Pool tables zilizotapakaa kila mahala TZ ni sumaku ya uvivu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pool tables zilizotapakaa kila mahala TZ ni sumaku ya uvivu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nzi, Mar 4, 2011.

 1. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,533
  Trophy Points: 280
  Salaam wanaJF!

  Kwakweli huu mchezo kwa TZ unafanywa visivyo na mwishowe umekua ni kituo cha vijana kukaa siku nzima bila kujishughulisha!

  Kwa wale waliobahatika kutembea hapa TZ watakubaliana nami,kua meza za mchezo huu zimetapakaa kila kona ya nchi hii;ukisafiri kwa njia ya barabara ndo utashuhudia hiki. Barabarani kote iwe kutoka Dar kwenda Morogoro-Iringa-Mbeya-Rukwa au Dar kwenda Morogoro-Dodoma-Manyoni-Singida-Igunga-Nzega-Shinyanga-Misungwi-Mwanza. Kutoka Dar kwenda Arusha kupitia Chalinze-Lugoba-Segera-Korogwe-Mombo-Hedaru-Mwanga-Same-Njia Panda/Himo-Moshi-Bomang'ombe-USA River-Arusha. Humu kote njiani kumetapakaa pool tables na vijana wenye nguvu na akili wakicheza mchezo huo kutwa nzima kuanzia asubuhi mpaka machweo!

  Mchezo huu ni mzuri lakini kwa hapa TZ nafikiri hautumiki ipaswavyo. Kwa wenzetu naona mchezo unapatikana kwny pubs sana,lakini si mtaani tena nje nje kama hapa kwetu.

  Hapa serikali ya mkwere haikosi lawama tena katika mitazamo miwili. Moja kwa serikali kushindwa kuweka mfumo wa namna ya kugovern na kuadminister mchezo huu. Pili kwa serikali kushindwa kuweka misingi ya kuwezesha vijana wafanye kazi(inaonekana wengi wa vijana hao wamekata tamaa ya maisha,hawaoni nyuma wala mbele) kwa kujituma na bidii,ivyo wanaona vijiwe vya pool tables kama stress releasers!

  Nini kifanyike wadau? Maana mara nyingi nikipitaga kwny vijiwe vya pool huwa nawashauri vijana wakajishughulishe kwani kwa kukaa kwny vijiwe ivyo wanakua wavivu. Lakini mara zote nao husema kua wakajishughulishe na nini?!
   
 2. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mada safi sana mkuu. Upande wa pili wa shilingi ni kwamba, hawa wanaocheza pool kwenye saa za kazi wana tatizo la ajira, either wako underemployed or unemployed.
   
 3. doup

  doup JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  wengine kwao huo ni ujasilia mali, eti wamewekeza
   
 4. bona

  bona JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  sidhan kama unaweza walaumu kwani wakikuomba kazi utawapa, and i can assure you sio kama wanapenda sana its just that hawana cha kufanya!
   
 5. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,533
  Trophy Points: 280


  Nakubaliana nawe mkuu. Kwenye hili suala la ajira. Ila hapo serikali ina lawama zake,kwani vijana hao wamekosa dira na matumaini.
   
 6. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,533
  Trophy Points: 280

  Sawa ni ujasiriamali. Lakini si katika mazingira haya. Serikali ilipaswa kuja na mwongozo na taratibu ya kuendesha mchezo huu nchi nzima. Ipige marufuku uwekaji wa meza hizo nje nje (angalau mtu ajenge pub au sports parlour fulani,ili mtu kupata huduma ya mchezo huo,lazima agharimike zaidi ya kununua tokeni tu). Hii itapunguza mchezo huu kua vijiwe vya watu wanaokaa siku nzima bila kazi.
   
 7. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,533
  Trophy Points: 280

  Mkuu kuwalaumu ni sawa kabisa. Kwani wengi wao ndo hao walioshiriki kuiweka serikali iliyopo madarakani. Wengi wao ndo wanaodanganyika na tisheti,kofia na elfu 10 10 za msimu wa uchaguzi. Kama hawana cha kufanya na wanakaa na kujifanya wanazoea shida,then lawama pia zinawaangukia!
   
 8. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Kuna wakati serikali iliweka amri ya kutocheza pool mpaka saa 10 jioni, hata unywaji wa pombe hapa Dar nao uliwekewa vikomo. Ila kutokana na siasa kuwa nyingi kuliko utendaji wa dhati, hata sielewi ile amri ilipotelea wapi. Upande wa hao vijana, mimi nimekaa nao, wengi ni wavivu na wanaopenda maisha ya mkato, wao hukaa vijiweni kwa kuwa nyumbani kuna kina mama wanaowapikia. Je, kila kijana mtaani hushinda kwenye pool? Kuthibitisha hoja yangu, tabia ya vijana wavivu wa kwenye pool huendana na kuendekeza ngono, ulevi, bhange na kadhalika. Tusikimbilie ukosefu wa ajira kuwa mwamvuli wa maovu yetu!
   
 9. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Seriously huo ni uwekezaji mkubwa sana you just do not know. Swala la kwamba vijana wanacheza mida yote to me sio issue yangu kama mjasiriamali kama serikali yao haijawapatia ajira mimi mwenye meza nimejipatia ajira. Sehemu nyingine kuliko ununue Hiece bora uwe na pool table moja inalipa zaidi...trust me!
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Kama wengi walivyosema ile ni biashara kwa wamiliki wa zile pool table.
   
 11. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,533
  Trophy Points: 280


  Sijakataa kama ni biashara. Je,ndo tunahitaji biashara ya kuneemesha mtu mmoja? Huo si ndo ubinafsi tunaoupigia kelele? Je,tunataka vijana wetu walundikane kwny kijiwe kimoja siku huku wakiwa hawazalishi chochote chenye tija kwa taifa,eti kwa sababu pool tables ni biashara kwa wajasiriamali?

  Kwa mtazamo huo hakika hatutafika hata chichiemu ikiachia ngazi.

  Hakika utaifa umeshapotea miongoni mwetu. Kilichobaki ni ubinafsi.
   
Loading...