mbele ya wapinzani sasa hivi ni kuhakikisha katiba iliyopo inabadilishwa na mfumo mzima wa NEC nao ubadilishwe ili siku zijazo kura iwe kura kweli.Sasa hivi ni zoezi la kukamilisha wajibu wa kikatiba tu.
   
 9. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ana maana waliojitokeza ni wengi kuliko idadi iliyotajwa na tume. Ila tume imefunika kura nyingi sana za wapinzani wa ssm kwa upande wa uraisi, na ndio sababu Slaa amepewa kura chache kuliko wabunge wake pamoja na madai ya wapiga kura kusema walipiga tatu bila!
   
 10. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sababu ya msingi ni kutoiamini NEC na ilo limethibitika NEC ilipotangaza walioshindwa kuwa washindi
   
 11. L

  Logician Senior Member

  #11
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Je unapendekeza mfumo gani?
   
 12. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #12
  Nov 6, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Nitakuwa katika position nzuri ya kuchangia hapa baada ya kufanya analysis of the results...
   
 13. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #13
  Nov 6, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  baadhi ya wanawake walinukuliwa kusema hawakwenda kupiga kura kwa sababu walitaka kupiga kura tofauti na matakwa ya waume zao, hivyo kukatazwa na wanaume kupiga kura.
   
 14. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #14
  Nov 6, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu Kabla ya Yote ni Lazima tujiridhishe kwamba je hai wapiga Kura 20,000,000 walikuwepo kweli au kulikuwa na Wapiga Kura Hewa ili kutoa nafasi kwa Uchakachuaji?
   
 15. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #15
  Nov 6, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nadhani suala la CCM kununu shahada sehemu ambazo upinzani hupo juu ni moja ya sababu ya wapiga kura wengi kutopiga kura maana shahada zipo kwa wazee wa kuchakachua. Ni jambo lililo wazi viongozi kibao wa ccm ngazi ya shina walikuwa wanapita na kuorodheha majina ya waliojiandikisha na kuchukua namba za shahada ya mpiga kura pia walikuwa wanachukua namba za simu za wapigakura au namaba ya simu ambayo mpiga kura akipigiwa anaweza kupatikana hii hali JIMBO la MONDULI na HAI ninaushaidi nalo na TAKUKURU walishapelekewa taarifa la suala hilo lakini mmmmmmmmmmmmmmmh sasa mlitegemea nini. ndio hivyo waliopiga kura hao 42.84%
   
 16. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #16
  Nov 6, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni wazi kabisa kwa nchi za dunia ya tatu ambazo nyingi umri wa kuishi hauzidi miaka 55 ni ngumu kukuta idadi ya watu wazima ni kubwa kuliko ya watoto. Tunaelewa fika maskini wanazaa watoto wengi hivyo nchi kama Tanzania watoto ni wengi kuliko vijana na watu wazima maana wasichana wengi hadi kufika umri wa miaka 18 tayari anakuwa na mtoto ushahidi ni ongezeko la mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hadi tumebuni matangazo ya FATAKI.

  Na kwakuwa tunasema watanzania tupo kati ya 40ml hadi 42ml ni wazi haiwezekani tukaandikisha wapiga kura 19m au 20m ndio maana toka mwanzo watu walipinga idadi ya waliojiandikisha ilivyotolewa na NEC kuwa idadi hiyo si sahihi na ni mbinu na mipango ya kuwa na wapiga kura hewa ili mbinu zote zikishindikana kuiba kura GHOST VOTERS watumike kumpa ushindi mgombea wa CCM. Wakati tunalalama kwa hoja hizo wenzetu mlikuwa mnaangalia maudhurio ktk mikutano. SASA mnarudi kuuliza hivi ni kweli wapiga kura walikuwa 20m nasema hapana maana kulikuwa na GHOST VOTERS kama 4ml ili watumike kumpa ushindi aliyeshinda sasa.
   
 17. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #17
  Nov 6, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tume ilikuwa na mkakati rasmi kufanya ugumu utokee, watu wengi wakwame kujitokeza ili CCM ishinde bila nguvu, walishajua vijana wengi wamejiandikisha hivyo Tume ilijipanga kimkakati kama ifuatavyo:
  * Kuondoa majina ya vijana wengi. Mfano kule Mara na pia kukwamisha wale wa vyuo vikuu wasirudi vyuoni.
  * kupanga vituo vya mbali na makazi ambapo watu wengi walikata tamaa kutembea umbali. Hata spika Sitta alilalamikia hili.
  * kubadilisha vituo na kupanga vipya mbali na walipojiandikishia. Hili limeripotiwa maeneo mengi, mfano Ukonga, sinza, mwanza nk.
  * kuchelewesha vifaa na kufungua vituo. Kwingine walianza saa 4 hadi saa 6.
  * toka awali hawakutoa elimu ya wapiga kura. Kama sio vyama vya kiraia kama Tamwa na Policy Eorum, hali ingekuwa mbaya zaidi.
  *Tume iliacha wananchi wasielewe madhara ya kutokwenda kupiga kura kwani kwa Tume walidhani ni Faida kwa CCM kumbe wamejishusha na kupoteza hadhi kwa kuishindwa kazi. Wali-assume kuwa wako sahihi badala ya ku-rely ktk facts za vyama vya siasa na vya kiraia kuhusu umuhimu wa watu wengi kujua namna ya kupiga kura na kujitokeza siku ya uchaguzi. Hii ndiyo failure kubwa mno, wastep down kukwepa aibu hizi.
   
 18. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #18
  Nov 6, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hakuna mwamko wa kisiasi Tanzania!
  Watu wanadhani siasi ni mchezo mchafu, nk!
  Hii ni aibu!
   
 19. Companero

  Companero Platinum Member

  #19
  Nov 6, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  7. Waliogopa vitisho vya uwepo wa fujo na umwagaji wa damu
   
Loading...