Pongezi za dhati kwa Rosemary Mwakitwange.........Kazi nzuri jana

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Watanzania tujenge tabia ya kupongezana mwenzetu anapofanya kazi nzuri na jana bila ya usimamizi wa karibu na wenye utashi uliotukuka wa dada yetu Rosemary si dhani kama mdahalo wa Dr. Slaa ungelifana jinsi ulivyofana.

Maswali ya awali ambayo Rosemary aliyauliza yaligusa karibu nyanja zote ambazo sisi wasikilizaji tulio mbali tungelipenda kuyauliza na kumaliza kiu tuliyokuwa nayo na huyu mgombea Uraisi ambao sis wengine tayari tumekwisha kumbatiza rasmi Raisi Mtarajiwa.

Hata wale waliokuwa na maswali na walioruhusiwa kuuliza walijikuta wakirudia hoja zile zile ambazo Rosemary alikwisha kuziuliza.

Ninachukua nafasi hii kumpongeza kwa niaba yangu binafsi na ya watanzania wengine ambao wanakubaliana na mitazamo hii.................Keep it up.
 
Ahsante kwa thread yako nzuri, binafsi huyu dada alifanya kazi professionally hivyo ni juu yetu kumpa moyo na kuwa mfano wa kuigwa. Siku zote huwa nasema in our country, Tanzania! there are smart people who can do wonders to develop the country. But politics ndo inaharibu kila kitu wakati wanaoingia ndani ya politics wanapoamua kutumia gharama zozote kuingia madarakani kwa manufaa yao binafsi.

Bravo sister Rosemary.
 
Dada Rosemary ni genius! She has always impressed me and yesterday she demonstrated her true colors, straight to the point and exploring questions! Bravo Sister!
 
Hivi huyu dada anajishughulisha na nini baada ya kutoka kwenye MAGAZETI YA ROSTAM AZIZI ?, cause jana amefanya kazi nzuri sana
 
:thumb: Rosemary. Huyu dada ni mwenye weledi mkubwa na mbunifu. Nilibahatika kufanya naye kazi Asasi moja ya Kimarekani. Ni mtu straight asiyekubali uonevu wa aina yeyote ile.
 
Kama hakuwa professional, waliouliza maswali jana wangekuwa kama nusu ya waliouliza.... Utaona alivyoamua kuunganisha maswali na kumfanya Dr aweze kuyajibu kwa pamoja comprihensively!!

Nilikupenda Rose.. Cool, collected, No nonses, Nondo_nondo, focused etc... you delivered...!

Karibu Jamiiforums... unigongee Thanks.
 
Watanzania tujenge tabia ya kupongezana mwenzetu anapofanya kazi nzuri na jana bila ya usimamizi wa karibu na wenye utashi uliotukuka wa dada yetu Rosemary si dhani kama mdahalo wa Dr. Slaa ungelifana jinsi ulivyofana.

Maswali ya awali ambayo Rosemary aliyauliza yaligusa karibu nyanja zote ambazo sisi wasikilizaji tulio mbali tungelipenda kuyauliza na kumaliza kiu tuliyokuwa nayo na huyu mgombea Uraisi ambao sis wengine tayari tumekwisha kumbatiza rasmi Raisi Mtarajiwa.

Hata wale waliokuwa na maswali na walioruhusiwa kuuliza walijikuta wakirudia hoja zile zile ambazo Rosemary alikwisha kuziuliza.

Ninachukua nafasi hii kumpongeza kwa niaba yangu binafsi na ya watanzania wengine ambao wanakubaliana na mitazamo hii.................Keep it up.

Nampongeza Rosemary Mwakitwange kwa kazi nzuri aliyoifanya jana 23-10-2010 kuanzia saa 1 hadi 3 jioni na hasa ku'organise' mdahalo. Hata alipokuwa New Habari (2006) Ltd juhudi zake zilionekana za kufanya paya day (ya mshahara) iwe tarehe 26 kila mwezi na baada ya kuacha kazi siku hizi wafanyakazi wanalipwa kila baada ya miezi 3 (siku 90). In other words, wanalipwa kila baada ya tarehe 90 au zaidi.
 
Is unfortunate that I dont know the lady, Kindly JF tupeni CV ya huyu dada
 
Pamoja na kwamba simfahamu sana lakini kazi aliyoifanya jana ilikuwa kubwa na zuri sana yenye mafanikio, Hongera sana dada ROSE kwa kazi nzuri. Ilipendeza sana!!!!!!!!
 
Hongera sana dada Rosemarry, mdaha, uloclo ulipendeza sana, uliweza controll the audience vizuri sana, na ulimpa Dr. Slaa muda wa kujibu hoja ulionyesha kabisa how professional you are, bravo sister.
 
Huyu dada Rose na akina Generali Ulimwengu, Shivji, Dr Azaveli Waitama, na baadhi ya wasomi wachache tunaowajua ni kati ya 'vifaa' muhimu sana ambao jamii yoyote ingesisimka kuwa nao maana kila wanachokaa wakabuni kinakuwa na value isiyatarajiwa na ndio maana watawala na mafisadi hawawawapi nafasi. Hongera sana Rose. Tunakuombe upange mdahalo wa mwisho ijumaa usiku pia ili Rais mtarajiwa afunge kitabu cha historia ya ukombozi na kila mtanzania ampe kura ya NDIYO hapo 31 Oct. Ndiyo fursa pekee ya kufa au kupona kwa taifa letu. ITV, Mwakitwange, Ulimwengu na waandaaji wote, hongereni sana. Tupeni tena raha Ijumaa usiku tafadhali. Kama sio kupitia ITV, basi hata chanel nyingine kama STAR TV, Tumaini au hata Mlimani TV.
 
Nami naungana na wenzangu kumpongeza Rosemary Mwakitwante. Mimi ninampongeza kwa jinsi alivyokuwa akimpa heshima Dr. Slaa, hasa the way she was addressing him.
 
hongera sana dada Da Rose, ulikuwa makini sana katika mahojiano yale na uliifanya kazi ile vizuri sana, Kula tano zako ^^^^^
 
Nampongeza dada Rosemary Mwakitwange kwa kazi nzuri ya kuratibu mdahalo wa jana 23-10-2010 kuanzia saa 1 hadi 3 jioni. Mimi nilipofahamu kuwa ni Dada Mwakitwange au Jenerali Ulimwengu ndio wanaendesha mdahalo, nilifarijika. Hata kama angekuwa ni mwanaharakati dada Ananilea Nkya au dada Kijo Bisimba napo ingekuwa poa tu, maana hawa ni watu neutral.Bravo dada Rosemary!
 
Back
Top Bottom