Poor Tanzania, tunahangaika na mchanga wa kilo 3

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,272
47,268
Hivi sisi ni wa kukimbizana na kontena la mchanga wenye kilo 3 za dhahabu? tena kwa mrahaba wa 4% kweli?

Haiingii akilini rais anaacha kushughulikia dhahabu iliyo tayari (parked) migodini anaunda tume kwa mabilioni ya shilingi kuchunguza kilo 3 kwenye kontena kweli?

Nani katuroga Watanzania, inauma sana.

FB_IMG_1496418987764.jpg
 
Tushazoea kula mapanki bana hiyo minofu hatuna utamaduni nayo... Haujawahi sikia wanasema maneno haya,,, utamu wa samaki ni kichwa na utamu wa nyama mfupa.... Sasa kwa akili ya haraka haraka unaacha mnofu wa nyama unakimbilia mfupa kweli?
 
Wale wa kanda ya ziwa watakuelewa
 
Tushazoea kula mapanki bana hiyo minofu hatuna utamaduni nayo... Haujawahi sikia wanasema maneno haya,,, utamu wa samaki ni kichwa na utamu wa nyama mfupa.... Sasa kwa akili ya haraka haraka unaacha mnofu wa nyama unakimbilia mfupa kweli?
Yaani we acha tu sasa kila mtu na acacia lakini ukiangalia kwa makini hata tukipewa makontena yote waliyozuia haifiki hata 1/10000 ya dhahabu tuliyoibiwa tangu 1997.
 
Yaani we acha tu sasa kila mtu na acacia lakini ukiangalia kwa makini hata tukipewa makontena yote waliyozuia haifiki hata 1/10000 ya dhahabu tuliyoibiwa tangu 1997.
Ata hao accacia watatupima wakiona tumezubaa watatuzubaisha hapo hapo kwenye mchanga kwa kujifanya kufanya mazungumzo ili tusibumburuke juu ya dhahabu za mgodini.. Yaani dah sijui ata mtu usemeje ili watu waelewe lakini ndio hivyo watu hutofautiana ktk mengi
 
Hivi sisi ni wa kukimbizana na kontena la mchanga wenye kilo 3 za dhahabu? tena kwa mrahaba wa 4% kweli?

Haiingii akilini rais anaacha kushughulikia dhahabu iliyo tayari (parked) migodini anaunda tume kwa mabilioni ya shilingi kuchunguza kilo 3 kwenye kontena kweli?

Nani katuroga Watanzania, inauma sana.

View attachment 518532
Swali la msingi ni kama kweli kuna Kg 3. Serikali imelitilia hilo shaka na imeamua kuchunguza. Matokeo tunaambiwa ni mara 10 zaidi. Msema kweli ni nani? Na tutajuaje? Pili hizo njia nyingine za upotevu nazo zinastahili kuchunguzwa na kudhibitiwa. Wote serikali na wapinzani wake kwa ujumla wanakubali kwamba tunapigwa malumbano yako kwenye mikakati ya kututoa hapo. Kwa uelewa wangu mdogo mpaka reporti ya pili itoke ndiyo tutajua serikali imeshauriwa ichukue hatua gani. Hilo lakini halizuii serikali kupewa tahadhari (kwa kuombwa au kukemewa), na serikali sikivu inatakiwa isikilize na iamue. Mwisho wa siku kupitia serikali watanzania watabeba msalaba wao (iwe zigo au uokovu).
 
Hivi sisi ni wa kukimbizana na kontena la mchanga wenye kilo 3 za dhahabu? tena kwa mrahaba wa 4% kweli?

Haiingii akilini rais anaacha kushughulikia dhahabu iliyo tayari (parked) migodini anaunda tume kwa mabilioni ya shilingi kuchunguza kilo 3 kwenye kontena kweli?

Nani katuroga Watanzania, inauma sana.

View attachment 518532
Hata ungekuwa nusu kilo ni Mali yetu .Nilazima tuupiganie.

Kwa wenye akili tunajua huu ndio mwanzo mzuri wakuanza kupigania haki zetu.
 
Sio dhahabu tu, kuna madini 38 yenye thamani kubwa kuliko dhahabu, fungua macho sio makalio.
Sawa gharama ya makinikia yote in total ni kiasi gani ukilinganisha na pure gold inayosafirishwa kutoka migodini.

"Vile vile tume ilikuta madini ya Rhodium kg 0.034kg = ml 700 kwa makontena yote", ni aibu unaibiwa trillions of sh wewe unakomaa na mil.700 it's a shame.
 
Huu sio mgodi ni bohari zinakofichwa huku nyie mkiachiwa mashimo na mchanga mgombanie.
hapo naona tunachanganya mambo mawili.
1:Wizi wa madini...(Kusema kuna kiasi x kumbe ni y). Na zaidi ya kiasi x, kuna aina sio tu 1,2,3 bali kuna na 4,5,6,7,8... ambazo mbona hutusemi???
2:Usafirishwaji wa madini Miche za zahabu kwa njia halali lakni sheria na taratibu tulizojiwekea ambazo nadhani haziko upande wetu.
Pia ukumbuke sio Wawekezaji tu hata wewe mtanzania ukiwa na mgodi sheria hiyohiyo utalipia 4% hadi upate faida.
maana uwekezaji wa migodi sio kama kibanda cha cherehani. Unahitaji Mtaji mkubwa sana.
Kama tunataka kuwafanya walipe 30% income tax siku wanaanza tubadili sheria.
Kuhusu ni mali ya nani. Ukianzisha kiwanda cha matofari hayo matofari kwa sababu yanatokana na Mchanga ambao ni mali ya tanzania utayafanya hayo matofari kuwa mali ya wananchi wanaokuzunguka:
La hasha badala yake, Utalipia kodi kwa mujibu wa sheria ili uuze bidhaa yako utakavyo.

KWa maono yangu Viongozi wetu wako kwenye jambo la kwanza, haliwazuii kuingia phase ya pili.
 
Hata ungekuwa nusu kilo ni Mali yetu .Nilazima tuupiganie.

Kwa wenye akili tunajua huu ndio mwanzo mzuri wakuanza kupigania haki zetu.
Mmepewa mfupa(makinikia) mgombanie huku wenzenu wanasafirisha nyama, hiyo ndiyo akili yenu, sisi wengine tunasema hapana.

Weledi tunasema mwanzo mzuri ni kupitia mikataba yote upya.
 
Mtoa mada pima akili yako kwanza, yangekuwa na thamani ndogo wasingesafirisha, fikiria cost za usafirushaji halafu cost za kufanya refinal unafikiria wao wajinga? Hizo ni mbinu zao za kutorosha madini yetu
 
Pia ukumbuke sio Wawekezaji tu hata wewe mtanzania ukiwa na mgodi sheria hiyohiyo utalipia 4% hadi upate faida.
Hizo akili za kuwatetea eti hadi wapate faida ndizo hatuzitaki. Ndio maana tunataka waliokubaliana 4% ikiwezekana wanyongwe, haiwezekani wachimbe zaidi ya miaka 17 watuambie bado wanapata hasara, ningekuwa Rais leo ningewaambia waondoke na makinikia yao.
 
Mtoa mada pima akili yako kwanza, yangekuwa na thamani ndogo wasingesafirisha, fikiria cost za usafirushaji halafu cost za kufanya refinal unafikiria wao wajinga? Hizo ni mbinu zao za kutorosha madini yetu
Usikurupuke soma mada inasemaje it is a comparison topic, kati ya 5% makinikia na 95% dhahabu iliyoko migodini kipi utaanza ku dili nacho.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom