Poorest road design ever

mamanalia

JF-Expert Member
Nov 7, 2009
666
146
Nadiriki kusema katika design za barabara nilizowahi kuona, barabara za BRT ndo poorest design ever.

Kweli barabara inawekewa ukuta na bila hata kujali wakazi wa pembeni watahitaji kuvuka au kuingia high way na magari yao!!!!!!!!!!!!! Ni bora hata wangeweka ukuta kwenye barabara zitazotumiwa na mabasi na kutoweka miukuta kwenye public roads.

Eti hawa nao wanajiita wahandisi!!!!!
 
Ni kawaida sana kuweka UKUTA na kama wasingeliweka, mlikuwa na HAKI ya kuandamana na kudai waweke.

Yakianza kwenda magari kwa mwendo kasi, ndiyo utajua maana ya hizo kuta. Ila mnaweza kuomba wawawekee za Plastic ili muweze kuona magari YETU MAFISADI yakipita barabarani.....

2004_silent_r4_c2.img_assist_custom.jpg

Design yote umeiona?unaweza ukawa unazungumza kitu usichokijua engineers sio wajinga kama unavyofikili.
 
kibaya mkuu sikonge ni kutoacha sehemu za kuingia high way, mfano ubungo hadi kimara ni kero kubwa kwani sehemu karibu zote zimezibwa na zitazibwa. Na kinachouma zaidi ni kuona serikali haitengezi barabara mpya inang'oa lami na kuweka ingine kwenye the same roads!!!

tunahitaji flyovers na ring roads na sio utoto kama huu wa brt.
 
Design yote umeiona?unaweza ukawa unazungumza kitu usichokijua engineers sio wajinga kama unavyofikili.

Tuwekee picha za design basi angalau tujue huo mradi ukiisha utakuwaje. Wameweka pale kimara mwisho picha ya daraja la waenda kwa miguu kwanini wasiweke mfano pale ubungo picha ya itavokuwa kwenye hayo maungio. Wametoa taa ubungo na kila mtu anajiuliza itakuwaje hapo.
Huu ni mradi wa umma watuwekee 3D drawings kutuonyesha mradi utapokamilika utakuwaje.
Kama wewe unazo hizo picha ziweke hapa jf tuzijadili.
 
Mimi najiuliza hilo gari kasi ikipungua au kuharibika mengine yatapita wapi au litapark wapi kubadilisha tyre.sipati picha. Foleni ya magari ya kasi itakavyokua moja likiharibika sababu barabara ina size ya gari moja.
 
Design is the improvement of existing.huo unaitwa mradi na kila mradi una hatua zake kwa kiingereza wanaita phase,ndio kwanza wapo hatua ya kwanza.usiwe na wasiwasi yote unayoyasema yamezingatiwa ipasavyo,
unaposema poor design unafananisha na kitu gani mkuu?
 
Cwez kuwakosoa Strabag coz project bado inaendelea. BTW hawa jamaa katika macontractor bora duniani wapo kwenye top ten.
 
Wabongo kujifanya wajuaji mradi hujaisha unajifanya kuleta ujuaji why usingejenga wewe unafikiri kua Hawa wa Austria kujenga BRT WALIPEWA KAMA MNAVYOPEANA NAMBA ZA SIM NA MADEM CLUB....[/ Hawa wa Austria ]

Mkuu; Rekebisha maneno haya kwani Austria haihusika najua mkandarasi ni Mjerumani na Mhandisi Mwelekezi (Supervising Engineer)anatoka Australia.

Jamaa anetoa wasiwasiwake ni haki yake
 
Mimi najiuliza hilo gari kasi ikipungua au kuharibika mengine yatapita wapi au litapark wapi kubadilisha tyre.sipati picha. Foleni ya magari ya kasi itakavyokua moja likiharibika sababu barabara ina size ya gari moja.

Sina hakika ila nadhani kwa kuwa ni njia moja watatumia utaratibu kama kwenye uendeshaji wa treni.

Kwa treni utaratibu uko hivi:-
- Kama likitokea tatizo dogo linarekebishwa na dereva au mafundi hapo hapo lilipotokea.
- Kama ni tatizo kubwa kutegemea kituo cha karibu kilipo inavutwa au kusukumwa na mwenzake hadi kituoni.

Ni vizuri lakini kuwa na utaratibu mzuri wa "preventive maintenance" kuepuka kuharibika mara kwa mara.
 
Nadiriki kusema katika design za barabara nilizowahi kuona, barabara za BRT ndo poorest design ever.

Kweli barabara inawekewa ukuta na bila hata kujali wakazi wa pembeni watahitaji kuvuka au kuingia high way na magari yao!!!!!!!!!!!!! Ni bora hata wangeweka ukuta kwenye barabara zitazotumiwa na mabasi na kutoweka miukuta kwenye public roads.

Eti hawa nao wanajiita wahandisi!!!!!

Acha presha tuliza moyo wako barabara bado haijaisha. au njoo BRT uone itakavyo kua ikiisha. kumbuka ime designiwa na expatriate sio mtz. najua watz hamwakubali kabisa
 
Kwa bahati nzuri nimesomea kidogo HIGHWay design..... ndiyo ubaya na uzuri wa Highway na hiyo wala siyo Highway kwa kweli kwani Highway zina masharti magumu sana na ni mbaya mno kwa wenyeji wa pembeni mwake ila walau wanakuwa salama na ajali za kugongwa kila siku. Highway zinakuwa chini na barabara zote nyingine zinakuwa juu yake. Ila kunaweza kutokea Special cases. Kwenye highway, barabara hazikatani, hakuna taa za barabarani (Usalama) nk. Zinajengwa ili ukiingia kwenye highway, basi husimami hadi unafika kwenye sehemu unayokwenda - no collision. Kwa sababu hiyo, inapunguza sana foleni ingawa ikitokea ajali, hasa kama kuna ukungu, basi gari kama 100 zinakwenda na maji. Kuna wakati jamaa alifunga barabara na truck na akaokoa watu wenhi sana.

Flyover(konokono) na Rings ni kitu hichohicho tu na itaishia kuwa na Highway na utarudi palepale. Rings haziwezi kuwa kama barabara za mitaani kwa kila mtu kujiingilia na kutoka, inakosa maana ya ring.
Kuishi MJINI kuna matatizo yake na maendeleo pia yana gharama zake Mkuu.....

kibaya mkuu sikonge ni kutoacha sehemu za kuingia high way, mfano ubungo hadi kimara ni kero kubwa kwani sehemu karibu zote zimezibwa na zitazibwa. Na kinachouma zaidi ni kuona serikali haitengezi barabara mpya inang'oa lami na kuweka ingine kwenye the same roads!!!

tunahitaji flyovers na ring roads na sio utoto kama huu wa brt.
 
Tatizo Watanzania tunakurupuka tu kulalamika..

Tembea uione Dunia ndio ujue barabara zinajengwa vipi..

Huu ndio mfumo wa bara bara ulivyo lazima kuwekwe ukuta kuzuia magari kuingia Highway ovyo ovyo..

Nchi nyingi sio tu kuingia na gari bali hata ukitaka kuvuka barabara hadi uende sehemu ya kuvukia maana bara bara nzima imezibwa,,

STRABAG sio kampuni magumashi kama unavofikiria..

Tena kuonesha walivyo serious kwenye kazi zao wamekuja na SMEC kama consultant wao..

Hapo hata magufuli hatii mguu, anawaogopa kama ukoma.. Anaonea kampuni za janja janja tu kuwapiga mikwara but akigusa STRABAG tu World Bank wanamfunga

Hizo kampuni ni kubwa sana na sana na sana kwenye mambo ya ujenzi unaweza uka google kwa ajili ya details zao na kazi walizowahi kufanya duniani
 
Mimi najiuliza hilo gari kasi ikipungua au kuharibika mengine yatapita wapi au litapark wapi kubadilisha tyre.sipati picha. Foleni ya magari ya kasi itakavyokua moja likiharibika sababu barabara ina size ya gari moja.

Wewe kweli mgeni. Nani kakwambia hayo magari yataharibikia njiani ? mmeanza kuuchulia mradi. ushindwe na ulegee
 
Ni kawaida sana kuweka UKUTA na kama wasingeliweka, mlikuwa na HAKI ya kuandamana na kudai waweke.

Yakianza kwenda magari kwa mwendo kasi, ndiyo utajua maana ya hizo kuta. Ila mnaweza kuomba wawawekee za Plastic ili muweze kuona magari YETU MAFISADI yakipita barabarani.....

2004_silent_r4_c2.img_assist_custom.jpg

Unajua mkuu shida yetu Waswahili hatutaki utaratibu. Tuataka kufanya mambo kienyeji enyeji tu!

Kwenye barabara tunataka kukatisha kila mahali, na ndiyo maana ajali ni nyingi sana.

Chukulia kama pale Manzese. Kuna daraja la kuvusha watembea kwa miguu lakini watu hawalitumii bali wanavuka tu kienyeji kila mahali!
 
Nadiriki kusema katika design za barabara nilizowahi kuona, barabara za BRT ndo poorest design ever.

Kweli barabara inawekewa ukuta na bila hata kujali wakazi wa pembeni watahitaji kuvuka au kuingia high way na magari yao!!!!!!!!!!!!! Ni bora hata wangeweka ukuta kwenye barabara zitazotumiwa na mabasi na kutoweka miukuta kwenye public roads.

Eti hawa nao wanajiita wahandisi!!!!!

Eti barabara nilizowahi kuona, wapi? Umeshasema highway, au hujui maana ya highway? Highway sio barabara za kuvukavuka ovyo. Mnataka maendeleo halafu mnapiga kelele...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom