kluger
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 2,093
- 1,897
Wasalaam,
Hivi karibuni wakati wa kupitisha budget ya serikali palipitishwa maamuzi mazuri sana ya kukuta kodi viinua mgongo vya wabunge wetu na waheshimiwa wengine huko serikalini, napongeza sana sana hatua hii.
Ikumbukwe kuwa kodi siku zote ni fair haichakugui wa kupendelea upande wowote, yaani palipo na mapato ni lazima kodi ya nchi pia ikatwe, hili ni muhimu na lakuheshimika kwa watu wote ili kupata huduma bora kwa watu wa chini wasiojiweza lakini watu wote kwa ujumla na maendeleo ya nchi.
Ilinishangaza kuona wanaotuongoza kuelekea kwenye maendeleo, wakilialia kuomba waendelee kutokulipa kodi.
Sasa tukija suala la posho, serikali hii imefuta posho zote za vikao, sasa kwa nini wabunge hawa waendelee kulipwa posho??tupo nchi moja kwa nini double standards? Kama hakuna posho za vikao iwe kwa wote ili kufikia malengo.
Kazi ya ubunge si ya kudumu, wapo wabunge ambao wanakazi zao za kudumu na hulipwa huko, lakini pia wapo wengine ni wafanyabiashara wazuri na vipato vyao vikiwa pale pale.
Ubunge ni Kazi ya wito, kutumikia wananchi ili kuwasaidia kupata maendeleo yao. Sasa posho ni ya nini wewe ukiwa hapo mjengoni kwenye Kazi za bunge zinazokufanya uitwe mbunge??
Mheshimiwa Rais nakuomba futa Posho hizi za wabunge ili kuleta maana ya usawa katika malipo ya posho katika nchi hii. Viongozi wawe na hali ya kuwajibika kwa vitendo.
Ahsanteni.