Pongezi za dhati kwa oungozi wa Hospitali ya Hubert Kairuki

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
2,954
8,093
Leo tarehe 06/06/2016 nilifika hospitali ya Hubert Kairuki kama mteja wa kawaida kwa ajili ya kupata huduma ya afya. Imenibidi kusafiri kutoka Mbeya ambako ndiko ninapoishi na kufanya kazi ili kufanya uchunguzi na kupata matibabu juu ya changamoto ya kiafya ambayo imenikabili hivi karibuni. Nilielekezwa na daktari mwenzangu kuwa niende Hubert Kairuki siku za jumatatu mchana ndio nitaweza kumpata daktari mmoja wa mifupa ambae ndie nilimchagua aweze kunihudumia. Kwa kuwa Kairuki wanakubali bima ya NHIF ambayo mimi ni mnufaika,nikaona nifike hapo.
Nilipofika mapokezi nilikuta mdada aliekwepo hapo mapokezi akiongea kwa ukali na wateja,na hata nilipojaribu kumuuliza utararibu wa pale ukoje (ilikuwa ni mara ya kwanza kufika hospitali ya Kairuki) alinijbu kwa ukali na kunifokea huku akiniambia "toka hapa, usinisumbue".
Baada ya kuona hali ile,nilituma meseji kuelezea kadhia ile kwenda namba ambayo ilikuwa imeandikwa pale eneo la kusubiria kuwa wateja tuitumie hiyo kuwasilisha malalamiko/kutoridhishwa na huduma. Baada ya dakika 5 nilipigiwa simu,na sauti ya upande wa pili ilijitambulisha na kusema kuwa yeye ni kiongozi hapo kairuki na kuwa ananishukuru sana kwa taarifa ile na kwamba anaifanyia kazi muda huo huo na atanipa mrejesho. Baada ya dakika 45 nilipigiwa simu tena na yule mtu na kuniambia kuwa amemuhoji mhusika na bahati nzuri amekiri kosa na kusema kuwa ni kweli alifokea wateja lakini ni kwa vile alighafilika maana alizidiwa na wateja walikuwa wengi sana na alikuwa peke yake, na ameomba msamaha kwa hilo. Pia, aliniambia kama bado nipo maeneo ya hospitali basi nipandishe ghorofani ili yule dada akaniombe msamaha uso kwa uso. Mwisho aliniambia mhusika amepewa onyo kali kwa mdomo.
Nitoe pongezi za dhati kwa uongozi wa hospitali ya Kairuki kwanza kwa uharaka ambao taarifa yangu imefanyiwa kazi,na pia kwa kuweza kunipatia mrejesho. Hii imeniaminisha kuwa kwenu msemo wa "mteja ni mfalme" hauishii kwenye mabango tuu. Mwisho kabisa ningependa kuwakumbusha wafanyakazi wa hospitali zote na maeneo yote ya huduma kuwa wateja tunaowahudumia ndio ambao wanasababisha kazi zetu ziwepo, hivyo ni muhimu sana tuwaheshimu. Ahsanteni.
 
wapunguze visu kwa wake zetu bahan wengine wanaweza kuzaa kwa kawaida.
 
Back
Top Bottom