Pope Francis abusu miguu ya viongozi wa Sudan Kusini Salva Kiir na Riek Machar, akiomba wasitishe vita

Of coz lkn naona kama vle kajishusha sana kupitiliza. Sijawah kuona kitendo hicho akiwa anawaomba maraisi wengne watunze amani
Angekuwa anafanya hivyo mara kwa mara isingekuwa ni jambo special. Ugomvi unaondelea Sudan ya kusini ni ubinafsi wa viongozi ndiyo maana anajaribu kutumia njii hii kwani nchi yenyewe ni maskini sana na wanaoangamia ni wananchi.
 
Huyo ni mtumishi wa Mungu, hao wengine ni miungu watu wanaotaka kuwa wa kwanza na kutukuzwa badala ya kuwa wa mwisho kama kama mafundisho ya injili yanavyowataka. Huyo Pengo ni kada mtiifu wa CCM ila siku zake madarakani zinahesabika
Kubusu tu miguu ya watu haitoi uwezekano wa kuwa mtumishi wa Mungu. Hata wale wasiokuwa wa huyo Mungu (wasiokuwa na dini ) wanafanya hata mitaani huku tunaowaona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Papa ni rais wa dunia.Anawajibu wa upatanishi popote pale anapoona mambo yanaenda kombo.





Ungetuwekea na kapicha ka kusindikizia hili bandiko lako ungetisha sana maana si wote tulioshuhudia hilo tukio. Na hata kama amewabusu hiyo miguu yao, bado haiwezi kuondoa ile dhana ya watu weupe kujiona wao ni bora na hivyo kuendelea kuwabagua na kuwanyanyapaa watu weusi kwa sababu zao za kipuuzi.
radiomariatanzania-20190413-0001.jpeg
radiomariatanzania-20190413-0002.jpeg
radiomariatanzania-20190413-0003.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila alhamisi kuu viongozi wa katoliki uwaosha miguu waumini wao
Na ukienda pale mburahati ktk kituo cha malezi utayaona hayo pia
Hahahaa....... Ile ni ibada mkuu ya ukumbusho wa Yesu alivyowaosha miguu wale thenashara.

Lete mfano kama wa Papa!
 
Najiuliza tu unyenyekevu ule ulioonyeshwa na kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kuwabusu miguu mahasimu wawili na wababe wa vita Rais Salva Kiir na Machar umetufunza nini sisi watanzania.

Sipati picha tukio hilo lingefanywa na viongozi wetu hapa Tanzania hawa akina Kardinali Pengo, Kakobe, Gwajima au alhad Salum!

Niendelee kuwatakia kwaresma yenye baraka!
I don't think kama hao waliosababisha vifo vya mamia ya wasudani wana deserve hiyo treatment wao wangepswa kwenda kubusu miguu ya ndugu wa watu waliokufa n.a. kupotea huko Sudan wawaombe msamaha!!
 
Ajabu kweli hajasoma kwenye bible kuwa siku za mwisho kutakuwapo na vita??? Huo ni unabii lazima utimie hata kama angewabeba kichwani kile kilichotabiriwa lazima kitimie-mathayo 24:6,7

Sent using Jamii Forums mobile app
Vita imeanza zaidi ya miaka 1000 iliyopita, sijui hao watu wa zamani wangekuwa na mawazo ya "maandiko yanasema" nyakati za mwisho.. Hitler, mwl nyerere, mkwawa walizaliwa na kuikuta Vita. Wamekufa na wameiacha vita

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna unyenyekevu hapo, kanisa linapoteza mvuto na kesi nyingi za unyanyasaji wa kingono. Hawa jamaa wana mbinu nyingi sana, baada ya kuona hii picha unafikiri kuna jamii ya kichaga itamuamini mtoto atakae sema amefirw.a na padre? " kanisa ni jema na halibagui watu, ndomana hata papa amebusu miguu ya watu weusi "
 
Hapa inaonyesha kuwa hawa viongozi wa Sudan Kusini wamekosa adabu kabisa! Walichotakiwa kufanya ni kuinuka na kumzuia Papa kubusu viatu vyao na kupiga magoti mbele yake na kumwomba radhi!!!!
 
Nilimsikia jana Steve Bannon akiwaka kuwa Vatican ibadilike lakini sikuelewa, kumbe!
 
Ni msanii kama wasanii wengine.
%88 ya Wakatoliki niwateja wa Jehanum kutokana na kuishi kwa amri za kanisa badala ya kuishi kwa neno la Mungu. Si ajabu pale kuna maslahi ya Vatican.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amefanya vizuri sana kwani inauma sana kuona binadamu tumewazidi hata simba kwa kuuwa
Wao walipatana wakapeana majukumu halafu wakatibuana hata hawajafika popote
SS ni njaa sana huko ila wana mafuta yanayowawezesha kuishi maisha mazuri sana wakisaidiana na upande mwingine
Ila Mwafrika popote alipo ni afadhali mnyama kwani akili zero hata mwenye PhD
Kuna wengine wanatakiwa awabusu WASIIBE

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Back
Top Bottom