""porojo Za Mkuu Wa Polisi Mwema"" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

""porojo Za Mkuu Wa Polisi Mwema""

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, May 24, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,580
  Likes Received: 5,762
  Trophy Points: 280
  •KATIKA KUONYESHA KUMFWATA MKUU WA KAZI JK .....UKIARIBU KAZINI SOLN NI KUAMISHWA TUCHEKE PAMOJA ::
  Mabadiliko makubwa Polisi, Tibaigana ang'atuka  JESHI la Polisi limefanya mabadiliko makubwa katika safu yake ya uongozi kuanzia ngazi ya wilaya, mikoa na wakuu wa upelelezi kufuatia maofisa wake wengi kufikisha umri wa kustaafu kwa lazima ifikapo Julai 1, mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Said Mwema, Kamishna wa Utawala na Fedha, Bw. Clodwig Mtweve, alisema Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Alfred Tibaigana anastaafu na nafasi yake inachukuliwa na Bw. Suleiman Kova, aliyekuwa Mbeya.

  Atakayeziba nafasi ya Bw. Kova ni Kamanda wa Mkoa wa Bw.Stephen Zelote ambaye nafasi yake inachukuliwa na Bw. Jamal Rwambow, akitokea Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni.

  Alisema Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Bw. David Saibullu anastaafu na nafasi yake inachukuliwa na Bw. Liberatus Lyimo Barlow, ambaye kabla ya uteuzi huo, alikuwa Ofisa Nadhimu Utawala na Fedha Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

  Aliyeteuliwa kushika nafasi ya Bw. Rwambow Mkoa wa Kinondoni ni Bw. Mark Kalunguyeye, ambaye kabla ya uteuzi wake alikuwa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Bw. Ray Karama, aliyekuwa Kikosi cha Kutuza Ghasia, Dar es Salaam ameteuliwa kuwa Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Wezi wa Mifugo Makao Makuu Arusha.

  Bw. Mtweve alisema, Bw. Abdallah Msika amehamishwa kutoka mkoani Kagera na kupelekwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam huku ASP Salewi aliyekuwa Kamanda Mkoa wa Pwani akipelekwa kuziba nafasi yake.

  Mabadiliko hayo pia yamemgusa Bw. Mwakyoma aliyekuwa Makao Makuu ya Polisi na sasa anaenda kuwa RPC Mkoa wa Pwani huku RPC wa Tabora, Bw. Mshahili akirejeshwa makao makuu Dar es Salaam na nafasi yake kuzibwa na Bw. Emson Mmari, aliyekuwa Makao Makuu ya Upelelezi.

  Bw. Lucas Kusima aliyekuwa Baraza la Ulinzi na Usalama, amehamishiwa Makao Makuu na nafasi yake itazibwa na Bw. Brown Lakey kutoka Makao Makuu ya Upelelezi.

  Katika mabadiliko hayo pia yamewagusa wanawake wawili ambapo Bi. Marry Nzuki aliyekuwa OCD Mkoa wa Dodoma anakwenda kuwa Kaimu Kamanda wa Polisi TAZARA huku SSP Lucy Makelemo aliyekuwa OCS Uwanja wa Ndege Mwanza anakuwa Staff Officer I Dar es Salaam.

  Alisema mabadiliko hayo pia yamewagusa wakuu wa upelelezi wa mikoa Mara, Kigoma, Shinyanga na Mbeya. Wanaotarajia kustaafu nafasi zao zimechukuliwa na Bw. Msato Marijani aliyekuwa OCD Wilaya ya Biharamulo (Kigoma), Bw. Deusdit Kato (Mara). Kabla ya hapo alikuwa OCD Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam.

  MSIKA SIJUI MARA YA NGAPI HII !!!!1
   
Loading...