POPOBAWA ATUA Tena Bongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

POPOBAWA ATUA Tena Bongo

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Mwiba, May 15, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kuna tetesi kuwa yule Mdudu wa Kipemba ametua kwa mara nyengine katika mitaa ya Bongo ,mwandishi wetu aliekuwa akipita mitaa iliyoathiriwa na kiumbe huyo wa ajabu alikutana na watu tofauti ambao walikuwa na maelezo yanayosababisha athari za mdudu huyo aliyewahi kukatiza mitaa ya bongo kati ya mwaka 2005 na kutesa.
  John Kilomwe wa mtaa wa Keko Magurumbasi alisema mwenzao mmoja alieathiriwa na mdudu huyo ilibidi atoe yaliyomkuta baada ya kurudiwa mara tatu na kufanyiwa kitendo cha aibu ,akizidi kusema sababu zilizomfanya ni kukataa kutoa aibu hiyo kwa marafiki zake na kuwaeleza majirani kitendo ambacho alieleza ni lazima baada ya kuhujumiwa upite kwenye mitaa ukiwaeleza watu jambo ambalo alisema hakuweza kulifanya kwa siku za mwanzo na alivyoona dudu hilo halichoki akaona ni bora awaeleze watu na hapo halikumrudia tena.

  Na wakazi wa mtaa wa morogoro road wameanza kulala nje huku wakikoka moto ,dawa ambayo walielezwa kuwa inalifanya dudu hilo kuwa na mazingira magumu ya kuvamia mawindo yake ,hadi sasa hakujaelezwa ni kwa sababu gani dudu hilo limehamia katika mitaa ya bongo.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Sijuwi wamekerwa nini jamaa zangu mpaka wameanza tena kutembeza bakora.Huyu mdudu bora angelielekeza hujuma zake kwa mafisadi na kuwalazimisha waungame na warejeshe hela za wananchi, la si hivyo awe anawarudia mara kwa mara. Ingekuwa safi kweli kweli
   
 3. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  hawa ni wajinga wanapaswa kutembelea watu walioiba kuanzia billion moja na kuendelea. au mnasemaje wanajf
   
 4. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  acheni uchuro wenu......mwiba jamaa yako ndio wale wakina mark mosha hakua cha popo bawa..
   
 5. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #5
  May 16, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hivi huyu popobawa haogopi ukimwi?Au haumhusu yeye?Au pengine anaueneza?Just thinking aloud.....
   
Loading...