Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,738
- 155,426
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amempongeza Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kwa kukiri kumiliki kadi ya CCM hadi leo.
"Kwanza nampongeza kwa kuanza kujifunza kusema ukweli maishani mwake, bila shaka ametambua kuwa uongo haulipi. Kitendo cha kukiri anamiliki kadi ya CCM bado ni cha kiungwana, kwa hili nampongeza, alisema Nape.
Akijibu tuhuma za Nape alizotoa juzi kwamba, baadhi ya vigogo wa Chadema akiwemo Dk Slaa bado wana kadi za CCM na baadhi yao wanaendelea kuzilipia, Katibu huyo wa Chadema alikaririwa kukiri kuwa na kadi ya CCM na kwamba anaitunza kama kumbukumbu muhimu kwake.
Pamoja na pongezi hizo, Nape amemtaka Dk Slaa kuwambia Watanzania kwamba kadi hiyo ameilipia mpaka lini na pia aache tabia ya kuwadanganya wenzake kurudisha kadi zao za CCM huku yeye akibaki na yake kibindoni.
Ni vizuri sasa Dk Slaa awaambie Watanzania amelipia mpaka lini kadi hii. Lakini aache kuwadanganya wenzake kurudisha kadi zao huku yeye akibaki na yake, huu ni unafiki," alisema Nape.
Nape ambaye amekiri kumheshimu Dk Slaa kama babu yake, amesema alishtuka kusikia Katibu Mkuu huyo wa Chadema akiwatuhumu viongozi wa chama hicho, hivi karibuni kuwa ni mamluki wa CCM huku akijua yeye ni mamluki namba moja kwani wenzake hawana kadi za CCM yeye anayo.
"Nimesikia anahoji hili linawasaidiaje Watanzania masikini? Swali hili limethibitisha upeo mdogo wa kufikiri wa kiongozi mkubwa na ninayemheshimu kama huyu. Lazima ajue kwamba yeye anaomba kuwa kiongozi hivyo lazima wananchi tumjue tabia zake," alisema Nape na kuongeza;
"Viongozi wanafiki wa aina yake ni janga kwa taifa letu. Usipokuwa mwaminifu kwa kidogo huwezi kuwa mwaminifu kwa kikubwa. Lazima anayetaka kuwa kiongozi aishi kwa anayoyasema."