Pongezi Vyeti vya Kuzaliwa kutolewa ngazi ya Mtaa na Kitongoji bure

pombe kali

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
249
489
Miongoni vya vitu nilivyo vifurahia kwenye uongozi wa sasa ambapo huduma za Vyeti vya Kuzaliwa kutolewa kwenye ofisi za serikali ya mtaa/ kitongoji au kata bure kwa watoto chini ya miaka mitano.

Ilikuwa ni utaratibu wa kusikitisha kuona wazazi na watoto wadogo wakitumia siku nzima kusongamana katika ofisi ya RITA, kuandikishwa baada ya kuzaliwa ni haki ya msingi ya mtoto lakini kuna watu waligeuza dili na ku sana kusababisha usumbufu usiokuwa na maana.

Kwa hili natoa pongezi
 
😂😂😂😂😂 watanzania hatuko sawa, ccm wanatuweza sana. Ilitokea wilaya niliyopo miaka miwili au mitatu nyuma, walitangaza hivyo hivyo Kama unavotuambia hapa, Ila walichopewa wale wazazi Ni mfano wa Cheti Cha kuzaliwa kina rangi ya pink hivi, wanaambiwa mtatumia hicho kwenda wilayani mkapewe Cheti orijino.😁 Na utaratibu Ni ule ule,unalipia then unasubiri.ukipata Cheti og uje uweke hapa
 
watanzania hatuko sawa, ccm wanatuweza sana. Ilitokea wilaya niliyopo miaka miwili au mitatu nyuma, walitangaza hivyo hivyo Kama unavotuambia hapa, Ila walichopewa wale wazazi Ni mfano wa Cheti Cha kuzaliwa kina rangi ya pink hivi, wanaambiwa mtatumia hicho kwenda wilayani mkapewe Cheti orijino. Na utaratibu Ni ule ule,unalipia then unasubiri.ukipata Cheti og uje uweke hapa
Hata hivi naona navyo ni vya pinki aiseeee, alafu ni tofauti kabisa na vile OG.
 
Hata hivi naona navyo ni vya pinki aiseeee, alafu ni tofauti kabisa na vile OG.
Serikali inajua wananchi wake Ni zero. Inatugeuza inavotaka. Kama wameamua wawape vyeri og. sasa wanatangaza kuwapa Bure then wanawapa sijui vitu Gani? Tuitoe madarakani hii kampuni ccm
 
Mimi nimetoka RITA jana kumuandikisha mtoto wangu wa miezi miwili, hilo la kuandikisha kwenye vitongoji we ulisikia wapi?
 
Sasa hivyo vyeti awali si vilikuwa vinatolewaa kwa 5000 tu

Watoe dawa bure mahospitalini hapo ndo itakuwa nafuu
 
Mimi nimetoka RITA jana kumuandikisha mtoto wangu wa miezi miwili, hilo la kuandikisha kwenye vitongoji we ulisikia wapi?
Zoezi linandelea mkuu, mkoa niliopo limeanza tarehe sita RITA pia wanatuma jumbe kwenye simu
 
Back
Top Bottom