Posho ya vikao ikifutwa, 2020 tutakuwa na wabunge halali bungeni

Huu ni mtego mkubwa sana kwa chadema sijui kama watachomoka..

hata kama ni chadema ndio wana tamaa hatutawavumilia na wewe Ruttashobolwa tuungane kupiga kelele kwa hili hata kama hoja italetwa na chadema kupinga hili usionyeshe mahaba kisa tu kaleta hoja mbunge wa chadema, TAIFA Kwanza vyama baadae.
 
Last edited by a moderator:
Kwani enzi za mwalimu wabunge walilipwa posho za vikao?Wajuzi tupeni hii.Ingawa wengine wapo bungeni kulinda maslahi yao ya kibiashara na si kutamani posho,si huwa tunaona wabunge ambao hawabuni majibu ya changamoto yoyote bali husubiri matukio wajioneshe kidogo kama wapo na ni wabunge.
 
Itasababisha matajiri kuweza kuwa wabunge maana wanazitegemeaga hizo kwenye kampeni!
 
Safari hii najua Zitto atakuja na hoja binafsi kuhusu hili jambo na atajenga hoja kwa kusema tumuunge mkono raisi wetu katika kubana matumizi.

Hiki kitakuwa kipimo kizuri kwa spika na wabunge wake.
Mibunge ya CCM ambayo ndio mengi haiwezi kukubali hii!
 
Kuna kitu naomba mnisaidie. Hivi ukiondoa hizo posho je huwa wanapewa Per diems, if not, how will they survive while there?
Per diems zipo pale pale! Hiyo sitting allowance ni ya kukalisha masaburi kwenye viti vya bungeni!!
 
hoja hii ikipelekwa bungeni haitapita na hapa wabunge watakuwa kitu kimoja hakutakuwa na sisiem wala ukawa wote watapinga posho zao zisifutwe.
lakin ukiangalia kiukweli hizi posho ndo zinafanya watu wapigane marungu kwa kugombea ubunge.
hoja hii isiwe ya wabunge iwe ya wananchi ndo itapita, wote km tunaweza tuwaombe wabunge waondoe baadhi ya posho zao ili watusaidie wananchi kupata baadhi ya huduma za msingi.
kama mbunge anakataa mil 90 anataka mil 120 kwa ajili ya kununua gari sidhani km anaangaia maslahi ya mwananchi wa hali ya chini.
na hizo gari zinamtembelea mwananchi wa wapi mbona huwa tunaziona tu beach na viwanja vingine dsm na hazionekani vijijini.
km mwanasiasa anpata posho ya kukaa basi mwalimu ya kusimama darasani, halikadhalka wanataaluma wengine wapate posho kulingana na huduma zao
 
Rushwa itapungua hata kesi zinazohusu uchaguzi zitapungua.
je ikifutwa wabunge gani wataumia? na ikiletwa pendekezo la kuifuta wabunge wataunga mkono?

naomba wabunge wamuunge rais mkono kuondoa matumizi yasiyo na lazima, kwa kuwa mnapata posho ya kujikimu msipokee posh ya kukaa.
Je unajua tofauti ya sitting allowance na perdiem?Mbona sitting allowance ni kidogo sana ukilinganisha na perdiem?Labda useme posho zote pamaja na perdiem inayokadiriwa kuwa zaidi ya laki 2 kwa siku zifutwe ndo unachosema kitatokea.Ila kama perdiem ikifutwa wabunge wataishije Dodoma?Sitting allowance ni kama elfu 70 tu(ambayo zzk aliikataa)Lakini anapokea perdiem ambayo ni kubwa zaidi
 
Rushwa itapungua hata kesi zinazohusu uchaguzi zitapungua.

Je, ikifutwa wabunge gani wataumia?

Ikiletwa pendekezo la kuifuta wabunge wataunga mkono?

Naomba wabunge wamuunge Rais mkono kuondoa matumizi yasiyo na lazima, kwa kuwa mnapata posho ya kujikimu msipokee posho ya kukaa.

nyoo thubutu hayo maneno mwambie s.nchambi kama mtaelewana
 
kuna mtu atatafunwa mbichi pale bungeni ngoja dj asikie huo upuuzi wa kuondoa ruzuku
 
Unaunda uadui Na MBOWE

Kumbe mnamuogopa mbowe daaah hatariiiii yule ni kiboko yenu haongwi, harubuniwi, hadanganywi kama Dr mihogo, ana misimamo kama ya Hitler au G. Bush hawaogopi halafu haendekizi njaa hakika hata kama ni mimi ningekula sahan moja na nyie kila mtu anapenda pesa sio wachagga tuu cku hizi
 
Je unajua tofauti ya sitting allowance na perdiem?Mbona sitting allowance ni kidogo sana ukilinganisha na perdiem?Labda useme posho zote pamaja na perdiem inayokadiriwa kuwa zaidi ya laki 2 kwa siku zifutwe ndo unachosema kitatokea.Ila kama perdiem ikifutwa wabunge wataishije Dodoma?Sitting allowance ni kama elfu 70 tu(ambayo zzk aliikataa)Lakini anapokea perdiem ambayo ni kubwa zaidi

Naona kama unaelewa kinyume nyume. Perdiem ndiyo hiyo ndogo sijui ni 70 elfu, lkn sitting allowance ni laki 3,hii ilianzia bunge la katiba baadaye wakaing'ang'ania iendelee katika Bunge la JMT.
 
Magufuli futa ruzuku zote kwa vyama..ruzuku itolewe wakati wa uchaguzi mkuu tu.fedha ziende kwenye elimu na afya

Naunga mkono hoja kidogo.
Ruzuku isifutwe yote kabisa,angalau ufutwe 50% Siasa zinafaida na ikifutwa yote,basi ni matajiri tu ndio wataendelea kutawala
 
Kumbe mnamuogopa mbowe daaah hatariiiii yule ni kiboko yenu haongwi, harubuniwi, hadanganywi kama Dr mihogo, ana misimamo kama ya Hitler au G. Bush hawaogopi halafu haendekizi njaa hakika hata kama ni mimi ningekula sahan moja na nyie kila mtu anapenda pesa sio wachagga tuu cku hizi
Madude gani hayo unamsifia kilaza!!
 
Magufuli futa ruzuku zote kwa vyama..ruzuku itolewe wakati wa uchaguzi mkuu tu.fedha ziende kwenye elimu na afya

Ruzuku ya vyama vya siasa ni muongozo wa wakubwa wa huko " mbele". JPM hawezi kuifuta, vinginevyo atanyimwa misaada.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom