Posho si dhambi, dhambi ni posho inapokosa utu - Lema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Posho si dhambi, dhambi ni posho inapokosa utu - Lema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crashwise, Nov 29, 2011.

 1. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  "POSHO SI DHAMBI , DHAMBI NI POSHO INAPOKOSA UTU" - LEMA

  Nimetafakari sana niliposoma kwenye magazeti kuwa sisi wabunge tumeongezewa posho bila hata sisi kufahamu jambo hilo .
  Na kila mtu ametoa maoni mbali mbali juu ya jambo hili, ni kweli ni msimamo wa chama chetu (Chadema) kupinga posho mbali mbali zisizokuwa na tija na tulikubaliana hivyo kwenye vikao vya Chama Chetu vya Wabunge na kupinga mfumo wa posho uliopo kwa sasa ni msingi sahihi wa Chama kuonyesha hisia na ubadhilifu mkubwa unaotokana na ulipwaji mbaya wa posho kama ambavyo imejitokeza mara nyingi na hata hivi karibuni tumeshuhudia madudu mengi kwenye ripoti ya kamati ndogo ya Bunge iliyomchunguza Jairo. Lakini suala hili haliwezi kuepukwa kabisa na Chama kinajua ila utaritibu wa ulipwaji posho kwa watumishi mbali mbali wa umma ni tatizo kubwa na kuna mapungufu mengi sana ndio maana kupinga posho haina maana tu ya kupinga kiwango cha pesa anachopokea Mbunge au mtumishi yeyote wa UMMA bali mfumo mzima wa sera ya posho ili uweze kuwa na tija na kupunguza mianya ya wizi katika mfumo huu ambao umekuwa ukitumika vibaya kuliibia Taifa.

  Pengine sisi wabunge ni vyema tukatambua kwanini wananchi wanapiga kelele kuhusu posho nilishawahi kusema Bungeni wakati nachangia kwenye Wizara ya Ustawi wa Jamii kuwa mshahara wa Wabunge, posho mbali mbali za Wabunge pamoja na marupurupu mengine yanaonekana kuwa anasa pale watumishi wengine wa serikali kama Manesi, Asikari Magereza, Polisi, Makarani Mahakamani wanapolipwa chini ya shilingi laki mbili na nusu kwa mwezi na wakati huo huo wanasikia mwakilishi wao akipiga kelele Bungeni kuwa posho ya laki mbili kwa siku ni ndogo. Ndio maana nimesema "POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU", Na hapa lazima kutokee ugomvi wa kimasilahi na mgogoro mkubwa kati ya mwakilishi na anaye wakilishwa.

  Pengine masilahi anayopata Mbunge ni ya kawaida sana tena sana ila yanaonekana kuwa anasa pale ambapo yeye kama mwakilishi anapolipwa kiwango cha posho cha siku moja ambacho ni sawa na mshahara wa mpiga kura wake kwa siku thelasini. Mimi nafikiri namna peke ya wabunge kutetea masilahi yao bora kwanza ni kupigania masilahi ya wapiga kura wote Tanzania na tukifanya hivi kama Wabunge hakuna Mwananchi hatakayeshangaa kwanini Mbunge awe na masilahi bora kwani ubunge ni nafasi kubwa pia inayositahili heshima kubwa kwani ni uwakilishi katika jamii.

  Ebu jiulize wananchi wanaposikia Wabunge wamepewa milioni tisini kununua magari na wakati huo huo serikali imenunua bajaji kuwa ndio magari ya kubeba wakinamama wajawazito yaani (Ambulance) ni wazi kabisa wabunge wataonekani ni watu katili na walioenda bungeni kwa masilahi binafsi japo kuwa ukweli unabaki kuwa Wabunge wanahitaji magari imara na mazuri. Lakini Wabunge kama watafikiri Bajaj ni sawa kuwa gari la wakinamama wajawazito na wao kuchukua milioni tisini kwa magari ya binafsi bila kupiga kelele na kukataa unyanyasaji huu kwa wakina mama na Wagojwa, hivyo ni dhahiri kuwa ugomvi hapa katika posho na masilahi ya Wabunge utasababishwa na tofauti ya masilahi dhidi ya wale waliowachagua kuwatetea ,Hivyo namna pekee Mbunge anaweza kutetea masilahi yake bora bila kuingiliwa na na kubugudhiwa ni Mbunge kuanza kufikiria masilahi ya watu wengine ambao pia ni watumishi wa UMMA ambapo yeye ni mwakilishi wake.

  Nafahamu kuwa pamoja na kupinga mfumo mzima wa utaritibu wa posho ulivyo sasa tafakari ya kweli ni kwamba masilahi ya watumishi wa UMMA bado ni madogo sana kwa hiyo Uzalendo wa kweli sio tu kupinga masilahi bora bali serikali iwajibike kikamilifu kudhibiti wizi na ufisadi unaotokana na utaritibu mbaya wa ulipwaji posho, kuongeza makusanyo katika kodi mbali mbali, kutumia rasilimali za Nchi vizuri ili masilahi ya watu wote Nchi hii yaweze kuwa na tija kwa maisha ya Watanzania na watu wengi waweze kuishi maisha ya faraja na kutimiza malengo yao muhimu ya maisha
  Ndio maana nimesema "POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU.

  Nitakuwa ni mtu mwenye mashaka sana kama nikiwaza kuwa masilahi duni na maisha ya kuishi chini ya kiwango ni Uzalendo, Sasa Wabunge mkitaka msipigwe mawe barabarani, msitukanwe, msionekane ni wasaliti wa jamii aliyowachagua, Sasa huu ni wakati wakusema, Mshahara wa Polisi, Magereza, JWTZ, Walimu, Makarani Mahakamani na hata sekta zote za Serikali na Binafsi masilahi ya mishahara yao yaongezwe kwa asilimia kama ambavyo mmjiongozea nyie kwenye posho zenu tena zinazohusu siku moja tu lakini wao wanaomba kwa mwezi lakini hawapati. Sasa pamoja na kupinga mfumo mzima wa sera ya posho kama ambavyo Mwenyekiti wetu wa Taifa alisisitiza na kuomba sera hii iangaliwe upya ili kupunguzia Taifa mzigo mkubwa na kuboresha viwango vya mishahara vya watumishi wa UMMA, ni vyema nikarudia kusema kuwa "POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU".

  Ni kweli gharama za Maisha zimepanda lakini hazikupanda kwa Wabunge tu pia kwa Wananchi wote wanaoishi Tanzania , Hivyo tukiacha ubinafsi tukawajibika vizuri Bungeni kulinda masilahi ya Taifa na kutetea maisha ya Wananchi wetu, bila shaka hata tukionekana tunaendesha magari ya kifahari kama Rolls Royce, Bentley, Benz, hakuna mwananchi hatakeyesema kwa nini Mbunge anaendesha gari zuri kwani kila mtu atakuwa na afadhali ya maisha ktk Nchi yetu.

  "Baba yangu aliniambia" Watu wengi wanaokwenda Kanisani na Misikitini huwa wanatoa sadaka ndogo kuliko pesa wanayotumia sehemu mbali mbali za anasa ndio maana Taifa lina Bar nyingi kuliko nyumba za Ibada.

  "TAFAKARI"

  LEMA- MP
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  duu..safi sana mbunge wangu..
   
 3. c

  cheseo Member

  #3
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Mheshimiwa nampa SALUTE,kila kitu kinajieleza wazi
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Kweli Tanzania inahitaji Ukombozi wa fikra tena kwa hati ya dharura
   
 5. Sordo

  Sordo JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tupo pamoja kamanda Lema! Nomba niunganishe na hii cotation yako kwenye waraka kwa wana Arusha siku ulipoamua kwenda gerezani kwa hiari "watakaotubeza na kututukana wasameheni wanahitaji ukombozi wa fikra" Mh.G.Lema
   
 6. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  NGOJA NIKUSAIDIE KUIPANGA VIZURI HII THREADY MUHESHIMIWA MBUNGE!

  Natumaini hapa utakuwa umesomeka vizuri muheshimiwa Lema nakupa Big Up kwa hili!
   
 7. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Lema hapa anajipambanua kama kijana mwenye kuona mambo katika upana wake........

   
 8. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Imekaa njema. Asante sana kwa tafakuri nzuri na imejieleza vyema.
   
 9. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #9
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Nimeikubali hiyo,ingeandikwa pia kwenye magazeti ili kufikia wananchi wengi na waweze kupanua mawazo.
   
 10. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nakuone wivu mkuu' una moja ya wabunge bora kabisa Tanzania!
   
 11. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Safiii mkuuu!
   
 12. L

  Lua JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  naona kamanda! umewafunga mdomo wachawwi wote. tulipa mwenga kaka.
   
 13. fige

  fige JF-Expert Member

  #13
  Nov 29, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakika huo ndio ugomvi wetu,kwamba nyie mnalalamikia laki mbili kwa siku na hamtutetei tunaolipwa laki mbili kwa mwezi.

  Kwa umaskini wetu tunaona nyie ni chinjachinja.Mfumo wa posho umeendelea kuwanufaisha wenye nacho badala ya wanyonge , umezidi kuua morali ya kazi kwa wanyonge na badala ya kuleta tija kazini umeleta uzembe na uhujumu uchumi kwani vikao vimekuwa ndio kazi na kazi zenyewe kutofanyika.

  Tunajua kuna watu wanalipwa vizuri kuliko wabunge,bahati mbaya sana ni wachache wanaoelewa hilo.Ndio maana tunaona nyie wabunge ndio mnaolipwa vizuri kuliko watumishi wote wa serikali.Hakika vita si ukubwa au udogo wa mishahara bali tofauti ya marupurupu na mishahara hiyo katika serikali moja.

  Hivi ,daktari bila nesi kazi itaenda ?Hakimu bila karani au TRA bila ulinzi ?aagh nimechukia sana
   
 14. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #14
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  labda wataiandika kesho kwa kweli imetulia..
   
 15. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #15
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nawashauli CHADEMA Chukueni posho kama Magamba, Lakini Kaeni kama team pangeni kila mbunge achukue posho kiasi gani kwenye posho na kiasi kinancho baki pangieni matumizi mbadala. Mfano Chukueni 100,000 kila mbunge kwa siku na 100,000 mnachanga mnanunua mfano vitanda muhimbili mnavipiga chapa ya chadema, next kikao mnaweza nunua kitu kingine jimbo lingine hivyo hivvo kila jimbo wekeni foot print kwa mtaji wa posho! The Magambas are desperate they cant afford to leave posho !
   
 16. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kweli Mh wewe ni mpambanaji makini
   
 17. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #17
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,396
  Trophy Points: 280
  yafaa hii tumpe sabodo aitoe kwenye kurasa nzima ya daily news na guardian na pia tumpe makinda na pinda.kama wana akili timamu watayatafakari na kuyafanyia kazi
   
 18. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #18
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ngandema, ni mawazo mazuri sana...
   
 19. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #19
  Nov 29, 2011
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  You have a point here! Very good.
   
 20. B

  Bhavick JF-Expert Member

  #20
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Du huyo ndiyo mbunge bwana!natamani ningezaliwa Arusha.mimi mbunge wangu anafanya kazi ya kuzindua albamu ya kumtukana Ruge!
   
Loading...