Post mortem - kabla na baada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Post mortem - kabla na baada

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by WomanOfSubstance, Sep 22, 2009.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Poleni na kusherehekea Idd.

  Wengi tutakuwa hoi na hata mifukoni nako kutakuwa hoi bin taaban.Ninaomba tutathmini mwenendo mzima kuanzia mfungo hadi tamati tuliposherehekea kwa mapilau, vinywaji, muziki, ngoma, na yale yote yalioendana na shughuli nzima.

  Ninavyokumbuka, kabla ya mfungo, kuna watu walivunja jungu kwa maasi ya kila aina - miziki, ulevi wa kupindukia, na mengine mengi. Pia kama maandalizi, kuwa wana dada walibahatika kuolewa chapchap akiwemo rafiki yangu mmoja jina nalihifadhi. Nawaombea mola awajaalie ndoa yao idumu.


  Kipindi cha mfungo kilikuwa kipindi cha utulivu na tulijaaliwa amani na mwelekeo mwema kabisa. Ama kweli Ramadhani ilikuwa Karim kiukweli. Ikaja sikukuu........ maandalizi yaliwashughulisha watu kwa sana - maofisini kulikuwa hakukaliki - mara shopping ya nguo mpya, manunuzi ya vyakula, mradi full shangwe. Kuna watu walinuna kisa hawakununuliwa nguo mpya.

  Sikukuu yenyewe.... nilishuhudia hasa watoto wakiwa na furaha huku wakiwa maridadi wakielekea sehemu sehemu kujirusha ama peke yao au na wazazi/walezi. Wenye sehemu za starehe walivuna sana hizi siku mbili maana kama ni vyakula, vinywaji na vingine basi kilikuwa kipindi cha kuvuna.

  Mwenzangu unalo la kuhadithia?
   
Loading...