Posho za wabunge: Wamiliki hoteli Dodoma wamkana Makinda

Dodoma bei za Guest zipo chini sana,mimi mwaka jana mwez wa 6 nilala VICTORIALAND LODGE tsh 12000(self&superspot tv) napata chai asubuh&mwez wa saba nililala ZUBBY LODGE tsh 15000(self&superspot tv)tiles,mitaa ya Iringa load,yule bibi na wenzake ni WALAFI tu.
 
Anna aliamua tu kutetea nyongeza ya posho walizojiongezea kinyemela bila kuwa na data za hali halisi ya gharama za maisha ya Dodoma. Sijui wabunge wote ni mafisadi?!
 
Mhhhhhhhhh! muda wote huo walikuwa wapi kutoa hayo maelezo?au ndo kusema akili zao zimeamka sasa!
.........
Hata hivyo, Mwenyekiti wa chama hicho, Chavuma Taratibu, alisema uchunguzi uliofanywa na chama hicho ................nadhani ndio jibu
 
Chama cha Wamiliki wa Hoteli na Nyumba za Kulala Wageni mkoani Dodoma, kimekanusha madai ya kupanda kwa gharama za huduma za malazi zilizoongeza gharama za maisha kwa wabunge kama ilivyotangazwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda. Mwishoni mwa mwaka jana, Makinda alitangaza kuwa posho za wabunge zimeongezwa kutoka Sh 70,000 mpaka Sh 200,000 kwa siku, kutokana na kupanda kwa gharama za maisha, kwa wawakilishi hao wawapo katika vikao vya Bunge. Alisema sehemu ya gharama hizo ni pamoja na malazi, kwa kuwa baadhi ya nyumba zilizokuwa zimekodiwa na wabunge wa Bunge la Tisa, bado wanazimiliki na hivyo kusababisha wabunge wapya kupanga hotelini, ambako gharama ni kubwa.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa chama hicho, Chavuma Taratibu, alisema uchunguzi uliofanywa na chama hicho wiki mbili zilizopita, umebaini kuwa kupanda kwa gharama za maisha mjini Dodoma hakulingani na majiji ya kibiashara ya Mwanza, Arusha, Mbeya, Morogoro na Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taratibu, uchunguzi huo umebaini kuwa mkoa wa Dodoma una nyumba za kulala wageni 413 zenye vyumba 3,973 ambavyo gharama zake ni kati ya Sh 5,000 na Sh 45,000 kwa siku, kwa kuzingatia ubora wa vyumba na huduma zilizopo.

“Kwa nyumba za kulala wageni zenye vyumba vinavyounganisha huduma za vyoo na bafu, gharama yake ni kati ya Sh 10,000 na Sh 20,000 kwa kuzingatia ubora wa vyumba,’’ alisema Taratibu. Alisema mbali na vyumba hivyo, pia vipo vingine maalumu vyenye hadhi ya juu ambavyo kwa siku ni kati ya Sh 80,000 na Sh 150,000 lakini vyumba hivyo Dodoma viko 25 tu. Alisema wanafahamu kuwa hakuna mbunge anayeweza kupanga vyumba hivyo maalumu vyenye hadhi ambavyo pia vinatofautiana bei kulingana na umaarufu wa hoteli na ubora wa vyumba vya kulala wageni vilivyopo katika hoteli husika.

‘’Kwa tamko hili, tunapenda kufuta uvumi wa kisiasa kuhusu kuongezeka maradufu kwa gharama za maisha, hatua hiyo inalenga kuvuruga soko la huduma zetu mkoani hapa kwa kuwaogofya wageni na watalii na hivyo kuathiri biashara hizo na huenda hata mapato ya serikali yakapungua kutokana na kodi inayotoza,” alisema Taratibu.

Alisema kelele za kudai posho haziwezi kuthibitishwa kwa kauli zisizofanyiwa utafiti wa kina, licha ya kuwa hali ya uchumi imeyumba kwa nchi nzima, kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta, kushuka thamani ya sarafu na uzalishaji duni uliosababishwa na tatizo la umeme uliodumu kwa mwaka mzima uliopita. Wamiliki hao wa hoteli wanaungana na vyama vya siasa, asasi za kijamii, viongozi wa dini na baadhi ya wananchi, kupinga nyongeza hiyo ya posho.

Chanzo: HabariLeo

Namsubiri mwenyekiti wa totoz za Dodoma naye aseme kama nao wamepandisha dau ili ukweli ujulikane!
 
Tunawalea sana wabunge wetu... we have such low expectations.
Hawa wajengewe hosteli na serikali, kwanini walale guest house?.. na mbunge wa Dodoma mjini nae analipwa posho?
 
Tunapishana nao sana kwenye viji corridor vya gest ambazo wote tunalipia elfu 20,sasa inashangaza huyu bibi kudanganya umma wa waTz kiasi hiki na Gest zao maarufu ambazo ni bei cheap nazijua sana ambapo waonaishi humo wengi wao ni hawa Wabunge
 
Tunawalea sana wabunge wetu... we have such low expectations.
Hawa wajengewe hosteli na serikali, kwanini walale guest house?.. na mbunge wa Dodoma mjini nae analipwa posho?

Hahahahahaha mkuu tena huyu bwana Malole cjui kapotelea wapi yani baada ya Uchaguzi hajarudi tena kwa wananchi kutatua kero zaidi,lakn ndio faida ya kuchagua Magamba
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom