Uchaguzi 2020 POROJO ILA KWELI: Swali la Ibrahim kwa Rais Magufuli

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
6,887
2,000
Rais Magufuli alipopita Masanza aliwaeleza waziwazi wapiga kura kuwa hawatishi isipokuwa kama watafanya makosa ya kutomchagulia viongozi wa CCM watajuta! Tena akasisitiza kwa kisukuma kuwa,haiwezekani chakula ulichokitunza kwa ajili ya mwanao ukakigawa kwa mtoto wa jirani. Sasa nichagulieni wale wa jirani ili mpate fundisho!”.

Nina jamaa zangu wanaoishi Masanza na nisingependawajute”. Najua wao ni wanachama wazuri wa CCM na wamenihakikishia kuwa watawachagua wagombea wote wa CCM, lakini itakuwaje kama kura zao hazitatosha?

Ningepata mwanya wa kukutana na Rais faragha ningemuuliza swali ambalo Ibrahim aliwauliza wajumbe wa Mungu baada ya kupata habari kuwa Sodoma walikokuwa wakiishi ndugu zake ilikuwa inakwenda kujuta!

Kama Ibrahim ningemuuliza,Je, kweli watu wema watajuta pamoja na waovu?" Huenda ikawa mna watu wema hamsini humo jimboni watakaochagua wagombea wote wa CCM. Je, jimbo zima litajuta badala ya kuliacha kwa sababu ya hao wema hamsini waliomo humo?

Na James Gayo.
 

Pyepyepye

JF-Expert Member
Jan 6, 2017
1,940
2,000
Hao wema tutawapeleka mwamanyili, kisha waliobaki tutawazuia wasitumie bararbara tulioijenga sisi kwa safari zozote, vinginevyo watumie nyungo.

Nimeongea kama polepole
 

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
8,714
2,000
James Gayo

angeweka na katuni ya KINGO

1450796_6041248_orig.jpg
 

KISIWAGA

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,556
2,000
Sasa kwani lazima watu waishi huko masanza

Kama serikali ikiwatenga masanza si mnahamia hata chato kwani mtaombwa viza
 

Ryaro wa Ryaro1233

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
322
1,000
Lakini Mara Kadhaa Mkuu amekua akisikika Kuwa " Maendeleo Hayana Chama".. sijui Maana yake ni nini?. Changanya Changanya Hata Wafia Chama kwa sasa Hawaelewi kipi Wakiamini.. Daah!!! Lissu Wapumzishe baba...
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
6,887
2,000
Lakini Mara Kadhaa Mkuu amekua akisikika Kuwa " Maendeleo Hayana Chama".. sijui Maana yake ni nini?. Changanya Changanya Hata Wafia Chama kwa sasa Hawaelewi kipi Wakiamini.. Daah!!! Lissu Wapumzishe baba...
Hao wafia chama wenyewe wanajipanga kumkata, soon kila kitu kitakuwa wazi. Tatizo kila mtu ana hofu ya maisha hata waliokuwa wababe wamenywea.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom