Pongezi za dhati kwa "survivors", pole kwa waliopitiwa na msumeno

Darcityconfidential

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
351
367
Habari wana-JF,

Awali ya yote, namshukuru MUNGU kwa zawadi hii ya uzima. Nusu ya kwanza ya mwaka 2020 imekua mgumu mno, ni kipindi ambacho kimefanya tujifunze vitu vingi sana kuhusu umuhimu wa kujali afya zetu sisi kama binadamu. Tulikumbwa na maambukizi ya ugonjwa wa corona virus (COVID19), ilituyumbisha sana kwa namna moja ama nyingine, kiafya ya akili, kiafya ya mwili, kiuchumi n.k. Hivyo ni jambo la msingi kabisa kushukuru MUNGU.

Sasa, moja kwa moja kwenye mada, binafsi, natoa pongezi za dhati kabisa kwa viongozi wote na watumishi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Mh. Dr. John Pombe Magufuli waliofanikiwa kwenda na kasi ya serikali kwa weledi na uadilifu. Binafsi nadhani awamu hii ya tano ni awamu ambayo ilikua ngumu, hasa kwa viongozi na watumishi wa serikali, hii awamu sio ya mchezo mchezo, unapokosea ama kukiuka sheria kinachofuata baada ya kuonywa huwa ni kuwajibishwa. Hivyo nimeona vema kutoa pongezi kwa wote waliofanya kazi kishupavu kwa kufuata taratibu na sheria hadi wakati huu ambapo tunajiandaa na uchaguzi mkuu hapo badae Oktoba 2020. Hongereni kwa kazi nzuri na MUNGU awabariki.

Pia natoa pole na kuwatia moyo wale wote waliowajibishwa kwa namna moja ama nyingine. Tumekua mashuhuda wa tenguzi na kufutwa kazi kwa viongozi na watumishi wa serikali walioshindwa kwenda na kasi ya serikali ya awamu ya tano tangu ilipoanza mwaka 2015 hadi sasa tunapoelekea uchaguzi mkuu oktoba 2020.

Mwisho, maoni yangu kwa viongozi na watumishi wa serikali waliopo na watakaoendelea kuwepo hata baada ya awamu ya tano, UADILIFU ndio nguzo ya maendeleo kwa wananchi, wasitumie vibaya mamlaka waliyopewa na wawe waadilifu.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom