Ponywa na epuka magonjwa "KIMAANDIKO" bila Dawa

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,701
" Moyo uliochangamka ni Dawa nzuri, Bali roho iliyopondeka hukausha mifupa" Mithali 17:22

Uchangamfu unaozungumzwa hapa ni ule ambao unaletwa kama matokeo ya Kumuamini Mungu na Neno lake.

Sio ule unaoletwa kwa kunywa pombe, kuvuta bangi au madawa ya kulevya, kuchepuka, kushelekea vitu ulivyovipata kidhalimu. Uchangamfu huu ukitunha Mimba huzaa Misongo, vidonda vya tumbo, ufukara wa kings mwilini, visukari,BP, na baadaye kuzaa vifo vya kujitakia na kujipangia.

Siri ya kuwa mzima haiko katika varanda na vyumba vya mahospitali, vilinge vya maombezi wala mitishamba. Bila Furaha ambayo ni tokeo la Kumuamini Mungu katika hali zote utaishia kukauka mifupa. Kumbuka ndani ya mifupa ndio kuna uroto ambao ni kiwanda cha kutengeneza Kinga, na majeshi ya mwili kukabili magonjwa.

Mtegemee Mungu ili anenepeshe mifupa na akupe Furaha ambayo ni Dawa bila Malipo.

Je, unataka kujua zaidi kuhusu sayansi ya kuepuka magonjwa kwa njia ya Neno LA Mungu. Endelea kufuatilia.
 
Back
Top Bottom