Posho za wabunge: Wamiliki hoteli Dodoma wamkana Makinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Posho za wabunge: Wamiliki hoteli Dodoma wamkana Makinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Jan 11, 2012.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Chama cha Wamiliki wa Hoteli na Nyumba za Kulala Wageni mkoani Dodoma, kimekanusha madai ya kupanda kwa gharama za huduma za malazi zilizoongeza gharama za maisha kwa wabunge kama ilivyotangazwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda. Mwishoni mwa mwaka jana, Makinda alitangaza kuwa posho za wabunge zimeongezwa kutoka Sh 70,000 mpaka Sh 200,000 kwa siku, kutokana na kupanda kwa gharama za maisha, kwa wawakilishi hao wawapo katika vikao vya Bunge. Alisema sehemu ya gharama hizo ni pamoja na malazi, kwa kuwa baadhi ya nyumba zilizokuwa zimekodiwa na wabunge wa Bunge la Tisa, bado wanazimiliki na hivyo kusababisha wabunge wapya kupanga hotelini, ambako gharama ni kubwa.

  Hata hivyo, Mwenyekiti wa chama hicho, Chavuma Taratibu, alisema uchunguzi uliofanywa na chama hicho wiki mbili zilizopita, umebaini kuwa kupanda kwa gharama za maisha mjini Dodoma hakulingani na majiji ya kibiashara ya Mwanza, Arusha, Mbeya, Morogoro na Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taratibu, uchunguzi huo umebaini kuwa mkoa wa Dodoma una nyumba za kulala wageni 413 zenye vyumba 3,973 ambavyo gharama zake ni kati ya Sh 5,000 na Sh 45,000 kwa siku, kwa kuzingatia ubora wa vyumba na huduma zilizopo.

  “Kwa nyumba za kulala wageni zenye vyumba vinavyounganisha huduma za vyoo na bafu, gharama yake ni kati ya Sh 10,000 na Sh 20,000 kwa kuzingatia ubora wa vyumba,’’ alisema Taratibu. Alisema mbali na vyumba hivyo, pia vipo vingine maalumu vyenye hadhi ya juu ambavyo kwa siku ni kati ya Sh 80,000 na Sh 150,000 lakini vyumba hivyo Dodoma viko 25 tu. Alisema wanafahamu kuwa hakuna mbunge anayeweza kupanga vyumba hivyo maalumu vyenye hadhi ambavyo pia vinatofautiana bei kulingana na umaarufu wa hoteli na ubora wa vyumba vya kulala wageni vilivyopo katika hoteli husika.

  ‘’Kwa tamko hili, tunapenda kufuta uvumi wa kisiasa kuhusu kuongezeka maradufu kwa gharama za maisha, hatua hiyo inalenga kuvuruga soko la huduma zetu mkoani hapa kwa kuwaogofya wageni na watalii na hivyo kuathiri biashara hizo na huenda hata mapato ya serikali yakapungua kutokana na kodi inayotoza,” alisema Taratibu.

  Alisema kelele za kudai posho haziwezi kuthibitishwa kwa kauli zisizofanyiwa utafiti wa kina, licha ya kuwa hali ya uchumi imeyumba kwa nchi nzima, kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta, kushuka thamani ya sarafu na uzalishaji duni uliosababishwa na tatizo la umeme uliodumu kwa mwaka mzima uliopita. Wamiliki hao wa hoteli wanaungana na vyama vya siasa, asasi za kijamii, viongozi wa dini na baadhi ya wananchi, kupinga nyongeza hiyo ya posho.

  Chanzo: HabariLeo
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Walikua wanataka kula kwa mgogo wa mahoteli ya watu, shame on them
   
 3. JS

  JS JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kaumbuliwa vibaya huyu Bibi......
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Haaaaaaa du kaumbuliwa si kidogo :-D
   
 5. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,216
  Likes Received: 10,583
  Trophy Points: 280
  Nasubiri kwa hamu vipindi vya Bunge vutakapo anza maana sijui huyo mama atatueleza nini watanzania. sijui litaficha wapi sura yake kama nyani.
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Mhhhhhhhhh! muda wote huo walikuwa wapi kutoa hayo maelezo?au ndo kusema akili zao zimeamka sasa!
   
 7. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  BIBI WA JAZBA/PANIC hajawahi kuliongolea suala hilo tangu wampinge, kaamua kuwa silence. ipo siku atasema tu ili azomewe vizuri
   
 8. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  walihitaji kufanya utafiti na kuwa na collective voice, sio kila mtu kulipuka na ksema lote. mambo mazuri hayataki haraka
   
 9. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  mambo ya bi kidude hayo.
  kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake
   
 10. M

  Megawatt B JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  The Citizen wameandika vizuri - kwamba kwa ufahamu wao, hakuna mbunge anayelala chumba kinachozidi Tsh.20,000/=
   
 11. M

  Maengo JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu hawakurupuki kama bi kiroboto wewe, wanafanya kwanza utafiti ili kuhakikisha kuwa watakachokisema ni sahihi.
   
 12. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Inakuwaje kiongozi mkubwa wa mhimili kama Bunge anatoa taarifa isiyotafitiwa. Hivi Bunge si lina kitengo cha utafiti na ukusanyaji wa habari na taarifa mbalimbali?
   
 13. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kukusanya habari na taarifa gani?
   
 14. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama makinda akiwa amekalia kiti cha spika naongea vitu ambavyo haviko kwenye kanuni hadi anasomewa kanuni na makamanda wa CDM, mnashangaa nini akilopoka uongo akiwa mtaani?
   
 15. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Laiti ingewezekana hayo mahoteli kuweka rate maalum kwa Wabunge wapenda posho (shilingi 140 000 kwa chumba kwa siku) ningefurahi sana!
   
 16. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Alituambia kama huna laki moja hujalala Dodoma kumbe uzushi!
   
 17. J

  John W. Mlacha Verified User

  #17
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  sema hatuna utaratibu wa kujiuzulu
   
 18. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #18
  Jan 11, 2012
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ...Kiroboto
   
 19. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #19
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Lile li bibi silipendi kwa sababu ni liongo sana,SHAME ON HER.
   
 20. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #20
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,600
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  Duh, Kweli hawa ni wenye nyumba!

  Alafu hawa wabunge na Mawaziri si wamenunua nyumba za srekali, nssf, ppf zote si zao?
  pia wengi wamepanga mtaani ambapo wanalipa kodi kati ya 300,000 na 500,000 kwa mwezi.
   
Loading...