Posho nyinginyingi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Posho nyinginyingi!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GY, Nov 3, 2009.

 1. GY

  GY JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  wakulu, msaada kidogo,

  1. Ivi yupi hasa wa kuhojiwa, anayetoa posho kwa mtu huku akijua kuwa mtu huyu kashalipwa na mwingine au anayepokea posho huku akijua keshapokea toka kwa mwingine? au wote

  2. Ni yupi hasa wa kudhibitiwa kati ya hao wawili, mtoaji au mpokeaji? au wote

  3. Ikiwa mtoaji wa posho ya ziada hana bajeti kwa ajili ya ya mpokeaji posho nyingi, mpokeaji posho nyingi atatendaje kosa la kupokea posho nyingi

  4. Je kama ni wewe unapewa posho nyingi, utapokea au utakataa?
   
 2. O

  Omseza Mkulu Member

  #2
  Nov 3, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ndg generation-Y.
  Karibu kwenye jamvi !
  Tangu umeingia mwezi huu Nov-09 umeongelea habari za posho kwa wingi kana kwamba zimekugusa /umehusika! .
  Maswali yako unayo majibu mwenyewe sasa sisi tukusaidie kitu gani?
  Swali la mwisho unauliza au unalazimisha watu wapokee hizo posho mara mbili?
  Kwa kifupi rizika na unachopata ambacho ni malipo ya kazi unayotakiwa kufanya!
   
 3. B

  Bumela Senior Member

  #3
  Nov 3, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 148
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mimi kwa mtazamo wangu wakudhibitiwa ni mtoaji posho, kwa sababu ;
  1.kama hakuna bajeti atatoaje?
  2.Na kama asipotoa je atadaiwa na mpokeaji?
  3.na lazima ikumbukwe kwamba ni juzijuzi tu wabunge walikuwa wanapitisha bajet za wizara, wabunge walihoji hizi hela za chai na chakula pamoja na samani mbona ni nyingi sana lakini serkali ilizitetea kwa nguvu zote sasa iweje walaumiwe walaji na wakati hela ipo kwa ajili ya hilo.
  HITIMISHO:Watoaji (serkali) ndio wakulaumiwa , wakudhibitiwa, wakuhojiwa,sio kwa kutoa bali kwa kuziombea bajeti hela mbazo hazihitajiki.
   
 4. GY

  GY JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  umekurupuka mkuu, ndo kwanza nimeuliza masuala ya posho! kuhusu kunigusa ni kweli zimenigusa sana kwani posho hizo zinalipwa kwa kutumia pesa, na pesa hizo zinatoka kwa watu masikini kama mimi kupitia kwenye kodi na vitu kama hivyo

  hata kama maswali haya nina majibu yake, bado wewe pia unauhuru wa ku-share majibu yako na wengine ili tujione kama tunafikiri sawa

  ikiwa suala la posho limekukera, unaweza kulipotezeyaaaaa!
   
 5. GY

  GY JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  fikra hai ni kama hizi. tujiunge kumsaidia ndugu yetu omzela, maana naona fangasi za ungunge zinakaribia kumaliza bongo yake
   
 6. r

  ramson34 Senior Member

  #6
  Nov 3, 2009
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  jamani kwa mimi ninavyooana kama kitu cha bure kama unapewa ni ruhusa kupokea kama yule anayekupa ana uwezo wa kukupa an bajeti inaruhusu maana si dhambi kwa kuwa ana uwezo!!
   
 7. G

  Gashle Senior Member

  #7
  Nov 3, 2009
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 119
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Maoni yangu mimi kila jambo na wakati wake, hatusemi tu ila huu ni mwendelezo wa Taarifa ya Richmond vs posho mbili kwa wabunge. Kama yote yana umuhimu wa kushughulikiwa tungefanya kwa utaratibu. Ilianza Richmond, na ndio iliotia taifa hasara kubwa zaidi, tumalize la Richmond kwanza. Tena kwa marefu na mapana yake kisha ndio tuje kwenye haya mengine.

  Kama anavyosemaga Julius "Miafrika ndivyo tulivyo". Attention yetu inakuwa disttracted na vitu vya kipuuzi kabisa. Report ya Richmond kwanza, mengine baadae.
   
 8. s

  saggy Senior Member

  #8
  Nov 3, 2009
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Habari wana jamii wenzagu.

  Kama wabunge wetu mnataka kumuenzi Baba wa Taifa Mwl. Julius K .Nyerere Kwa VITENDO kataeni kupokea Posho mara mbili na hiyo mliyopokea MRUDISHE kwa wanachi tulio Maskini wa Tanzania tuliowachugua.Kwakuwa Azimio la Arusha lilihusu pia maadili ya Viongozi napenda kuanisha yale yanayohusu maadili ya Viongozi Kutoka katika Azimio la Arusha:

  1.A leader must either be a peasant or a worker and in no way should he/she be associated with the practise of Capitalism or Feudalism

  2.No Leder should hold shares in Company

  3.No Leader should hold directorships in any privatetly owned Company

  4.N o Leader should recive more than one salary

  5.No should own houses which he/she rents


  Kwa maoni yangu mimi mzozo huu umebuniwa KISIASA na wapambe wa JK na Lowa hasaa kwa malengo yafuatayo:


  1.Kudhoofisha sura ya Bunge kwa wananchi,wakati wa mjadala wa Richmond kwakuwa wanachi watakuwa wanahamishia hasira zao kwa Wabunge kwa kupokea Posho mara mbili na hivyo hawawezi kuwaamini na kuunga mkono kile watakachosema kuhusu ufisadi wa Richmonduli wakati wakichangia mjadala huo.

  2.Kudhoofisha Kambi ya Upinzani kwakuwa Malumbano yamemezwa na wabunge wa SISIEM ambao WAMEIBA hoja ya kupambana na UFISADI Kutoka Kambi ya Upinzani na wameihamishia kwao baada ya Kuona mapambano dhidi ya ufisadi yana MVUTO sana kwa wananchi.Wapinzani muwe macho!

  3.Malumbano haya yatawagawa WAPINZANI wa JK ambao wangepata nafasi ya kujipanga kumwondoa madarakani katika uchaguzi ujao mwaka 2010.

  KUBWA ZAIDI:Malumbano haya yaliyopamba Vyombo vya Habari yanafanya wananchi tusahau na kuzungumzia KERO zetu kama

  -MGAO WA UMEME
  -MADAI YA WALIMU WAYODAI SERIKALI
  -MIKOPO INATOLEWA KIMIZENGWE KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
  -HUDUMA BORA ZA MAJI,UMEME NA AFYA
  -MIUNDO MBINU DUNI
  -UCHAFUZI WA MAZINGIRA HUKO MIGODINI
  -UKOSEFU WA MAKAZI BORA
  ETC ,ETC

  MAONI YANGU:Tuzungumzie KERO HIZI JAMANI wenye Vyomb vya Habari!!!
   
Loading...