Poor Jornalism IPP | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Poor Jornalism IPP

Discussion in 'Matangazo madogo' started by mgomi, Aug 24, 2008.

 1. m

  mgomi Member

  #1
  Aug 24, 2008
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK amwaga vigogo sita

  2008-08-23 15:43:59
  Na Mwandishi Wetu, Jijini


  Wale vigogo wanaotuhumiwa kuchota mapesa ya umma kwa manufaa yao, waliodhani Rais Jakaya Kikwete atawakingia kifua, sasa wameula wa chuya kwani JK kawanawa kama hawajui vile.

  Katika kudhihirisha kwamba hivi sasa kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe, imedaiwa kuwa, JK ameapa kutoingilia kwa namna yoyote mamlaka ya kisheria kuchukua mkondo wake, hata kama watuhumiwa ni watu walio karibu naye.

  Taarifa kutoka kwa chanzo cha gazeti hili, zinadai kuwa ni kutokana na msimamo huo ambapo JK ametoa baraka zake ili watuhumiwa wote wa sakata la ufisadi, waburuzwe kortini ili kukabiliana na tuhuma zinazowakabili.

  ``Hali sasa ni ngumu kwa baadhi ya waheshimiwa maana mzee (rais) amesema hatamlinda mtu yeyote, japokuwa baadhi ya watuhumiwa ni watu wanaofahamiana vizuri,`` kimedai chanzo chetu kutoka Serikalini.

  Kwa mujibu wa chanzo hicho, kila kigogo ambaye ushahidi utaonyesha zipo hoja za msingi za kumburuza kortini, JK hataingilia kwa namna yoyote.

  ``Wale watuhumiwa sita aliosema mzee katika hotuba yake juzi kwamba watafikishwa kortini, ni mwanzo tu, wengine watafuata,`` chanzo hicho kimedai.

  Kwa mujibu wa chanzo hicho, Rais Kikwete amefikia uamuzi huo wa kuacha watuhumiwa hata kama ni vigogo waumbuke mahakamani, kwa lengo la kufanikisha vita dhidi ya rushwa na kuiletea heshima Serikali yake.

  ``Unajua siku zilizopita kuna watu walidhani sheria inafanya kazi kwa watu wadogo tu, sasa hilo halipo. Yeyote ambaye kuna ushahidi wa kutosha wa kumburuzwa kortini, atabebwa tu,`` kimeongeza chanzo hicho.

  Akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juzi, Rais Kikwete alisema Taasisi ya Kupambana na Kuzuia rushwa nchini, TAKUKURU inakusudia kufikisha mahakamani kesi sita za rushwa kubwa.

  ``Kesi nyingine sita uchunguzi wake umekamilika... ziko mbioni kufikishwa kortini,`` alisema Rais Kikwete.

  Akizungumzia hatua nyingine za mapambano dhidi ya rushwa ambazo tayari zimeshughulikiwa na Serikali, Rais Kikwete alisema kesi zilizofikishwa kortini zimeongezeka kutoka kesi 50 mwaka 2005 hadi kufikia kesi 156 mwaka huu.

  Akasema TAKUKURU ambayo ndiyo inayosimamia kesi hizo tayari imeshinda kesi 35 kutoka kesi sita tu ilizokuwa imeshinda mwaka 2005.

  Aidha akasema ili kuimarisha vita dhidi ya rushwa, Serikali imeajiri vijana 442 katika Taasisi ya kupambambana na Kuzuia Rushwa, TAKUKURU kwa ajili ya kuwadaka wala rushwa.
   
 2. B

  BigMan JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2008
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  poor jornalism how ?
   
 3. v

  vassil Senior Member

  #3
  Aug 27, 2008
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  calling it poor is an understatement, this is evil journalism it's like there are two jk sitting in statehouse,one in the eyes of IPP media and the other one for the rest of us
   
Loading...