Porojo za Kapuya

Tanzania 1

Senior Member
Oct 4, 2007
197
24
Kapuya aliwapiga chini vijana wengi wa JKT miaka michache iliyopita, alipokuwa waziri wa ulinzi. Isitoshe, alitoa ahadi bungeni kuwa angewapa ajira vijana hao. Sasa anakuja na porojo lingine!!:

Serikali kumwaga ajira milioni tano

2008-07-22 10:55:44
Na Mashaka Mgeta, Dodoma

Serikali inakusudia kutengeneza ajira mpya milioni tano, zikiwa ni zaidi ya zilizoahidiwa na Rais Jakaya Kikwete, wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

Akiwa kwenye kampeni hizo, alipogombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Kikwete, aliahidi kuwa serikali yake itatoa kipaumbele katika maeneo mbalimbali, ikiwemo kutengeneza ajira mpya milioni moja.

Hata hivyo, akijibu hoja za Wabunge waliochangia hotuba ya bajeti ya wizara yake, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, alisema serikali inakusudia kufikia ajira milioni tano, kutokana na mkakati uliaondaliwa kuhusu ukuzaji wa ajira nchini.

Alisema mkakati huo uliandaliwa kwa ushirikiano wa serikali, Shirika la Kazi Ulimwenguni (ILO) na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Alisema mkakati huo unatoa fursa zaidi kwa watu wa kada na makundi mbalimbali, wakiwemo wenye ulemavu.

Aidha, Profesa Kapuya, alisema hivi sasa serikali inawasiliana na wadau kama taasisi zisizokuwa za kiserikali na mashirika mbalimbali, ili kupata takwimu halisi ya ajira mpya zinazotengenezwa nchini.

Alisema hadi kufikia sasa, takwimu zinaonyesha kuwepo ajira mpya 437,035, ambazo zinatarajiwa kuongezeka kupitia jitihada mbalimbali zinazofanywa na kutoa mfano wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA).

Profesa Kapuya, alisema fasihi ya elimu ya Ukimwi mahali pa kazi, ipo katika hatua ya uchapishwaji na itakapokamilika, itasambaza kwa ajili ya matumizi yake.

Aidha, alisema serikali inatambua kuwa viwango vinavyolipwa kutokana na madhara yanayotokea sehemu ya kazi, havilingani na athari zinazowakabili walengwa.

Alisema kutokana na hali hiyo, serikali inapitia sheria hiyo kwa ajili ya kuandaa mswada wa mabadiliko yake, utakaowasilishwa bungeni katika mkutano ujao mjini hapa.

Pia, Profesa Kapuya, alisema wizara yake inaendelea na mpango wa kukagua vibali vilivyoombwa na wageni kwa ajili ya kufanya kazi nchini, ili kubaini ikiwa vinakiuka taratibu zilizopo.

Alisema kwa mujibu wa taratibu hizo, kazi zinazopaswa kufanywa na wageni, hazitakiwi kuwa katika kiwango kinachoweza kufanywa na wazawa.

Wakati huo huo, Profesa Kapuya, alisema imebainika haja ya kuongeza wigo wa ushiriki wa vijana, kushiriki katika uundwaji wa baraza la vijana la Taifa.

Profesa Kapuya, alisema mchakato huo ulianza, ulisababisha kufanyika kwa mikutano miwili, ambapo iligundulika kuwepo haja ya kuwashirikisha vijana wengi zaidi, hasa kutoka maeneo ya vijijini.

Alisema mchakato wa sheria unaokidhi mkakati wa kuundwa kwa baraza hilo, utawasilishwa kwenye kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, mara utakapokamilika.
SOURCE: NIPASHE
 
Tusimshangae kazi ya wanasiasa ni kusema uongo, anamuiga boss wake aliyehaidi maisha bora kwa kila aamtanzania ambayo sasa yamekuwa ni ndoto za mchana
 
vile vile usisahau kuwa Bajeti ya wizara anayoongoza huyu bwan Kapuya imepitishwa in record time ya 15 minutes! This has NEVER happend in the history of this parliament.

mengine naona ni nyongeza tuuu
 
aaah Kapuya hakuna kitu mle anataka kuwaajili kwenye migodi yake sasa sijui kama watatosha hao 5ml.
 
avatar10550_69.gif
avatar10550_69.gif
avatar10550_69.gif
avatar10550_69.gif
avatar10550_69.gif
avatar10550_69.gif
avatar10550_69.gif
avatar10550_69.gif
avatar10550_69.gif
avatar10550_69.gif
avatar10550_69.gif
avatar10550_69.gif


Acha wafu wazikane!!
 
Back
Top Bottom