POPE: Twende Galilaya

Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,989
1,441
Heri ya pasaka wana wa jamvi.

Jana wakati wa misa ya vigilia ya ufufuko wa bwana, Papa anatukumbusha kupitia injili inayomzunguzia mwanamke aliyekwenda kumpa yesu mafuta kama ilivyo desturi ya wayaudi lakini anakuta mlango wa kaburi imeviringishwa. Yesu anapowatokea wanafunzi wake baada ya ufufuko anawaambia waende galilaya.

Papa anasema, katika hali waliyokuwa nayo wale wanawake juu ya siku zijazo bila masiha ziwapa hofu na mashaka ni kwa namna wataishi, papa anafananisha hali hiyo na ya sasa kwa ulimwengu tulionao, tukiwa tumegubikwa na hofu pia mashaka ya maradhi ya Corona ya 2019! Hatujui kesho itakuwaje wala tutashindaje vita hii!

Lakini papa anatukumbusha kuwa, Twende Galilaya kama Yesu alivyowaambia wanafunzi na wafuasi wake.

Kwa nini Galilaya?
Galilaya ni mji mtakatifu, pia ndiko mitume walikoitwa na Mungu (Yesu alipochagua mitume 12)
Ni mji wa kumbukumbu kwa kifupi.
Ni mji unatukumbusha kuwa ndipo tulipopendwa, kuitwa na kualikwa na Mungu kumfuata, kutimiza mapenzi yake na kutkatifuza ulimwengu.
Ni mji ambao yesu aliwaaga na kupaa mbinguni.
Ni mji ambao yesu aliwapa mamlala dhidi ya ulimwengu.

Kwenda Galilaya?
Papa anafafanua maelezo ya yesu pamoja na Hofu yao kuwa ni mwito kwetu nasi sasa kama wao kuwa.

Tuwe na Matumaini pamoja na Nguvu ya kuhimili hofu na mashaka (gifts of Hope and Courage)

Matumaini ni haki yetu tunayojaliwa na Mungu hivyo tuendelee kumuomba.

Courage pia ni Zawadi ya Mungu inayotupa nguvu tushinde hofu na mashaka katika kipindi hiki cha Corona.

Mwito wa yesu anaouleza papa kuwa twende Galilaya unatutaka "TO BRING THE SONG OF LIFE" anasema kama si sisi tunaopaswa kuimba wimbo huo ni nani ataimba?

Twende Galilaya ambao ni mji wa kumbukumbu ambao hupo katika maeneo yote hasa mioyoni mwetu kwa kutumia hizo zawadi mbili za kimungu ndivyo KU BRING THE SONG OF LIFE kwa kila mmoja. Galilaya anakosema Yesu twende yeye Tayari ametangulia mbele hivyo tutamkuta.

Daima yesu amekuwa akitangulia mbele katika maisha yetu: ametangulia siku zote kwenye maisha yetu, ametangulia pia kwenye vifo vyetu hivyo, Tumtumainie na kuwa naye Daima.

TWENDE GALILAYA NAYE TUTAMKUTA HUKO

Source: vaticannews
 
Nashindwa kuelewa hao wanawake walioenda kupaka maiti mafuta siku ya tatu ,maiti za kiyahudi haziozi zikizikwa? Maiti iliyozikwa siku tatu nyuma unaipakaje mafuta? Haitoi harufu?

Huo utaratibubupo mpaka leo mtu anazikwa halafu baada ya siku kadhaa wanaenda kutoa maiti kupaka mafuta halafu wanazika tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashindwa kuelewa hao wanawake walioenda kupaka maiti mafuta siku ya tatu ,maiti za kiyahudi haziozi zikizikwa? Maiti iliyozikwa siku tatu nyuma unaipakaje mafuta? Haitoi harufu? Huo utaratibubupo mpaka leo mtu anazikwa halafu baada ya siku kadhaa wanaenda kutoa maiti kupaka mafuta halafu wanazika tena

Sent using Jamii Forums mobile app
Uelewa wa kawaida unahitajika, usitumie hisia au harufu..

Namna ya kuzika pia inahusika

Kwa kuwa ni tamaduni za zamani zinaweza kuwa zilishaachwa au laa!
 
Nashindwa kuelewa hao wanawake walioenda kupaka maiti mafuta siku ya tatu ,maiti za kiyahudi haziozi zikizikwa? Maiti iliyozikwa siku tatu nyuma unaipakaje mafuta? Haitoi harufu? Huo utaratibubupo mpaka leo mtu anazikwa halafu baada ya siku kadhaa wanaenda kutoa maiti kupaka mafuta halafu wanazika tena

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama vile akili zako ni za kushikiwa, kwa maelezo na uelewa wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Twendeni Galilaya tuondoe hofu na tujae amani ya bwana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom