Posho Za Madiwani Juu!!!

Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
613
19
WanaJambom wenzangu nawasalimu.... Hii habari nimeikuta kwenye "www.ippmedia.com" kidogo imenchanganya.... Nina maswali kadhaa nimekuwa najiuliza, "hawa Madiwani walifutwa miaka flani nyuma mpaka nadhani BM alipowarudisha mwaka 1995". Nakumbuka hoja ya kuwarudisha ni kuharakisha mboreko wa maisha na kuleta maendeleo katika vitongoji/majimbo yao ya uchaguzi. Sasa miaka 10 baadaye kwa kweli sijaona kikubwa waheshimiwa hawa walicholeta zaidi ya kutafuna "Posho"... Sasa leo naona wameongezewa posha, ambayo ukumbuke inagharimiwa na Halmashauri husika, sasa hapo jamani si matumizi ambayo hayana faida?? Kuna Mbunge "POSHO", DC, DED, Watendaji Kata na listi goes on ambao wote hawa wanatakiwa wapate "POSHO" za vikao on top ya mishahara. Sasa with our Cabinet ya 60 people na Madiwani, Wabunge na wengineo wanaotimia takribani 1000 nchi yetu kweli itafika?? Kila kikao, "Pesa", kila mwezi "Pesa" na wale walalahoi maendeleo "Kapa!"

Jamani naomba hili wale mliokuwa katika mlengo wa kujua maswala ya maendeleo mtusaidie kutushauri manake mimi hapa kwa kweli nimechoka mbaya!!!

Madiwani posho juu
2007-12-14 09:42:39
Na Charles Masayanyika, PST Kiteto


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Mizengo Pinda, amesema kuwa serikali imeboresha posho na stahili za madiwani ambazo zitalipwa na halmashauri zenyewe kupitia vyanzo vyao vya mapato.

Alizitaja posho hizo kuwa kila mwisho wa mwezi, diwani atalipwa Sh. 60,000 na kwamba posho ya kikao imepanda hadi kufikia Sh. 40,000.
Kwa upande wa wenyeviti wa halmashauri, alisema watapata posho ya Sh. 100,000 kila mwezi, huku meya atakuwa akipata kati ya Sh. 150,000 hadi Sh. 350,000.

Hata hivyo, Waziri Pinda alisema serikali italipa kiinua mgongo cha mwisho wa utumishi toka Sh. 540,000 hadi kufikia Sh. 1,980,000 baada ya kumaliza kipindi chao cha muda wa miaka mitano na akaeleza kuwa suala la usafiri, matibabu na gharama za mazishi bado linashughulikiwa na serikali.

Alisema ongezeko hilo la posho limetolewa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 1982 ya kanuni za madiwani kuwa na uwezo wa kujitosheleza na kujenga heshima ya nafasi hiyo kama walivyo madiwani wengine wa nchi za mataifa ya Ulaya badala ya kujiingiza katika mianya ya rushwa.
SOURCE: Nipashe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom