Pongezi za Selasini kwa Serikali zawa gumzo bungeni

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu,

Tulishawahi kusema ipo siku kila mmoja ataongea ukweli wake.
=====
1580221878830.png
Pongezi kwa Serikali ya Tanzania zilizotolewa na mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini bungeni mjini Dodoma zimeibua shangwe kutoka kwa wabunge wa CCM.

Dodoma. Pongezi kwa Serikali ya Tanzania zilizotolewa na mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini bungeni mjini Dodoma zimeibua shangwe kutoka kwa wabunge wa CCM.

Mbunge huyo ambaye hivi karibuni alijiuzulu kuwa kaimu mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ameipongeza Serikali leo Jumanne Januari 28, 2020 alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kuhusu upatikanaji wa maji wilayani Rombo.

Selasini amesema hivi sasa katika jimbo lake maji yanatoka, kuishukuru Serikali.

Awali, naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema Serikali imepanga kutumia chanzo cha maji cha ziwa Kyara kufikisha maji Rombo, kwa kuanza inapeleka Sh1.5 bilioni.

"Kwa awamu zote za Serikali na wabunge walionitangulia wamekuwa wakitaka ziwa Kyara litumike kama chanzo cha maji lakini haikuwezekana, lakini Serikali hii naipongeza imewezesha," amesema Selasini.

Chanzo: Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabunge wengi tu wa upinzani huishukuru serikali hata Peter Msigwa aliwahi kuishukuru serikali sema akili zako zimeshindwa kung'amua kati ya kushukuru serikali na kushukuru chama cha mapinduzi...kwa akili zako utasema amekishukuru chama cha mapinduzi...Kwa wasiolewa wanadhani huduma za kijamii kama maji,umeme,barabara ,miundombinu ya Elimu ni ya kushukuru ,wananchi tunalipa kodi na tunatakiwa kuletewa huduma hizo kwa sababu kazi mojawapo ya serikali yoyote kuleta huduma hizo...hizo sio hisani ni mahitaji muhimu ya wananchi ambyo serkali inatakiwa ipeleke moja kwa moja kwa wananchi bila kuombwa.
 
Hakuna mbunge ambaye hataki kurudi bungeni, huu ndio muda wa kuwajua wanasiasa wetu rangi zao halisi.
 
Kwahiyo nayo hii ni habari ya kuweka hapa JF kuwa ccm wamepongezwa na mbunge wa chadema halafu unaenda kupewa buku7 pale na bwana Slow down, Lumumba kirahisi tuu hivi. Elimu Elimu Elimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
After money kazini huyu anajipekecha mapema ili aendelee na ubunge wake Kwa upande wa CCM hakika mchaga ni Noma Kwa kuchungulia fursa.
Na dawa ya Magufuli ni sifa Tu atakupa kila kitu..... hongera selassini Kwa kuchungulia mipango mapema
 
Back
Top Bottom