Pongezi za dhati kwa mh Prof Joyce Ndalichako

delako

JF-Expert Member
Oct 6, 2012
2,743
1,492
Habari wana jf,
Kichwa cha habari chahusika, Leo naomba nitoe pongezi zangu za dhati kwako na wasaidizi wako kwa ujumla kwa kufanikisha kuwakamata na kufuta matokeo kwa baadhi ya shule katika mitihani ya darasa la saba 2018.
Tokea uteuzi wako nilitegemea ili pamoja na mengi mazuri ila wizi wa mitihani kwa shule za msingi ulikuwa unafanyika kwa kiwango kikubwa Sana mh.
Ulichofanikiwa ni kwa kiasi ila bado mianya hipo,wizi huu unaanzia kwa watendaji wako huko huko serikalini mh nasema haya kwa maana haiwezekani baada ya uchunguzi matokeo ya wilaya nzima ya chemba mkoani Dodoma yalifutwa na mitihani hyo kutokana na taarifa zenu ni kuwa ilikuwa inasambazwa kwa what's app kwa wakuu wa shule ambao walitengeza group na kupeana mitihani hiyo
Mh ulipoanzia usiishie hapo bado kuna kazi kubwa ya kufanya ila imani nawe ninayo tena kubwa sana na ninaamini unaweza mh,Mitihani ile ilitoka siku 2 mpaka tatu kabla ya siku ya mtihani hiyo ni hatari Sana kwa kizazi tunachokitengeneza mh,na uchunguzi wenu mliufanya kwa kipindi kifupi na kufanikiwa kukamata shule zaid ya 5 mf.Hazina na new hazina ya Dsm,allience na new alliance za Mwanza na shule zote za wilaya ya chemba mkoani Dodoma n.k
Hiyo ni mifano tu mh,mitihani hyo ilikuwa ni set nzima kwa maana ya math, science, kisw,sst na English pamoja na majibu yake.mh angalia vizuri watendaji wako kwa umakini Sana na sio mbaya Kama utabadiri mfumo Kama ambavyo katibu wa baraza alivyosema wakati wa kuanza kwa mitihani ya kidato cha nne na QT.
Mh fuatilia pia walimu wanaofundisha katika shule hasa darasa la mtihani(grd7)
Unakuta mwl Mf A yupo shule Fulani mwaka huu shule ilikuwa ya 1000 Kati ya 10090 nchini kote kwa watahiniwa zaid ya 40, anaenda/wanaenda wao shule Inakuwa 3 bora kitaifa mwaka unaofuata mwl/walimu wale wale wanaenda shule nyingine ambayo haikuwahi hata kuwa ya 3000 wanaenda wao mwezi wa 9 shule hipo 5 bora kitaifa!!!
Kinachofanyika ni kutafuta kwa kila namna kuiba mitihani hyo na wanaiba set nzima maana wakiiba math &science tu,kisw kwa English medium na sst hazitawaacha salama.
Binafsi siamini kwa shule za msingi shule yenye watahiniwa zaid ya 40 kuwa na wastani wa 240/250,je darasa zima ni magenius??? Watoto/wanafunzi wa kitanzania tunawajua na sisi ni mashahidi
Kwa sec yawezekana maana kuna below na kwa shule zilizo smart usipofikisha wastani wewe unachujwa Hakuna bla bla ila kwa shule za msingi kwanza serikali imekataa kukalilisha watoto sasa inawezekana vipi kila mwaka wewe unawatainiwa zaid ya 40 na unakuwa katika 10 bora???Mh WANAKUIBIA MITIHANI .Mh Rais alifanya uteuzi bora kwako kukupa hiyo wizara na ulipoteuliwa tu 100% nilifarijika kuwa elimu yetu imepata mtu na sio wa leo tumefuta B/k and commerce,kesho physics na chemistry zimeunganishwa na kuwa somo moja!!
Mh prof Joyce Ndalichako acha kwingine kuyumbe ila sio katika wizara yako mh.NINA IMANI SANA KWAKO NA WATANZANIA KAMA HATUTA FAIDIKA NA ELIMU UNAYOISIMAMIA BASI TUTAKUWA TUMELAANIWA MH.
Mdau wa ELIMU
Naomba kuwasilisha.
 
Mwambie aliyekutuma siku zake zinahesabika. Baada ya kuona Uzi unaoelezea madudu yake jana , Leo umekuja na swaga ya pambio!!? Umechelewa, atafyekwa tu!
 
Amekulipa kiasi gani cha fedha kumtetea hivyo? Lipi zuri alilofanya? Kuchapisha vitabu sumu vya TET na kuvichoma kila mara ambazo ni kodi za walalahoi zikiteketea ndio la maana? Mh rais anamlia timing tuu, ipo siku mbuyu utang'ooka. Na uje hapa hapa uandike mapungufu yake.
 
Back
Top Bottom