Pongezi za Nape kwa Dr. Slaa ni za kizushi na kinafiki

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
67,485
130,814
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amempongeza Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kwa kukiri kumiliki kadi ya CCM hadi leo.

"Kwanza nampongeza kwa kuanza kujifunza kusema ukweli maishani mwake, bila shaka ametambua kuwa uongo haulipi. Kitendo cha kukiri anamiliki kadi ya CCM bado ni cha kiungwana, kwa hili nampongeza,” alisema Nape.

Akijibu tuhuma za Nape alizotoa juzi kwamba, baadhi ya vigogo wa Chadema akiwemo Dk Slaa bado wana kadi za CCM na baadhi yao wanaendelea kuzilipia, Katibu huyo wa Chadema alikaririwa kukiri kuwa na kadi ya CCM na kwamba anaitunza kama kumbukumbu muhimu kwake.

Pamoja na pongezi hizo, Nape amemtaka Dk Slaa kuwambia Watanzania kwamba kadi hiyo ameilipia mpaka lini na pia aache tabia ya kuwadanganya wenzake kurudisha kadi zao za CCM huku yeye akibaki na yake kibindoni.

“Ni vizuri sasa Dk Slaa awaambie Watanzania amelipia mpaka lini kadi hii. Lakini aache kuwadanganya wenzake kurudisha kadi zao huku yeye akibaki na yake, huu ni unafiki," alisema Nape.

Nape ambaye amekiri kumheshimu Dk Slaa kama babu yake, amesema alishtuka kusikia Katibu Mkuu huyo wa Chadema akiwatuhumu viongozi wa chama hicho, hivi karibuni kuwa ni mamluki wa CCM huku akijua yeye ni mamluki namba moja kwani wenzake hawana kadi za CCM yeye anayo.

"Nimesikia anahoji hili linawasaidiaje Watanzania masikini? Swali hili limethibitisha upeo mdogo wa kufikiri wa kiongozi mkubwa na ninayemheshimu kama huyu. Lazima ajue kwamba yeye anaomba kuwa kiongozi hivyo lazima wananchi tumjue tabia zake," alisema Nape na kuongeza;

"Viongozi wanafiki wa aina yake ni janga kwa taifa letu. Usipokuwa mwaminifu kwa kidogo huwezi kuwa mwaminifu kwa kikubwa. Lazima anayetaka kuwa kiongozi aishi kwa anayoyasema."
 
Magwangala

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
2,146
1,129
Mnafiki mkubwa,bado ana machungu ya kukosa ugombea ubunge wa jimbo la ubungo kupitia CDM,alidhani ataweza kumpiku Mnyika,amuulize Mtatiro!
 
bantulile

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,572
602
Kama Dr. Slaa ni mamluki wa CCM, kwa akili ya kawaida Nape, Katibu mwenezi wa CCM asingethubutu kueleza siri hii hadharani. Kwa kuthubutu kwake Nape katibu mwenezi wa CCM kueleza haya ni ishara tosha kuwa hizi ni siasa za maji taka. Mamluki ni lazima andike taarifa ya mabo aliyoyaona kwenye chama alikotumwa kupeleleza, Nape aweke hapa kwenye JF mojawapo ya taarifa iliyoandikwa Dr. Slaa kama ushahidi wa hoja yake. Maneno yote kumheshimu Dr. Slaa kama babu yake hayatuongezei shibe yoyote. Mwaga ushaidi hapa, tuuone vinginevyo watu watakupuuza. Pili kama ni kawaida ya Nape kuropoka siri za chama chake wataje mamluki wengine zaidi ya Dr. Slaa.
 
Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,461
Kila nikisoma au kumsikiliza huyu dogo nakumbuka njaa inavyoweza kumaliza ubongo mwanadamu na kumfanya mwehu. Ninakila sababu za kuamini dogo ni mwehu bila shaka yeyote.

Nape anahitaji matibabu ya haraka. na dalili za ndondocha ni pamoja na kunenepa hovyo.
 
REMSA

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,579
929
Dr.Slaa babu wa Nape!!??au Dr Slaa baba wa Mwandosya!!?
 
chama

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
8,001
2,414
Personal issues zinaingiaje kwenye mjadala wa kisiasa?
Hoja ijibiwe kwa hoja

Unawazimu hapa hakuna cha personal issue tunaangalia ETHICS and INTEGRITY; Slaa ni muongo hafai hata kuwa katibu kata!!
 
Lusaa

JF-Expert Member
Sep 12, 2011
270
112
Personal issues zinaingiaje kwenye mjadala wa kisiasa?
Hoja ijibiwe kwa hoja

Personal issue ziko wapi hapo? Kwanini hujiulizi kama Dr Slaa anasababu za msingi za kuendelea kumiliki kadi ya Magamaba hadi leo.
 
abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=2]Wednesday, December 5, 2012[/h][h=3][/h]

UWT, MBUNGE WAZOZANA ARUSHA

KATIBU Mkuu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibroad Slaa, amemvaa Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Itikadi na Uenezi ya CCM, Nape Nnauye akisema madai aliyoyatoa dhidi yake ni ya kipuuzi na yasiyokuwa na tija kwa Watanzania waliopigika na umasikini.

dr_slaa.jpg
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Nape kudai kuwa katibu huyo ni CCM damu ndiyo maana hata kadi yao ameendelea kuwa nayo hadi leo licha ya kuhamia CHADEMA.

Akifungua mkutano wa NEC Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza juzi, Nape alidai kuwa Dk. Slaa tangu aikimbie CCM na kuhamia CHADEMA hajarudisha kadi yao.

Hata hivyo, Dk. Slaa licha ya kukiri kuwa na kadi hiyo ya CCM hadi leo, alifafanua kuwa hiyo ni mali yake halali na ameihifadhi kwenye makumbusho kwa ajili ya kumbukumbu kwa ajili ya wajukuu zake na vizazi vijazo.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Dk. Slaa alisema madai ya Nape ni hoja ya kipuuzi isiyokuwa na tija kwa wananchi na kwamba hazina mashiko, bali zimelenga kupoteza muda na wananchi.

"Kadi ni mali yangu, na nimeihifadhi kwenye makumbusho kwa ajili ya historia ya wajukuu. CCM wanaweweseka kutokana na kushindwa kwake kuisimamia Serikali yao ili kuwaletea maendeleo wananchi,” alisema.

Dk. Slaa alitamba kuwa Nape na wenzake waachwe wapige mayowe, lakini mwaka 2015 ndiyo wataisoma namba. Kwamba huo utakuwa mwisho wa CCM maana CHADEMA wanaandaa mipango bora zaidi ya kuwasaidia Watanzania kimaendeleo.

“Na Tanzania itakuwa mfano mkubwa wa kimaendeleo katika utawala wa CHADEMA," alisema Dk. Slaa huku akisisitiza kwamba umasikini uliowagubika Watanzania mwisho wake ni 2015.
CCM wavurugana

Jijini Arusha vita ya makundi ya urais 2015 ndani ya CCM, imeanza kujitokeza upya baada ya kuibuka mvutano mkali kati ya Mwenyekiti wa Jumiuya ya Wanawake (UWT) mkoani hapa, Florah Zelote na mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige.

Licha ya Magige kutoka mkoa huo akipitia kundi la vijana, mwenyekiti wa UWT anadai kuwa mbunge huyo anajipitisha na kutoa misaada kwa lengo la kusaka ubunge kupitia jumuiya hiyo mwaka 2015.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili, zinasema kuwa Zalote alitoa madai hayo kwenye kikao cha baraza la UWT wilaya ya Arumeru Novemba 30, mwaka huu, ambapo anadaiwa kuwaeleza wajumbe kuwa Magige hana jipya kwani misaada anayotoa ni ya kutaka kujijenga ili apate ubunge kupitia jumuiya hiyo.

Kwamba Mwenyekiti huyo aliweka wazi kuwa UWT mkoani Arusha inawakilishwa bungeni mmoja tu, Namelok Sokoine ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani, hayati Edward Sokoine.

Habari za ndani zinadai kuwa Zalote, alitumia kikao hicho kuwahamasisha wanawake kutohudhuria hafla ya uzinduzi wa taasisi ya Magige, iliyokuwa ikifanyika siku hiyo akidai kuwa kuhudhuria ni ‘kumpa ujiko’ mbunge huyo wa kuwania ubunge wa UWT 2015.

Akizungumza kwa simu na gazeti hili jana, Zelote alikiri kutohudhuria hafla hiyo iliyoandaliwa na Magige kutokana na kuwa na majukumu mengine ya kiofisi.

Hata hivyo alikanusha madai ya kumzungumzia Magige kwenye kikao hicho ingawa alikiri kuwa alikuwa na mwaliko wa hafla ya uzinduzi wa taasisi yake maendeleo lakini alishindwa kuhudhuria.

Alisema kuwa alitoa udhuru kupitia katibu wake ambaye alijibu barua ya mwaliko iliyofika ofisini kwake kwa kuwaarifu kuwa hataweza kuhudhuria kwani atakuwa wilayani Arumeru.

“Ninajua utawala bora na ninauheshimu sana, sijamtaja Magige popote, hata wakati wa kikao changu, nilimuongelea mwakilishi wetu wa UWT bungeni, Namelok Sokoine yeye ndiye nilimsemea kwa wajumbe kuwa kwa sasa hawamuoni kwani yuko nje ya nchi anamuuguza mama yake, lakini akirudi tutapita naye kwenye maeneo yao,” alisema.

Aliongeza kuwa ni vema Magige kama ana malalamiko afuate taratibu za chama badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari.

Naye Magige aliliambia gazeti hili kuwa ameamua kuzindua taasisi hiyo kwa ajili ya kusaidia jamii ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake ya kibunge.

Alisema kuwa akiwa ni mbunge anayetokana na CCM ana wajibu wa kutekeleza Ilani ya chama hicho jambo alilodai kuwa anaamini hata mwenyekiti huyo wa UWT anatakiwa kulifanya.

Kuhusu kugombea ubunge kupitia UWT mwaka 2015, Magige alisema hiyo ni haki yake kikatiba na akitaka hakuna wa kumzuia.

Chanzo Tanzania Daima

Posted by Abdul at 11:25 AM
 
idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,095
37,206
mimi nashuri aichome hadharani,ili kuepukana na huu ujinga wa Nappe.!!
 
Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,046
6,510
Aimiliki Kadi ya CCM au hasiimiliki kuna faida gani kwa watanzania. Nape bora akajiunge na Komba wawe wanaimba nyimbo za "TUNACHUKUA, TUNAWEKA, WAAAAA"
Sio mwanasiasa makini Nape!
 
Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,046
6,510
Unawazimu hapa hakuna cha personal issue tunaangalia ETHICS and INTEGRITY; Slaa ni muongo hafai hata kuwa katibu kata!!

Gombea wewe uone kama hutapata kura 1 ya kwako tu; hata mpenzi wako hawezi kukupigia kura.
 
sifongo

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,896
5,296
Ccm acheni siasa za kipuuzi, kwani kadi kitu gani jana tu nimeona yangu ya clinic enzi hizo hii haina maana bado nahuhudhuria clinic.......hembu serikali ya ccm nendeni huko ngorongoro wananchi wanakufa na njaa wanahitaji msaada kadi ya slaa haisaidii kitu, anaweza akawa nayo ili akiitazama ajione jinsi alivyowakosea watanzania kuwa mwanachama wa ccm miaka hiyo.
 
chama

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
8,001
2,414
Samahani mkuu nilishawahi kupata umbea eti Nape sio mtoto wa Brigadia Moses Nnauye, wanaojua watujuze, it might look personal lkn kwakuwa sasa ni public figure ni vema tukaingia uvunguni ili muda mwingine tuwe na tentative conclusions.

Wewe unauhakika huyo uliyeambiwa baba yako ni baba yako? Anza kwako kwanza halafu ndiyo tuje kwa Nape; wadau wanasema baba yako ni yule muuza genge jirani!
 
Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
5,703
1,881
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amempongeza Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kwa kukiri kumiliki kadi ya CCM hadi leo.

"Kwanza nampongeza kwa kuanza kujifunza kusema ukweli maishani mwake, bila shaka ametambua kuwa uongo haulipi. Kitendo cha kukiri anamiliki kadi ya CCM bado ni cha kiungwana, kwa hili nampongeza,” alisema Nape.

Akijibu tuhuma za Nape alizotoa juzi kwamba, baadhi ya vigogo wa Chadema akiwemo Dk Slaa bado wana kadi za CCM na baadhi yao wanaendelea kuzilipia, Katibu huyo wa Chadema alikaririwa kukiri kuwa na kadi ya CCM na kwamba anaitunza kama kumbukumbu muhimu kwake.

Pamoja na pongezi hizo, Nape amemtaka Dk Slaa kuwambia Watanzania kwamba kadi hiyo ameilipia mpaka lini na pia aache tabia ya kuwadanganya wenzake kurudisha kadi zao za CCM huku yeye akibaki na yake kibindoni.

“Ni vizuri sasa Dk Slaa awaambie Watanzania amelipia mpaka lini kadi hii. Lakini aache kuwadanganya wenzake kurudisha kadi zao huku yeye akibaki na yake, huu ni unafiki," alisema Nape.

Nape ambaye amekiri kumheshimu Dk Slaa kama babu yake, amesema alishtuka kusikia Katibu Mkuu huyo wa Chadema akiwatuhumu viongozi wa chama hicho, hivi karibuni kuwa ni mamluki wa CCM huku akijua yeye ni mamluki namba moja kwani wenzake hawana kadi za CCM yeye anayo.

"Nimesikia anahoji hili linawasaidiaje Watanzania masikini? Swali hili limethibitisha upeo mdogo wa kufikiri wa kiongozi mkubwa na ninayemheshimu kama huyu. Lazima ajue kwamba yeye anaomba kuwa kiongozi hivyo lazima wananchi tumjue tabia zake," alisema Nape na kuongeza;

"Viongozi wanafiki wa aina yake ni janga kwa taifa letu. Usipokuwa mwaminifu kwa kidogo huwezi kuwa mwaminifu kwa kikubwa. Lazima anayetaka kuwa kiongozi aishi kwa anayoyasema."
Mkuu huyo mheshimiwa Nape ameona Dr Slaa kuwa na kadi ya CCM ni janga la taifa kuliko viongozi wakuu wake walioficha mabilioni yetu huko ulaya???? Kwani Dr Slaa kumuita janga ameficha fedha zetu Uswiss, kama ni kadi si alikata kwa hiari yake au aliiba hiyo kadi toka CCM????? Mwambie Nape aache kabisa kupotosha Watnzania wakati yeye analinda wezi kuanzia EPA, RICHMOND, BUZWAGI,MEREMETA, list ni ndefu. Nape yeye kamuona Dr Slaa kumiliki kadi ya CCM ni janga, awaambie wakubwa zake warudishe fedha zetu waache kufilisi taifa letu!!!!! Nape atwambie mambo yamaana ya kuinua uchumi wa nchi yetu aache ngonjela itakuwa yeye ndilo janga anaye linda wezi na mafisadi!!!!

Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
5,703
1,881
Unawazimu hapa hakuna cha personal issue tunaangalia ETHICS and INTEGRITY; Slaa ni muongo hafai hata kuwa katibu kata!!
Wezi wa fedha zetu ndio unaona wanafaa kuliko Dr mwenye kadi ya kumbukumbu ya CCM, KOSA LA Dr Slaa ni nini ameiba nini????
 
assuredly4

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
1,216
217
giLESi Nape hana jipya ni kawaida yake kuropoka. mwambie awaulize wenzake waliokuwa wananchama wa TANU zile kadi walirudisha kwa nani? yeye mwenyewe kadi ya CCJ alirudisha kwa nani? je vitambulisho vya shule tulizosoma tulirudisha lini? hakuna ajabu yoyote Dr. Slaa kutorudisha kadi ya CCM kwasababu wangejidai na kujinafasi ndiyo maana yeye hajatatak kuirudisha.

ccm bwana wakikamatwa pabaya hata majani anashikilia ili waonekanae, ccm watueleze miaka 50 ya uhuru kwann bado wanadai Tanzania nchi changa na maskni? mdogo wake yuko wapi? kwann hamna maji, umeme, shule za maana, nyumba za walimu, vitabu vya kufundishia, huduma bora za afya n.k. kwannn rushwa imekithiri na kupindukia

Nape atueleze sera ya kujivua gamba imetekelezwa vipi. kwann watz bado maskn pamoja na utajiri mwingi uliopo?
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom