TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 13,744
- 21,192
Rais Magufuli alipopita Masanza aliwaeleza waziwazi wapiga kura kuwa hawatishi isipokuwa kama watafanya makosa ya kutomchagulia viongozi wa CCM watajuta! Tena akasisitiza kwa kisukuma kuwa, “haiwezekani chakula ulichokitunza kwa ajili ya mwanao ukakigawa kwa mtoto wa jirani. Sasa nichagulieni wale wa jirani ili mpate fundisho!”.
Nina jamaa zangu wanaoishi Masanza na nisingependa “wajute”. Najua wao ni wanachama wazuri wa CCM na wamenihakikishia kuwa watawachagua wagombea wote wa CCM, lakini itakuwaje kama kura zao hazitatosha?
Ningepata mwanya wa kukutana na Rais faragha ningemuuliza swali ambalo Ibrahim aliwauliza wajumbe wa Mungu baada ya kupata habari kuwa Sodoma walikokuwa wakiishi ndugu zake ilikuwa inakwenda kujuta!
Kama Ibrahim ningemuuliza, “Je, kweli watu wema watajuta pamoja na waovu?" Huenda ikawa mna watu wema hamsini humo jimboni watakaochagua wagombea wote wa CCM. Je, jimbo zima litajuta badala ya kuliacha kwa sababu ya hao wema hamsini waliomo humo?
Na James Gayo.