Zero Hours
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 12,944
- 18,652
Ni matumaini yangu kuwa, asilimia kubwa ya members wa JF ni watu wazima kabisa na wanaojielewa. Kwa uelewa wangu, mtu mzima anayejielewa hawezi jumuika katika maandamano yayosemekana kuandaliwa kwa nia ya kumpongeza JPM kwa hatua aliyofikia mpaka sasa juu ya Wizi wa Mali za Umma hasa madini yetu yaliyokuwa yakisombwa na Acacia.
Hivyo basi, Ninapendekeza kwa wale wanajamii forum walioguswa na wangependa kutoa pongezi au shukurani zao za dhati kwa Rais JPM, tuchukue nafasi hii kufanya ivyo kupitia uzi huu.
Si vibaya kumpongeza mtu hata kama kafanya mabaya mengi lakini hata akifanya zuri moja tu ni vyema kumpongeza ili aendelee kufanya mazuri kama haya.
Mi binafsi ningeaza kwa kumpa hongera kwa hatua aliyofikia mpaka sasa. Mi ni mmoja wa wale tulidhani ni maigizo ya kutafta kiki kwa pikipiki. ila hivi leo tumeanza muelewa. Ningependa pia kumkumbusha kuwa hata sisi Wapinzani ni Watanzania. Sisi wote ni ndugu. Tunataka maendeleo ila undugu wetu pia tunapenda uendelee kama alivyoukuta....
ANGALIZO.
Napendekeza tutoe pongezi bila mihemko. Ninajua wapo baadhi yenu ambao mnaweza kuwa tofauti au mkipingana na hatua alizochukua Magufuli. Ila ningewaomba kama mpo opposite mpite kushoto maana uzi huu hauwahusu.