Posho, kwa madaktari ubinafsi ila kwa wabunge suluhisho kwa ugumu wa maisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Posho, kwa madaktari ubinafsi ila kwa wabunge suluhisho kwa ugumu wa maisha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dr Adam Francis, Jan 31, 2012.

 1. Dr Adam Francis

  Dr Adam Francis Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ikiwa ni siku ya tatu tu tangu mheshimiwa mmoja abaininishe kuwa kile wanacho dai madaktari kina sura ya ubinafsi na kwamlolongo wa hesabu ndefu kuwa hakijazingatia uwezo wa serikali kibajeti leo gazeti la mwananchi limepambwa na habari yenye kichwa RAISI KIKWETE ABARIKI POSHO ZA WABUNGE, ambapo sasa watakuwa wakipata sh 330,000/= kwa siku. Kabla ya kwenda mbali labda tujikumbushe kidogo kuhusu huyu muheshimiwa;
  1. alitetea DOWANS ambayo tumeambiwa ni kampuni ya matapeli walipwe mabilioni bila jasho lolote
  2. alitetea posho za wabunge ambao mishahara na malupulupu yao yanawazidi madaktari kwa mara nyingi tu ziongezwe.
  3. alisema ZANZIBAR sio nchi
  4. alitaka wanaotuhumiwa kuua albino wauwawe
  ndugu zangu huyu bwana mwenye sifa hizo hapo juu alionyesha uhodari mkubwa katika kufanya hesabu za kujumlisha katika kuonyesha kuwa madai ya madaktari kutaka walipwe posho za kufanya kazi kwenye mazingira hatarishi kiafya, posho za kukesha hospitari huku wake zao wakiwa nyumbani wakati unapokuwa zamu, poho ya nyumba, mkopo wa magari na nyongeza ya mshahara ni ya kibinafsi na haytekelezeki. kama hiyo haitoshi alituchimba mkwara kuwa vibarua vyetu vitaota nyasi, sasa ndugu wananchi labda mseme wenyewe kwanini tusimsikilize huyu bwana?
   
 2. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Wewe ni dokta MD, au dokta Ph.D?
   
Loading...