Posho za wabunge CCM vipande - Makinda ameingilia kazi ya Dr. Kashililah | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Posho za wabunge CCM vipande - Makinda ameingilia kazi ya Dr. Kashililah

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Dec 15, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wakati hali ikiwa hivyo kwa wabunge, kada maarufu na waziri wa zamani katika Serikali ya Awamu ya Tatu (jina linahifadhiwa) ameweka wazi kuwa Rais Kikwete alikuwa hajasaini ongezeko hilo la posho kwa wabunge. Kada huyo alisema huenda Kikwete amekwama kusaini nyongeza hizo kutokana na malipo makubwa atakayopata mbunge kila mwaka ikiwa ni nje ya mshahara wake na malipo mengine. "Kama nyongeza hizi zitakubalika, basi mbunge angelipwa jumla ya sh 43,560,000 kwa mwaka kama posho ya vikao na fedha za kujikimu, ikiwa ni mbali ya mshahara na marupurupu mengine anayolipwa.

  "Kwa mwaka kuna vikao vinne vyenye jumla ya siku 132, hivyo kwa ongezeko hilo la posho kwa mwaka mbunge analipwa sh 43,560,000…wanaweza kupata mikopo benki hadi ya sh milioni 300 ambayo watailipa ndani ya miaka mitano, sh milioni 90 za kununua gari na pia hupata posho kwenye vikao vya kamati ambayo ni karibu siku 62 kwa mwaka. Vikao hivyo pekee hulipwa sh milioni 7. 3 mwa mwaka pamoja na malipo wanapotembelea nchi za nje kikazi au hapa nchini," alisema kada huyo.


  Alisema pia mbunge hurudishiwa gharama ya mafuta lita kama 120 anaposafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ama fedha alizotumia akitoa risiti ya mafuta anapotumia gari lake binafsi.


  Kada huyo alisema Spika wa Bunge, Anne Makinda, amejinyakulia mamlaka yasiyokuwa yake kwa kutumia udhaifu wa utawala uliopo.
  "Mambo yote ya fedha yako mikononi mwa Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah na hadi sasa katibu ambaye alikuwa Uingereza wakati Spika anatangaza posho, amesikika na kusisitiza kuwa posho mpya hazina ruksa ya mamlaka," alisema kada huyo ambaye alieleza kushangazwa na ukimya wa Hazina na Ikulu juu ya suala hilo.


  Kada huyo wa CCM alisema kinachoonekana katika sakata hili ni
  fukuto pana ndani ya CCM na taasisi ya Bunge, hivyo ni vema likaangaliwa kwa mtizamo tofauti badala ya kuliona la kawaida kama masuala mengine.

  Tanzania daima
   
 2. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM na serikali yake wanachekesha sana. Hawa wabunge walishaanza kulipwa hii posho toka bunge la November (Kwa Mujibu wa Rai wa Leo). Katibu wa Bunge akadanganya kuwa nyongeza haijapandishwa. Spika akaja kuongea kinyume na Katibu wake kuwa tumetoa nyongeza. Hakuna hata mmoja kati yao aliyesema kuwa wanasubiri au wamepeleka maombi kwa Rais. Halafu kingine cha kujiuliza hapa Rais anasaini kama nani? Nauliza hivi bunge ni mhimili mmojawapo wa serikali, nani ni msimamizi wa maslahi ya wabunge? Hapa linakuja suala jingine, je ni nani msimamizi wa maslahi ya Rais, je bunge linaweza kukwamisha malipo ya Rais kama yanazidi kiwango? Naona hili suala la posho linachukuliwa kisiasa zaidi kuliko kuliona kama moja ya masuala muhmu katika usimamizi wa fedha.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nchi inapokuwa na uongozi dhaifu matokeo yake kila mmoja anaamua anavyotaka.

  Dalili kubwa kabisa ambayo hujitokeza wakati nchi haina uongozi madhubuti ni pale viongozi wanapochukua hatua ya kutumia nguvu bila akili katika kutetea maslahi yao na kuzima haki wanazodai raia.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wakenya wameliona hili walipoandikwa kwenye magazeti yao kama ifuatavyo: "Tanzania greatly likes to be recognised for her ‘internationalist' policies, with her leaders spending more time strutting the world than they do in their own country, though the facts show they are quite parochial."
   
 5. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Serkal tz kila mtu kivyake!kila nikikumbuka sababu alizozitoa makinda juu ya kupanda kwa posho nachoka kabisa
   
 6. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2011
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Tulipowachagua vipofu kutuongoza mlitegemea nini? Mheshimiwa aliposema hajui ni kwanini Tz ni masikini watu hawakumwelewa kwani hata wao hawajielewi. Maana yake ni rahisi sana, haelewi anaongoza watu wa aina gani na taifa lipi. Yanayotokea leo ni matunda ya uchaguzi mbovu wa rais na wabunge. Vumilieni maumivu zaidi kwa next four years nadhani mtapata somo. Niliwakumbusha kabla ya uchaguzi, lakini sikio la kufa!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 430
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hapa kunajitokeza umuhimu wa kuingiza mabadiliko katika katiba yatakayocheki mamlaka za Bunge, Rais na Mahakama katika suala zima la maslahi. Kwa mfano; Rais wakati ana mamlaka ya kuidhinisha/kukataa posho itakayopendekezwa na wabunge kama ilivyo sasa, ni nani wa kumdhibiti Rais atakapoamua kujilimbikizia au kujipandishia mshahara/posho? Je Mahakama itakuwa na uwezo gani wa kusimamisha malipo yatakayoonekana si halali kulingana na sheria, kanuni na hali halisi ya uchumi wa nchi?
   
 8. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwa hili mimi natamani wangekuwa chenga na si vipande tu. Hata wabunge tulionao bila ya kujali chama ni wachumia tumbo tu. Labda kidogo kwa mbaaaali Zitto.
   
 9. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  kwakweli CCM inatutesa sana. yaani wasomi na vijana kama sisi badala ya kutumia mishati yetu kujenga nchi kama nyerere alivyodhani itakuwa tumepaswa kuanza kazi ya kugombea uhuru upyaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!

  ebu cheki mwenyewe vichwa vya ukweli vinavyopata moto hapa JF!!!!mara inginewe nashindwa kufanya kazi kutwa!

  fuc***g CCM!
   
 10. s

  sangale sabore Member

  #10
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ujue unaweza kuwa na akili ya darasani lakini kichwani ukawa unamatatizo kama uyo mama
   
 11. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #11
  Dec 15, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,874
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  KIUCHUMI CLASSICAL, (si
  kimaadili): Kitendo cha
  wabunge kuongezewa POSHO
  ni cha KUPONGEZWA
  KABISA!!!!! kwa kuwa: 1. Posho
  ni INCENTIVE TO WORK. Hivyo
  ufanisi wa mbunge utaimarika
  ktk kutumikia wananchi, 2.
  Kitendo hiki kitashawishi
  ELITES WA NCHI HII kuhamia
  bungeni 2015!! hivyo bunge
  litaingiliwa na wataalam (who
  search for green pasture)
  watakaokuwa chachu ya
  maendeleo kupitia mipango
  na maamuzi..., 3. Posho
  ITAPUNGUZA (sio kumaliza)
  tabia ya wabunge kujihusisha
  na ubadhirifu, na biashara
  nyingine.
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Chama kitakachoingia madarakani kitakuwa na hali ngumu sana ya kuinusuru nchi kwa vile Kikwete ataiacha nchi katika deni kubwa mno.
   
 13. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #13
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Safari bado ni ndefu
   
 14. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #14
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Katibu wa Bunge ni mnafiki! anajua nini kinaendelea kwani na yeye kama mtendaji mkuu wa bunge anaufahamu mpango mzima. Kilichomfanya kusema uongo kuwa posho hazijalipwa ilhali zimelipwa alitaka tumuelewe vipi? Afadhali mama wa watu amesema hadharani kuwa posho hizo zimelipwa. Cha msingi posho hizo zifutwe na tuangalie namna ya kutatua matatizo ambayo ni kero kwa Watz badal;a ya kuwalipa wanaopiga usingizi mjengoni!
   
 15. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #15
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kazi ipo ....
   
Loading...